Uchaguzi 2020 Je, wajua kuwa Mfumo wa Serikali ya Majimbo unatumika kwenye Nchi zenye kukosa Umoja wa Kitaifa?

Ninaomba kura yako iende kwa Magufuli na wagombea wa CCM
 
Huyu Askofu ni mzinifu,mchafuzi,mtumzima anawazalisha mabinti wa watu kisha anawatelekeza.
anajidai kupigania haki wakati kawaacha watoto wake wa nje ya ndoa wanateseka wakiwa na maisha magumu.

keshamzalisha Peace watoto wawili kamuacha kisha kadandia kabinti kingine anafanya nacho zinaa.
Hivi "Yesu" yupo kweli,na anaona hawa warithiwake wanachofanya?
 
Umoja wa kitaifa unapotezwaje kwa kuwa na majimbo?

Hivi sasa hatuna majimbo lakini sehemu zenye wagombea toka upinzani zinapigwa mkwara kuwa zisipochagua mtu toka CCM hazita pata maendeleo.

Je, hatua hiyo siyo kudhoofisha umoja wa kitaifa?

Hofu iko wapi? Kwamba Rais atakosa utii wa majimbo? Bila shaka majimbo hayathibiti vyombo vya usalama kwa namna yoyote.
 


Your browser is not able to display this video.
 
Mimi sio mpiga kura, na ningelikuwa mpiga kura nisingelimpa Magufuli. Kwa lipi kujenga Barabara ba kununua ndege kwa kodi zetu?
Basi utapiga 2025 panapo majaliwa na kumchagua kiongozi ambaye hatumii Kodi zetu kutuleta maendeleo
 
Acha uwongo . Marekani kuna udini ? Marekani kuna ukabila ? Mfumo wa majimbo ni sahihi kwa kusukuma maendeleo kwa kasi zaidi. Kajifunze India uone majimbo yao ya Gujarat, Uttar Pradesh na mengineyo. Kuna ukabIla India ? Shenzi wewe
Acha kuifananisha marekani na kanchi kako ka tanzania.

Marekani,uhuru tu pekeake ina miaka kalibu 300.
Itaifananishaje na tz.
 
Najua unatumika ktk nchi zenye Demokrasia, where no political leader comes into office without VOTES of the people. Mfumo wetu ni wa kikoloni ambapo viongozi mnaletewa na Malkia au Mfalme, bila kumchagua ktk uchaguzi wowote, mnamtaka au hamumtaki ndiyo kiongozi wenu (Dcs, RCs) tunadanganywa eti wabunge ndiyo viongozi wkt hawana mamlaka yeyote hata ya kuamuru choo cha tundu moja kijengwe, zaidi ya kwenda kumbembeleza waziri na rais walete maendeleo na wasipoleta mbunge hana cha kuwafanya. Serikali ya Majimbo ndiyo uhuru na demokrasia ya ukweli
 
Basi utapiga 2025 panapo majaliwa na kumchagua kiongozi ambaye hatumii Kodi zetu kutuleta maendeleo
Nafikiri wananchi tunazo periority zetu, uhuru wetu wa kujieleza , uhuru wetu wa kuchagua na tatu kuhakikisha maisha yetu na vizazi vyetu si maisha ya dhiki. Ndege inagusa vipi maisha ya mtu wakijijini ambaye hana maji na hatimizi mlo mmoja kwa siku?
 
Na China?
 
 
Unafananisha nini kasema wazungu hawana makabila? Kwa Taarifa yako makabila yapo na yanathaminiwa kweli kweli. (Kama Hamna makabila maneno kama tribe, tribalism, ethic, ethinism etc) uunadhani ni kindengereko?
 
Acha kupotosha ukweli kwa kutoa mifano michache isiyo na uhusiano na mfumo wa kuendesha nchi. Katika mifano yako umeiingiza na Ujerumani kwamba kuna majimbo baada ya kuungana na Ujerumani mashariki. Ukweli ni kwamba iliyokuwa Ujerumani ya magharibi ilikuwa na mfumo wa majimbo wakati wote na Ujerumani mashariki ilipounganishwa nao wakaingia kwenye mfumo. Lakini pia umeacha nchi kama uingereza, India Mexico na nyingine nyingi ambazo zinatumia mfumo huu. Ukweli ni kwamba mfumo wa kiutawala tunaotumia sasa hivi hauna tofauti na aliokuwa anatumia mkoloni kwani mfumo huu unaweka mamlaja yote ya nchi pamoja na rasilimali zake mkononi mwa mtu mmoja anitwa Rais akichukuwa nafasi iliyokuwa inakaliwa na gavana. Mfumo huu unamfanya mtu mmoja awe kama mfalme. Ndiyo maana tunapata lugha ya mh. ya kwamba atapeleka maendeleo sehemu zile zinamwunga mkono na kuwanyima kiasi cha kuwasimanga wale wasiomwunga mkono. Watanzania tumegeuzwa ombaomba nchini kwetu. Vipaumbele vya maendeleo yetu vinaamuliwa na mtu mmoja akitumia bunge lisilo na meno.
Pia neno majimbo lisiwe ndo sababu ya kuukataa mfumo. Tukitaka hata majina yanaweza kuwa mikoa. Wakati wa mkoloni aliyaita province ambayo yalikuwa 9. Nyerere akatafsiri na kuyaita mikoa lakini utendaji ukabaki vilevile.
Kwenye madhehebu ya dini ya kikristu wanatumia majimbo yanayoongozwa na askofu. Sijasikia kama wakanisa yamekuwa vipandevipande badala yamesaidia kuwapa waumini madaraka ya kuamua baadhi ya mambo badala ya kila kitu kuamuliwa na papa ama askofu mkuu.
Nimalizie kwa kusema uhuru wa kweli ni ule unaokupa uwezo wa kuendesha mambo yako na kuwa na viongozi wa ngazi zote waliowekwa kwa ridhaa ya wananchi. Na hili linawezekana tukiwa na mfumo unaowezesha hilo bila tuauitaje majimbo ama mikoa
 
Acha kuifananisha marekani na kanchi kako ka tanzania.

Marekani,uhuru tu pekeake ina miaka kalibu 300.
Itaifananishaje na tz.
Kuna mambo yanaweza kufanyika hata kama nchi ina miaka 10 tangu ianze kujitawala. Ukiielewa sera ya majimbo utaamini ninachokuambia. Na kitu kikubwa zaidi hapa ni kwamba, mimi ninachokizungumzia hapa ni kurudisha madaraka kwa wananchi. Si lazima wananchi wa Kagera wachaguliwe mkuu wa mkoa na rais anayekaa Dodoma.

Lakini pia mtu huyu kama atachaguliwa na wananchi ataweza kuwajibika kwao moja kwa moja na si kuwa kichwa ngumu akitumia nguvu ya uteuzi ya rais
 
Kasome vizuri hiyo mifumo,
Halafu vutapicha hali ya nchi yako ilivyo .
Usifuate maneno ya vijiweni.

Mimi naamin watanzania bado hawana elimu ya mifumo ya serkali yao inavyoongozwa.

Leo hata nikikwambia uchore kaomchoro serkali kuu usikute hujui.

Hivyo kunaumuhimu wa elimu kwanza.

Ila kwa mimi nasemahivi!!
Mifumo hii kwa tanzania bado sana.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…