Kwanza kabisa, uzi huu hauna lengo la kukashifu imani au itikadi yoyote na msimamo wa mwandishi haufungamani na upande wowote!
ASILI YA ISRAEL, SAUDI ARABIA na PALESTINE, katika dini kuu tatu, yaani Uislamu(Islamic), Ukristo(Christianity) na Uyahudi (Judaism) anatajwa IBRAHIMU au Abrahamu! Mzee huyu ndiye chimbuko la imani hizi, na ndiyo kitu wanachokubaliana wote.
IKO HIVI Mzee Abrahamu alichelewa Sana kupata mtoto! Mtoto wake wa kwanza alizaliwa kwa kijakazi (House girl) akaitwa ISHMAEL (ISMAIL) baba wa waarabu halisi. Mtoto wa pili (wa kwanza na pekee kwa mama yake) aliitwa ISAKA (isaac) chimbuko la wayahudi wa kweli unataka kujua wakristo walitokeaje? Endelea [emoji3]
KWANINI SAUDI ARABIA ANAIUNGA MKONO ISRAEL? Kwa watu wengi wamekuwa wakishangaa ushirikiano wa Israeli na Saudi Arabia! Mwarabu huyu tofauti na wengine amekuwa akionyesha kuiunga mkono Israel na hii ni sababu ni ndugu wa damu! Hata mzee Ibrahimu alivyofariki alizikwa na wanawe wawili ISHMAEL na ISAKA!!
SASA PALESTINE NI NANI KAMA SIYO MWARABU? Kwenye Bible wana wa Israeli walivyofika nchi ya ahadi walipewa eneo la kutawala, na walizungukwa na mataifa mbalimbali wakiwemo WAFILISTI (philistines au PALESTINIAN) [emoji3]Kuna wakati kwenye biblia historia inaonyesha Israel akipewa kichapo cha mbwa koko na wafilisti, Ushasikia habari za Daudi na Goliathi? Huyu mwamba (Goliath) alikuwa jemedari wa jeshi la Wafilisti [emoji3][emoji3]Ukijaribu kuwasuluhisha unaingilia ugomvi usioujua!
VITA YAO haijaanza Leo! Naam vita ya Palestine na Israel imekuwa ni ya muda mrefu Sana! Kwenye biblia miaka zaidi ya 2000 kabla ya Yesu vita hii ilikuwepo!
Kuna clip mzee wa upako Anthony Lusekelo kalieleza suala hilo kwa upana
Yoshua 9
YOSHUA 9
Udanganyifu Wa Wagibeoni (wapalestina)
1 Basi ikawa wafalme wote waliokuwa magharibi mwa Yordani waliposikia juu ya haya yote, wale waliokuwa katika nchi ya vilima, upande wa magharibi mwa vilima na katika pwani yote ya hiyo Bahari Kuu, hadi kufikia Lebanoni (wafalme wa Wahiti, Waamori, Wakanaani, Waperizi, Wahivi na Wayebusi), 2 wakajiunga pamoja ili kupigana vita dhidi ya Yoshua na Israeli.
3 Hata hivyo, watu wa Gibeoni waliposikia juu ya hayo yote Yoshua aliyowatendea watu wa Yeriko na Ai, 4nao wakaamua kufanya hila: Wakajifanya kama wajumbe wakiwa na punda waliobebeshwa mizigo wakiwa na magunia yaliyochakaa na viriba vya mvinyo vikuukuu vyenye nyufa zilizozibwa. 5Walivaa miguuni mwao viatu vilivyoraruka na kushonwa kisha wakavaa nguo kuukuu. Chakula chao kilikuwa mkate uliokauka na kuingia koga. 6 Ndipo wakamwendea Yoshua kambini huko Gilgali wakamwambia yeye pamoja na watu wa Israeli, “Tumetoka katika nchi ya mbali, fanyeni mkataba nasi.”
7 Basi watu wa Israeli wakawaambia hao Wahivi, “Lakini huenda mnakaa karibu nasi, twawezaje basi kufanya mapatano nanyi?”
8 Wakamwambia Yoshua, “Sisi ni watumishi wako.”
Yoshua akawauliza, “Ninyi ni nani, nanyi mnatoka wapi?”
9 Nao wakamjibu: “Watumishi wako wametoka nchi ya mbali sana kwa ajili ya umaarufu wa Bwana Mungu wenu. Kwa kuwa tumesikia taarifa zake: hayo yote aliyofanya huko Misri, 10 pia yale yote aliyowatendea wafalme wawili wa Waamori mashariki ya Yordani; huyo Sihoni mfalme wa Heshboni na Ogu mfalme wa Bashani, aliyetawala huko Ashtarothi. 11Basi wazee wetu na wale wote wanaoishi katika nchi yetu walituambia, ‘Chukueni chakula cha safari; nendeni mkakutane na watu hao na kuwaambia, “Sisi tu watumishi wenu, fanyeni mapatano nasi.” ’ 12Mkate huu wetu ulikuwa wa moto tulipoufunga siku tulipoanza safari kuja kwenu, lakini sasa angalia jinsi ulivyokauka na kuota ukungu. 13Viriba hivi vya mvinyo vilikuwa vipya tulipovijaza, lakini ona jinsi vilivyo na nyufa. Nguo zetu na viatu vimechakaa kwa ajili ya safari ndefu.”
14 Basi watu wa Israeli wakavikagua vyakula vyao bila kupata shauri kutoka kwa Bwana. 15 Ndipo Yoshua akafanya mapatano ya amani pamoja nao kuwaacha waishi, nao viongozi wa kusanyiko wakathibitisha kwa kiapo.
16Siku ya tatu baada ya hao kufanya mapatano na Wagibeoni, Waisraeli wakapata habari kuwa hao watu ni jirani zao waliokuwa wanaishi karibu nao. 17 Ndipo wana wa Israeli wakasafiri na siku ya tatu wakafika kwenye miji yao ya Gibeoni, Kefira, Beerothi na Kiriath-Yearimu. 18 Lakini Waisraeli hawakuwashambulia kwa kuwa viongozi wa kusanyiko walikuwa wamewaapia kwa Bwana, Mungu wa Israeli.
Kusanyiko lote likanungʼunika dhidi ya hao viongozi, 19lakini viongozi wote wakawajibu, “Tumeshawaapia kwa Bwana, Mungu wa Israeli, kwa hiyo hatuwezi kuwagusa sasa. 20 Hivi ndivyo tutakavyowafanyia: Tutawaacha waishi, ili ghadhabu isije juu yetu kwa kuvunja kiapo tulichowaapia.” 21 Wakaendelea kusema, “Waacheni waishi, lakini wawe wapasua kuni na wachota maji kwa ajili ya jamii yote.” Hivyo ahadi waliyoweka viongozi kwao ikawa hivyo.
22Kisha Yoshua akawaita Wagibeoni na kuwaambia, “Kwa nini mmetudanganya kwa kutuambia, ‘Tunaishi mbali nanyi,’ wakati ambapo ninyi mnaishi karibu nasi? 23 Sasa mko chini ya laana: Daima mtakuwa wapasua kuni na wachota maji kwa ajili ya nyumba ya Mungu wangu.”
24Wakamjibu Yoshua, “Watumwa wako waliambiwa waziwazi jinsi Bwana Mungu wenu alivyomwamuru mtumishi wake Mose kuwapa ninyi nchi hii yote na kuwaangamiza wakazi wake wote toka mbele zenu. Kwa hiyo tuliogopa mno kwa ajili ya uhai wetu kwa sababu yenu, ndiyo maana tukafanya neno hili. 25 Sasa tupo mikononi mwako. Tufanyieni lolote mnaloona kuwa jema na haki kwako.”
26Kwa hiyo Yoshua akawaokoa mikononi mwa Waisraeli, nao hawakuuawa. 27 Siku hiyo Yoshua akawafanya Wagibeoni wapasua kuni na wachota maji kwa ajili ya jamii na kwa ajili ya madhabahu ya Bwana mahali pale ambapo Bwana angepachagua. Hivyo ndivyo walivyo hadi hivi leo.