Je, wajua kuwa wanyama waweza kukupa taarifa kama kuna janga kubwa sana linakuja?

Je, wajua kuwa wanyama waweza kukupa taarifa kama kuna janga kubwa sana linakuja?

Kuku wanaoishi karibu na makaburi husikia sauti ya marehemu akiwaita wakati mnaondoka baada ya kumzika. Inasemekana yale maji ya kibirika yakifika kwenye sikio la marehemu, marehemu huzinduka na kuanza kupokea adhabu za kaburi. Ukiwaangalia kuku wakati huo utaona wameinua shingo zao wanasikiliza
Mh![emoji2211][emoji2211]
 
Nyuma ya nyumbani kwetu kuna dimbwi halikaukagi kila siku usuku ni mwwndo wa vyura kelele hadi kuna kucha je?hii ni ishara gani
Ni ishara ama wewe au mkeo. Mmoja wenu sio muaminifu kwenye ndoa. Ndio maana hao vyura hutoa ishara wakati wa tendo la ndoa
 
Hivi yote mnayoongea ni kweli au mnaongeza na chumvi?
 
NJIWA
Unajua kama njiwa ndio mfugo ambao hautaki kufugwa na mlevi, au watu wanaogombana sana mke na mume fuatilia kuhusu njiwa utayajua usiyoyajua.
msiba unakaribia nyumbani njiwa hawatoki kutwa mzima wanaweka kimya ata kelele hawatoi iyo siku na vikundi kwa uzuni hata kula yao haiyeleweki na mtu akishafariki tayari wakaja watu wengii nyumbani wakaleta fujo na kelele wanaeza kuhama wote na wasirudi tena kuepusha kuhama inataikiwa uwaambie kuwa leo kuna wageni wanakuja kuzika njiwa asubuhi sana wataondoka jioni watarudi.
unawasiliana nao kwa lugha au vitendo?
 
Huwa wanajuaje kwamba hapa ndio kaelekezwa kupeleka ujumbe?
hapo ndipo tunapojiuliza mimi na wewe.
Lakini ni mambo ya ulozi na uganga au tuseme sijui wanabeba maono ya mtumaji maana niliwai kuona mtu mmoja kamfunga kibahasha njiwa alafu anamshika na kumwelekeza anayoyataka apeleke ujumbe na majibu tuliyapata siku ya pili.
 
unawasiliana nao kwa lugha au vitendo?
Hapana sio kwa vitendo,wanafanya hivi asubuhi mapema mda wa kutoka nje mwenye njiwa anaenda kuwaambia kwa sauti uku anawapa chakula, mf. Unaeza kuwaambia "kuleni chakula mapema leo kuna wageni wengi wanakuja kwenye shughuli ya fulani hapa nyumbani kutakuwa na kelele"
Wakimaliza kula hutomwona njiwa kutwa nzima jioni wanarudi.
Nilimuona bibi yangu akifanya hivyo tena yeye akiongea kilugha chake.
 
Kuna wadudu weusi wakubwa zaidi ya sisimizi wanapenda kuwinda kwenye vichuguu, inasemekena ukionana nao wamewinda sana wanawdudu wengi ni baraka sana kwako.
 
Kuku wanaoishi karibu na makaburi husikia sauti ya marehemu akiwaita wakati mnaondoka baada ya kumzika. Inasemekana yale maji ya kibirika yakifika kwenye sikio la marehemu, marehemu huzinduka na kuanza kupokea adhabu za kaburi. Ukiwaangalia kuku wakati huo utaona wameinua shingo zao wanasikiliza
Hakuna kitu kama hicho
 
Kuna wadudu weusi wakubwa zaidi ya sisimizi wanapenda kuwinda kwenye vichuguu, inasemekena ukionana nao wamewinda sana wanawdudu wengi ni baraka sana kwako.
hata sisimizi ukiona wamejaa chumbani kwako ujue utapata hela.
 
Na je nzi wao wakiwa wengi wanatoa ishara gani ?
 
Wengine wanafata uchafu wa mabaki ya vyakula mkuu, haiwezi kuwa ishara ya uchafu.?
hapana. mimi mara nyingi nikiwaona sisimizi wengi ghafla najua tu hela inakaribia kuingia. yani huwaga wanatokea ghafla halafu baada ya muda wanapotea.
 
Kila alichokiumba Mwenyezi Mungu kina kazi yake maalumu ambayo binadamu mara ingine kuijua yaweza chukua karne.

Wanyama huwa wana uwezo wa kujua janga kubwa sana linapotaka kuja. Kwa mfano, kondoo kama kuna radi inataka kupiga chini, huwehuka na kuanza kukimbia huku na kule na kugonga miti kwa kichwa chake akikupa taarifa kuwa radi yaweza shuka eneo hilo chukua tahadhari upesi kama ulikaa chini ya mti mvua ikinyesha unatakiwa utoke haraka ukae sehemu ya wazi kujinusuru na radi ambayo hupenda kupiga kwenye miti.

Kukiweko joka kubwa karibu au mwanga Mchawi mbwa huwa wanabadilika tabia na kuanza kutoa milio fulani hivi isiyoeleweka kutoa taarifa kuwa kuna kitu cha kutisha tishio kiko karibu.

Mengine yasikilize kwenye hii video uone maajabu ya wanyama kupata taarifa za majanga makubwa mapema na kuziwakilisha kwa binadamu lakini kutokana na binadamu kuwa na uelewa mdogo taarifa hizo ambazo binadamu angezingatia maafa yangeweza kuepukika zinashindwa kumsaidia binadamu matokeo yake mamilioni ya watu kuangamia pasipo sababu.

​
Hata kuku wa kienyeji kama kuna hatari hasa ya mdudu mbaya kama nyoka anaeingia ndani kuna mlio anatoa
Kanga wa kufuga ndio kabisa ana machale mno
Punda wa kufuga ndio kabisa ndio maana wafugaji hawaachi
Ndege porini pia kuna mlio akitoa anaashiria hatari
 
hapo ndipo tunapojiuliza mimi na wewe.
Lakini ni mambo ya ulozi na uganga au tuseme sijui wanabeba maono ya mtumaji maana niliwai kuona mtu mmoja kamfunga kibahasha njiwa alafu anamshika na kumwelekeza anayoyataka apeleke ujumbe na majibu tuliyapata siku ya pili.


Hili suala huwa najiuliza sana sipati jibu.
 
Back
Top Bottom