hapa unatakiwa kufafanua nani alikuwa Privity to the contract? maana waliosaini wote wawili walikuwa ni wahusika wakuu wa huo mkataba, sasa anaye ingia hapo nu kuwa si muhusika katika huo mkataba ni nani? Karume au Nyerere? maana kuwa privity to the contract ni pale mtu kudai haki katika kitu ambacho si muhusika mkuu katika mkataba.3. Mkataba wa Kimataifa ni nini, una sifa gani na Jee Muungano watu ni mkataba wa kimataifa?.
Mkataba wa Kimataifa, ni mkataba kati nchi moja na nchi nyingine, au mikataba yote ya jumuiza za kimataifa ambayo nchi ama hutakiwa kuridhia, au kulazimishwa kuiheshimu hata kama haikuridhia. Mikataba hii au itifaki mbalimbali (protocals), hupaswa kuridhiwa kabla haijawa sheria kwa nchi husika.
Mfano Tanzania iliridhia mkataba wa mahakama ya kimataifa ya Biashara, ICC. Dowans iliposhinda ile kesi, imepaswa kuisajili hukumu hiyo kwenye mahakama zetu (ratification), ili hukumu hiyo igeuke sheria zetu, (domestic law) na kutekelezwa. Watu humu walipiga sana kelele, nilipouangalia mkataba ule humu jf, nikawaambia wana jf wenzangu, hatuna pa kutokea, tozo ile italipwa tuu mara baada ya tozo hiyo kusajiliwa, kinachoendelea sasa ni delaying tactics ambayo nayo tutailipia dearly!.
Muungano kati ya Tanganyika na Zanzibar, ni mkataba halali wa kimataifa wenye sifa muhimu za mkataba, japo una mapungufu mengi kubwa likiwa ni kitu kinachoitwa "Privity of Contrac" ambapo mkataba ulikuwa kwa lugha ya Kiingereza na signatory mmoja alikuwa msomi anaejua kusoma na kuandika kiingereza, wakati signatory wa pili hakujua kusoma, kuandika wala kiingereza, hivyo alisaini kwa dole gumba!.
Ufafanuzi zaidi kuhusu Muungano kuwa ni mkataba wa kimataifa, unapatikana pia katika ukurasa wa kwanza wa andiko la
Prof. Shivji kwenye kitabu cha "The Legal Foundation of the Union in Tanzania and Zanzibar Constitution, DUP, 1990.
Kwa faida ya wasoma kimombo, tembelea
THE UNION BETWEEN TANGANYIKA AND ZANZIBAR
Pasco...point of information please, zingatia hii;
Ni katiba ya mwaka 1980 iliyounda Baraza la Wawakilishi na kuwezesha uchaguzi wa kwanza tokea mapinduzi ya mwaka 1964. Lazima tusisahau kuwa mara tu baada ya mapinduzi, Jamhuri ya Unguja na Pemba iliyoanzishwa haikuwa na katiba, haikuwa na bunge na haikuwa na baraza la Mawaziri, mihimili hii yote ilipigwa marufuku na majukumu yake yote kukasimiwa kwa Baraza la Mapinduzi kwa njia ya "decree".
Nafikiri kosa kubwa linalofanywa na wengi ni kushindwa kuzingatia tofauti katika majukumu na taratibu kiutendaji kati ya iliyokuwa Baraza la Mapinduzi la 1964 na Baraza la Wawakilishi la 1980 tunapojadili kuridhiwa kwa Muungano na vyombo hivi viwili. Tanganyika tulikuwa na vyombo vilivyoendeshwa kwa kwa misingi ya katiba rasmi ya nchi tofauti na Zanzibar iliyokuwa chini ya constitutional decree.
Mwanakijiji, huyu jamaa sijui kama anajua anachoongelea au anachanganya mambo...hapa tunamtaka aseme ni chombo kipi huko Zanzibar kilitakiwa (kiutaratibu) kiridhie Muungano mwaka 1964 na hakikufanya hivyo. Asiongelee vyombo ambavyo havikuwepo wakati huo na kwa nini hata vilipokuja kuundwa miaka mingi tu baadaye havikuhoji hadi leo. Tunamsubiri Pasco tena kwa hamu.Mag3, ndio maana wengine tunasubiri hilo somo maana hadi hivi sasa hakuna mahali popote ameonesha kuwa Muungano haukuwa umeridhiwa Zanzibar.
Labda nianze
Pasco, usijiumize sana babangu, unajikamua bure Kwa nondo unazotaka kujikunja nazo .. Kiini cha suluhu umeshakigusia kwamba serikali haiwezi kufanya maamuzi yake pasipo kuwauliza wananchi wake, Na hii ni Kwa kupitia kura ya Maoni..
Nadhani kuna dhana kwamba Upande mmoja wa Muungano hawautaki uchumba huu.. Kwa upande wa Bara wananchi wengi hawana uelewa chanya Wala hasi kuhusu muungano .. Wanachojua Zansibar hawatutaki sisi wabara.. Kwa mantiki hiyo kuna Hoja ya baadae ya kujadili mfumo wa upigaji kura..
Bara yenye wakazi zaidi ya milioni 48 sasa Na Zanzibar yenye wakazi milioni 1.2 ambao ni asilimia 2.4 ya wakazi wa inayoitwa JMT, kura lazima itakuwa Na uwalakini.. Kama watu wote Zanzibar watapiga kura ya kuukataa Muungano, na wakazi milioni 3 tu wa bara wakaukubali, je Hoja ya muungano itabaki MTAMBUZI?
nadhani labda mjadala makini tuuelekezee kwenye suluhisho la nini kifanyike Na sio uhalali Wa Muungano..
Kama Muungano una madudu, kwanini madudu hayo yasimwagwe hapa Na tukayadadavua na kupata suluhu linaloweze kuwa msaada Kwa viongozi ambao wanaumiza vichwa Na mzimu huu unaoitwa MUUNGANO?
Tatizo la Pasco ni kwamba anataka kujaribishia taaluma ya sheria hapa jamvini, ndio maana hataki kuuacha mjadala uwe huru na kuja na vikwazo kibao........mara msiniulize maswali, oh nitajadiri kila kipengere.........., kuna puppets wa .........., Kwa kweli hana majibu ya "contraversial issues" anazoziibua zaidi ya ubabaishaji tu.Mwanakijiji, huyu jamaa sijui kama anajua anachoongelea au anachanganya mambo...hapa tunamtaka aseme ni chombo kipi huko Zanzibar kilitakiwa (kiutaratibu) kiridhie Muungano mwaka 1964 na hakikufanya hivyo. Asiongelee vyombo ambavyo havikuwepo wakati huo na kwa nini hata vilipokuja kuundwa miaka mingi tu baadaye havikuhoji hadi leo. Tunamsubiri Pasco tena kwa hamu.
kwani tanganyika iliridhia muungano?
Pasco...point of information please, zingatia hii;
Ni katiba ya mwaka 1980 iliyounda Baraza la Wawakilishi na kuwezesha uchaguzi wa kwanza tokea mapinduzi ya mwaka 1964. Lazima tusisahau kuwa mara tu baada ya mapinduzi, Jamhuri ya Unguja na Pemba iliyoanzishwa haikuwa na katiba, haikuwa na bunge na haikuwa na baraza la Mawaziri, mihimili hii yote ilipigwa marufuku na majukumu yake yote kukasimiwa kwa Baraza la Mapinduzi kwa njia ya "decree".
Nafikiri kosa kubwa linalofanywa na wengi ni kushindwa kuzingatia tofauti katika majukumu na taratibu kiutendaji kati ya iliyokuwa Baraza la Mapinduzi la 1964 na Baraza la Wawakilishi la 1980 tunapojadili kuridhiwa kwa Muungano na vyombo hivi viwili. Tanganyika tulikuwa na vyombo vilivyoendeshwa kwa kwa misingi ya katiba rasmi ya nchi tofauti na Zanzibar iliyokuwa chini ya constitutional decree.
unataka kusema zanzibar hakuna serikali na wala haikuwepo hapo mwanzoHata kama Tanganyika iliridhia , lile lilikuwa ni bunge lililochaguliwa na watu , jee kule Zanzibar, Baraza la Mapinduzi kalichagua nani ?? Na lilikuwa linamwakilisha nani ?? Au nyerere
unataka kusema zanzibar hakuna serikali na wala haikuwepo hapo mwanzo
Kwa maana hiyo huyatambui Mapinduzi ya Januari, 1964, huitambui Serikali ya Mapinduzi iliyoongozwa na Raisi Abeid Karume, na hulitambui Baraza la Mapinduzi. Sasa ipi serikali unayoitambua kabla ya Muungano? Ilichaguliwa na nani na iliongozwa na nani? Hao viongozi wake waliofungwa katika majela ya Nyerere Tanganyika ndio akina nani?serikali iliyowekwa na Nyerere ilikuwepo maana ile serikali iliyochaguliwa na watu ilikuwa imekamatwa na kufungwa katika majela ya Nyerere Tanganyika , wakati huo ni kabla ya Muungano
Kwa maana hiyo huyatambui Mapinduzi ya Januari, 1964, huitambui Serikali ya Mapinduzi iliyoongozwa na Raisi Abeid Karume, na hulitambui Baraza la Mapinduzi. Sasa ipi serikali unayoitambua kabla ya Muungano? Ilichaguliwa na nani na iliongozwa na nani? Hao viongozi wake waliofungwa katika majela ya Nyerere Tanganyika ndio akina nani?
Wala hata usianze kujisuasua, hizi ni rasha rasha tu, wengine tunamsubiria Pasco ashushe nondo alizoahidi tumpe vidonge vyake.
mimi nikiyatambua nisiyatambue ndio iwe nini humu JF ???UKWELI KITU CHENGINE NA KUTAMBUA KITU CHENGINE, HEBU WAULIZE HAO WANAOKUFUNDISHA NI NANI ALIMCHAGUA KARUME HATA AKAWA RAISI ??? MAJIBU YA MASUALI YAKO MENGINE SOMA HICHI KITABU LABDA WEWE ULIKUWA HUJAKIONA HUMU JF
Kwaheri Ukoloni, Kwaheri Uhuru! Zanzibar na Mapinduzi ya Afrabia by Harith Ghassany in History
kulikuwa hakuna muda wa kuridhia huo muungano by enactment of laws by the revolutionary goverment? kama hawakuridhia kwa kufanya hivyo lakini wakaendelea kuishi kama wamefanya hivyo, then mkataba ni halali by implication.
mimi nike jifanya ni agent wako na wewe ukaniacha niishi hivyo, then mimi ni agent wako by implication.