wanabodi,
kufuatia chokochoko ya kuuchokoa muungano ilianzishwa na kikundi cha uamsho huko zanzibar, zimeanza kutolewa hoja mbalimbali ikiwemo watanzania tupewe fursa kuujadili muungano na ikibidi ipigwe kura ya maoni kuwauliza watanzania na wanzanzibari kama wanautaka muungano, jee wanataka muungano wa aina gani, na endapo hawautaki, process ya kuuvunja rasmi aianze.
Wako wengi wanaupenda muungano na wangependa uendelee ila uboreshwe!. Pia wako wanao ona sasa imetosha na muungano uvunjwe!.
Maudhui ya mada hii ni kuwaeleza wanabodi, jambo muhimu liitwalo "kuridhia" ambapo serikali ya tanganyika na serikali zote zilipaswa kuuriidhia huo muungano kwa utaratibu unaitwa "ratification" ambapo ni serikali ya tanzania pekee ndio iliyofanya process ya "ratification", zanzibar, haikufanya!.
Kwa vile zanzibar, haikuuridhia muungano, kama ni kweli zanzibar inataka kujitoa katika muungano wetu huu adhimu, mlango uko wazi, yaani wide open for zanzibar to just walk out, with no regret and no strings attached kwa sababu hawakuuridhia ule mkataba wa muungano, hovyo mkataba huo hauko binding kwao!.
Mada yangu hii inakuwa na sehemu zifuatazo.
1. Kuridhia ni nini (ratification).
2. Rafication hufanyikaje.
3. Mikataba ya kimaifa ni nini? Na jee muungano kati ya tanganyika na zanzibar ni mkataba wa kimataifa?.
4. Process ya ratification kwa upande wa tanganyika.
5. Process ya ratification kwa upande wa zanzibar.
6. Hadaa ya ratification ya zanzibar, ilipangwa na nani na kwa nini?.
7. Kukosekana kwa ratification upande wa zanzibar kunamaanisha nini.
8. Pamoja na kutokuwepo ratification, jee muungano ni halali?
9. A way forward 1:tudumishe muungano?, muungano wa aina gani?.
10. A way forward 2:tuuvunje muungano?. What are the consequences?.
1. Kuridhia, au ratification, ni process inayofanywa kwa nchi husika kuridhia mikataba ya kimaifa ili kuipa uhalali wa kisheria kutumika katika nchi husika. Mfano mzuri ni mkataba wa muungano baina ya tanganyika na zanzibar, tanganyika ni nchi, na zanzibar ni nchi, hivyo ule mkataba wa muungano ni mkataba wa kimataifa.
Jee kila mkataba wa kimataifa ni lazima uridhiwe?. Jibu ni hapana, sio kila mkataba wa kimataifa ni lazima uridhiwe, ili mkataba wa kimataifa uridhiwe lazima mkutaba husika uwe na kipengele kinacholazimisha mkataba huo kuridhiwa. Tukirudi kwenye mfano wetu wa mkataba wa muungano, kipengele cha viii cha articles of union, kinalazimisha process ya ratification lazima ifanyike ili kuuhalalisha mkataba ule.
(viii) these articles shall be subject to the enactment of laws by the parliament of tanganyika and by the revolutionary council of the peoples' republic of zanzibar in conjunction with the cabinet of ministers thereof, ratifying the same and providing for the government of the united republic and of zanzibar in accordance therewith.
nyerere na karume wangeweza kuamua wakishasaini makubali yale iishie hapo, ingekuwa hivyo hivyo hitaji la kuridhia lisingekuwepo!.
2. Ratification hufanyikaje?.
Kwa vile mikataba yote ya kimataifa ni lazima iwe ni ya maandishi, vivyo hivyo, ratifikation lazima ifanyike kwa maandishi na sio kwa kauli.
Kwa bunge letu, masharti ya kuridhia hufanywa kwa mujibu wa kifungu cha 63(3)(e) cha katiba ya jamhuri ya muungano wa tanzania, kinachotamka kuwa, bunge litajadili na kuridhia mikataba yote inayohusu jamhuri ya muungano na ambayo kwa masharti yake inahitaji kuridhiwa na kwa mujibu wa kanuni za bunge, kanuni ya 114(11) ya 2007.
1. Waziri husika huwasilisha mezani kwa spika mkataba husika
2. Spika ataipa kamati husika kupata maoni yake
3. Kambi ya upinzani itapewa fursa ya kuandaa maoni yake.
4. Mkataba huo utatangazwa rasmi kwenye order paper ya siku ya kuwasilishwa
5. Waziri atawasilisha, kisha maoni ya kamati, maoni ya kambi ya upinzani na majadiliano.
6. Bunge litakaa kama kamati kupitia kifungu kwa kifungu
7. Bunge litarudi kama bunge na kuridhia mkataba husika
8. Mkataba huo unakuwa sehemu ya sheria za nchi,
9. Unasainiwa na rais na kutangazwa katika gazeti za serikali gn.
10.ndio unakuwa umeridhiwa, yaani ratified!.
3. Mkataba wa kimataifa ni nini, una sifa gani na jee muungano watu ni mkataba wa kimataifa?.
Mkataba wa kimataifa, ni mkataba kati nchi moja na nchi nyingine, au mikataba yote ya jumuiza za kimataifa ambayo nchi ama hutakiwa kuridhia, au kulazimishwa kuiheshimu hata kama haikuridhia. Mikataba hii au itifaki mbalimbali (protocals), hupaswa kuridhiwa kabla haijawa sheria kwa nchi husika.
Mfano tanzania iliridhia mkataba wa mahakama ya kimataifa ya biashara, icc. Dowans iliposhinda ile kesi, imepaswa kuisajili hukumu hiyo kwenye mahakama zetu (ratification), ili hukumu hiyo igeuke sheria zetu, (domestic law) na kutekelezwa. Watu humu walipiga sana kelele, nilipouangalia mkataba ule humu jf, nikawaambia wana jf wenzangu, hatuna pa kutokea, tozo ile italipwa tuu mara baada ya tozo hiyo kusajiliwa, kinachoendelea sasa ni delaying tactics ambayo nayo tutailipia dearly!.
Muungano kati ya tanganyika na zanzibar, ni mkataba halali wa kimataifa wenye sifa muhimu za mkataba, japo una mapungufu mengi kubwa likiwa ni kitu kinachoitwa "privity of contrac" ambapo mkataba ulikuwa kwa lugha ya kiingereza na signatory mmoja alikuwa msomi anaejua kusoma na kuandika kiingereza, wakati signatory wa pili hakujua kusoma, kuandika wala kiingereza, hivyo alisaini kwa dole gumba!.
Ufafanuzi zaidi kuhusu muungano kuwa ni mkataba wa kimataifa, unapatikana pia katika ukurasa wa kwanza wa andiko la
prof. Shivji kwenye kitabu cha "the legal foundation of the union in tanzania and zanzibar constitution, dup, 1990.
Kwa faida ya wasoma kimombo, tembelea
THE UNION BETWEEN TANGANYIKA AND ZANZIBAR
angalizo.
Unaruhusiwa kucoment chochou wakati mada hii ikiteremka, ila naomba usiniulize kitu chochote kabla sijafika mwisho,
maana sitakujibu ila nikishamaliza sura zote kumi, nitapokea maswali, maoni au mapendekezo.
Natanguliza shukrani.
Pasco.