Je, wajua kuwa Zanzibar haikuridhia Muungano? Ina Maana Gani?

Je, wajua kuwa Zanzibar haikuridhia Muungano? Ina Maana Gani?

Pasco,

Nakupa pongezi sana kwa kutoa darsa zuri sana kwa wengi na nataraji umefungua mambo mengi sana ambayo wengi sana wamekuwa hawayajui ima kwa kutofuatilia historia hizi au kwa kuona mambo yanakwenda sawia na upeleka mzigo wote kwa waZnz ambao ndio wahanga wakubwa sana wa huu mvungano wenu kiuchumi na kijamii.

Pamoja na pongezi zangu lakin kuna kosa moja kubwa sana sio tu kisharia lakin pia kikanuni za kiuandishi wa Habari/ makala zozote. Umetoa suluhisho mwanzoni kabisa wa mada yako. Wewe ulitakiwa uandike kila ulichokijua na kuamini kuwa kipo sahihi sana katika historia ya muungano.

Kumbuka kuwa kalamu ya mwandihi ni sumu kali sana kuliko bomu la nyuklia. Mwandishi siku zote anatakiwa kuandika pasipo kuegemea upande wowote au kuiamulia jamii ifate vile anavyodhani kuwa yeye yupo sahihi. SUMU KUBWA YA UANDISHI NI USHABIKI. Hivyo punguza ushabiki kwa hili.

Kwa vile Zanzibar, haikuuridhia rasmi Muungano, kama ni kweli hizi chokochoko za Uamsho ni uthibitisho kuwa sasa Zanzibar inataka kujitoa katika muungano wetu huu adhimu, kisheria, mlango uko wazi, yaani wide open for Zanzibar to just walk out, with no regret and no strings attached kwa sababu hawakuuridhia ule mkataba wa muungano in then first place!, hivyo mkataba huo hauko binding kwao!.

Hapo juu nilipo underline naona imekupuruchuka ahali yangu. Kwani ulitakiwa usome vizuri sana Katiba ya Muungano na ile ya Znz kuona na kujua masuala ya Muungano yanajadiliwa wapi. Na vile vile ulitakiwa ufahamu kuwa ndani ya bunge la Muungano kuna wabunge wa Znz. Wakti tunasubiri darsa zaidi labda utudokolee kidogo
1. Ni kipengele gani cha sharia ambacho BLW kinaweza kutumia kuujadili muungano wenu ambao umeridhiwa na Bunge la muungano pekee?

2. Je unajuwa kwa mujibu wa sharia za Muungano JMTz masuala yote ya muungano yanajadiliwa na Bunge la Muungano tu chini ya Afisi ya makamo wa Rais wa Muungano?

3. Nani yupo sahihi wa kudai haki zaidi za kuujadili Huo mvungano kati yha Bunge la Muungano na BLM?
 
Wenzetu Wanzanzibari, ndani ya bunge la Katiba, kwa kuridhia katiba hii mpya, automatically sasa mtakuwa ndio mmeridhia rasmi muungano, kwa sababu, ile katiba yenu, itashushwa chini ya katiba ya Muungano, ile process ya rarification iliyokosekana, itakuwa by passed na kura ya maoni kuikubali katiba mpya!.
Nawatakia majadiliano mema!.

Pasco.
 
Ukiwa Tanganyika unasema
Muungano wa Tanganyika na Zanzibar. Ukiwa Zanzibar unasema Muungano wa
Zanzibar na Tanganyika.

mechi ikichezwa na timu zilezile nyumbani na ugenini jina la mechi linatofautina. timu ya nyumbani ndio hutajwa kwanza.
 
Pasco,

Nakupa pongezi sana kwa kutoa darsa zuri sana kwa wengi na nataraji umefungua mambo mengi sana ambayo wengi sana wamekuwa hawayajui ima kwa kutofuatilia historia hizi au kwa kuona mambo yanakwenda sawia na upeleka mzigo wote kwa waZnz ambao ndio wahanga wakubwa sana wa huu mvungano wenu kiuchumi na kijamii.

Pamoja na pongezi zangu lakin kuna kosa moja kubwa sana sio tu kisharia lakin pia kikanuni za kiuandishi wa Habari/ makala zozote. Umetoa suluhisho mwanzoni kabisa wa mada yako. Wewe ulitakiwa uandike kila ulichokijua na kuamini kuwa kipo sahihi sana katika historia ya muungano.

Kumbuka kuwa kalamu ya mwandihi ni sumu kali sana kuliko bomu la nyuklia. Mwandishi siku zote anatakiwa kuandika pasipo kuegemea upande wowote au kuiamulia jamii ifate vile anavyodhani kuwa yeye yupo sahihi. SUMU KUBWA YA UANDISHI NI USHABIKI. Hivyo punguza ushabiki kwa hili.

Hapo juu nilipo underline naona imekupuruchuka ahali yangu. Kwani ulitakiwa usome vizuri sana Katiba ya Muungano na ile ya Znz kuona na kujua masuala ya Muungano yanajadiliwa wapi. Na vile vile ulitakiwa ufahamu kuwa ndani ya bunge la Muungano kuna wabunge wa Znz. Wakti tunasubiri darsa zaidi labda utudokolee kidogo
1. Ni kipengele gani cha sharia ambacho BLW kinaweza kutumia kuujadili muungano wenu ambao umeridhiwa na Bunge la muungano pekee?

2. Je unajuwa kwa mujibu wa sharia za Muungano JMTz masuala yote ya muungano yanajadiliwa na Bunge la Muungano tu chini ya Afisi ya makamo wa Rais wa Muungano?

3. Nani yupo sahihi wa kudai haki zaidi za kuujadili Huo mvungano kati yha Bunge la Muungano na BLM?
Mkuu Barubaru, leo ndio naiona hii!, kwa vile hii mada iliishia katikati, Tume ya Warioba imeikamilisha!, Wajumbe wa Bunge la Katiba, watatoka na katiba mpya, ikiishapigiwa kura ya maoni, huo sasa ndio mkataba mpya wa Muungano wetu!.
Pasco
 
Ahsante mkulu.

tuombe mola maana naona issue ya muungano ni kaa la moto. Mkataba wa muungano kizungu mkuti. Sitta anasema sahihi ya Nyerere na Msekwa zimechezewa, Mwanasharia mkuu znz hajawahi kuuona, Chief minister znz Nahodha hajapata kuuona, Katibu wa bunge anasema upo Dar na ni vigumu kuupeleka Dodoma, MSEKWA upo UN, na UN wamesema katika kumbukumbu zao hawajawahi kuupokea.

Sasa tujiulize upo wapi?

sasa naanza kuelewa sababu zilizomfanya nyerere kuwa mkali pale watu walipokuwa wanataka kujadili muungano,alikuwa anawapa majina yote mabaya na kuwa potray vibaya kwa umma....kuna watu waliitwa wahuni....kuna watu waliitwa wajinga...wapumbavu, there are more serious issues which will emerge out of this....taking into account nyerere alimpiga chini kikwete kwenye urais dhidi yya mkapa,now kikwete is here to wipe nyerere's legacy in the history of this nation,the last thing which stands is the union,but it seem to be a house built by using ice bricks,with rising temperature,it will melt away
 
Duh Pasco umeshusha nondo za nguvu, nadhani wengi wetu huku hata kuzisoma imekuwa issue kwa sababu ya kutaka vitu vrahisi. Hongera Pasco sijui unaandika dissertation ya Muugano huu fake
 
Mapinduzi ya Zanzibar yaliongozwa na Field Marshal John Okelo wakati Karume anakula urojo Mchamba wima...No wonder Karume akalazimika kukubaliana na Julius Kuungana akiogopa Credit na heshina ambazo Okelo angezipata kwa Wa Zanzibar...Huyu ndie Baba Ndie Baba wa Taifa la Zanzibar

Pasco

kwa faida ya wengi.
Hebu tueleze historia ya John Okelo na namna alivyoongoza mapinduzi ya Zanzibar wakati Karume yuko Mchamba wima akila urojo
 
Last edited by a moderator:
At this point and stage its like a grown-up man asking his parents to furnish him with their binding marriage certificate to prove that their marriage was genuine....a waste of time...especially when i viewed 'zanzibar revulution 1964 Video taken by KAR plane from the google
 
sasa naanza kuelewa sababu zilizomfanya nyerere kuwa mkali pale watu walipokuwa wanataka kujadili muungano,alikuwa anawapa majina yote mabaya na kuwa potray vibaya kwa umma....kuna watu waliitwa wahuni....kuna watu waliitwa wajinga...wapumbavu, there are more serious issues which will emerge out of this....taking into account nyerere alimpiga chini kikwete kwenye urais dhidi yya mkapa,now kikwete is here to wipe nyerere's legacy in the history of this nation,the last thing which stands is the union,but it seem to be a house built by using ice bricks,with rising temperature,it will melt away

Waarabu tuna msemo mmoja ''NI RAHISI SANA KUWADANG'ANYA WATU, LAKIN NI VIGUMU KUWAAMBIA WATU KUWA MUMEDANG'ANYWA''.

Sasa ukweli unadhihiri na kumuona huyu baba alivyokuwa laghai na alisimamia kulinda uwongo wake mpaka umauti wake.

JAMANI HATI YA MUUNGANO IPO WAPI kwani hata katibu wa BLM anasema hana na hajawahi kuiona zaidi ya kuisikia.

At this point and stage its like a grown-up man asking his parents to furnish him with their binding marriage certificate to prove that their marriage was genuine....a waste of time...especially when i viewed 'zanzibar revulution 1964 Video taken by KAR plane from the google

Wazungu wamasema '' in order to build something strong , it helps to start with best and possible materials''

SASA MSINGI WA MUUNGANO WENU MBOVU SANA laazima ufukuliwe na kujengwa upya kama itawezekana. Kwani kwa kuutazama utaona muungano uliwekwa na viongozi kwa faida ya viongozi na sio na wananchi kwa faida ya wananchi.

Pole sana

Bunge la KATIBA MPYA linaahirishwa kupisha bunge la bajeti...... Kwi... Kwi... Kwi... Kwi.....
 
kwani MKATABA WA MUUNGANO UMESHAONEKANA?

Maana Sita ameanza kuhaha kuutafuta na mepita mpaka kwa viongozi wa dini kujisalimisha. Tukumbuke kuwa ni umahiri mkubwa sana kuvunja nguvu za adui yako bila kutumia nguvu.

2/3 ya kura ya maamuzi huko dodoma na kwenye kura ya maoni ndio utakuwa mwisho wa yote.

ZNZ HURU ILEEEEEEEEEEEEEEEEEEE

Ndugu zangu, kwa nguvu zake Mungu tutavuka haya majaribu salama. Naamini jk hayupo ku-wipe jk's legacy kama mchangiaji mmoja alivodai. Natumaini tutavuka salama!
 
Ndugu zangu, kwa nguvu zake Mungu tutavuka haya majaribu salama. Naamini jk hayupo ku-wipe jk's legacy kama mchangiaji mmoja alivodai. Natumaini tutavuka salama!

Ndio salama kwa zanzibar yenye mamlaka kamili.
 
8. Pamoja na kutokuwepo ratification, Jee Muungano ni halali?....

20.Kupitia hoja hizo na nyingine ambazo sikuzitaja, Mimi Pasco wa JF, kwa Mamlaka niliopewa na Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Chini ya Kifungu cha "Freedom of Expressions", Sasa Natamka Wazi kuwa Muungano Kati ya Tanganyika na Zanzibar, Haukuwa Ratified Properly in Zanzibar!. Ila pia Nasisitiza, Muungano Huu ni Halali, japo ulikosa uhalali kwa njia ya Expressly in Zanzibar, umepata uhalali huo Impliedly!.

Natanguliza shukrani.

Pasco.

Leo ndio Sikuu ya Muungano, japo hati halisi za muungano, hatimaye zimetolewa huko zilikofichwa kwa miaka 50, bado kuna maswali bila majibu kuhusu hati hizo,
  1. Kwa nini zilifichwa miaka yote 50 na kuja kuibuliwa sasa?!.
  2. Kwa nini hakuna hati Zanzibar, wakati zilisainiwa hati mbili ya Tanganyika na Zanzibar?, kulikopelekea Wanzanzibari kwenda mahakamani kuidai hati yao?!.
  3. Kwa nini hati hiyo haikuambatanishwa na sheria ya muungano iliyotungwa tarehe 25/04/1964?!.
  4. Kwa nini hati hiyo haikuambatanishwa na tangazo la kuitambulisha Jamhuri ya Muungano ya Tanganyika na Zanzibar kujiunga UN?!.
  5. What was so special kuhusu hati hiyo, no a sigle copy was made up to 50 years ndipo imetolewa copy?.
Hayo ni maswali tuu, ila pia mimi Pasco wa jf, ni muumini wa serikali moja!.

Nawatakieni sherehe njema za muungano.

Pasco
 
kwani MKATABA WA MUUNGANO UMESHAONEKANA?

Maana Sita ameanza kuhaha kuutafuta na mepita mpaka kwa viongozi wa dini kujisalimisha. Tukumbuke kuwa ni umahiri mkubwa sana kuvunja nguvu za adui yako bila kutumia nguvu.

2/3 ya kura ya maamuzi huko dodoma na kwenye kura ya maoni ndio utakuwa mwisho wa yote.

ZNZ HURU ILEEEEEEEEEEEEEEEEEEE

Mkuu hatimaye zile hati halizi za muungano, zilikuja kufukunyuliwa huko zilikofichwa na kukabidhiwa rasmi kwenye Bunge la Katiba, ila yale yale maswali yangu pale juu bado yapo!.

Nakutakia maadhimisho mema ya sikukuu ya muungano hapo kesho!.

Ahali yangu huo sio Muungano bali ni MVUNGANO.

Kwani ndanimwe kuna malalamiko na manung'uniko lukuki toka kwa wananchi wa nchi hizo mbili. Mvungoano huo utaona unalindwa na kutetewa na viongozi na sio wananchi wa kawaida.

Iko siku haki itasimama na Ulanghai utapotea.

Tuombe kheir

Back
Top Bottom