Je, wajua kwamba Katiba hii mbovu inamruhusu Rais kuteua Watu wa familia yake kushika vyeo mbalimbali?

Katiba mbovu imeanza awamu hii? Wakati wa Paroko hamkuliona hilo?. Wagalatia acheni husda! Mmepaniki!
 
Vetting ni utopolo gani?? Nafasi zote nyeti US lazima watu wake wathibitishwe na kamati husika za bunge la Seneti. Hadi bodi ya posta inathibitishwa na seneti. Washauri wa Rais Marekani sio watumishi Rasmi wa umma.

Bora tu ukae kimya. Yaani mtu kuwa karibu na rais siyo nafasi nyeti?
Hivi unaelewa kweli unachoongea!!?
 
Pamoja na kuhitaji katiba nzuri, pia wananchi wanaojielewa ni muhimu.
Kwa hali ilivyo sasa, mjadala ulivyo, hakuna hoja zenye mashiko kwa wale wanaotetea katiba iliyopo. Hali hii inaonesha kuwa wanaohitaji katiba mpya wana hoja za msingi zaidi.
 
Kwani hao watoto na wajukuu wa Rais wanakuwa ni watanzania au la!?
 
Na anachochotewa CAG hana udhibiti nacho. Ndio matokeo ya rais kugawa pesa kwenye misafara yake kama tissue paper.
 
Ni kweli, lakini pia ukiangalia kuwa katiba nzuri inataka usawa kwa raia wote; haina maana kuwa watoto na ndugu wa rais siyo sawa na raia wengine wanaoweza kuteuliwa na rais.
 
Na mimi na sisitiza katiba ni zuri, hao wenye katiba nzuri wakoje ukilinganisha na sisi ,katiba cannot garantee you good on the tablet
Work had usifuate mkumbwa mtu kupanua mdomo na wew unamuuigilizia
Bahati mbaya wewe ni kipofu na kiziwi. Utasongaje mbele wakati katiba haina uwezo wa kukulinda? Katiba inayo mpa rais uwezo wa kufanya lolote na asiulizwe?
 
Na ikitokea akaondoka anaingia makamu alieteuliwa na rais aliye okota dodo chini ya mwarobaini.
 
Katiba mpya itazuia mtanzania asiteuliwe kushika nyadhifa hizo kama ana qualify eti kwa sababu ana unasaba na raisi? Rais Kenedy wa Marekani alimteua mdogo wake kuwa mwana sheria mkuu wa serikali! Vipi hapo? Maana mnapendaga kupiga USA!
 
Rais Kenedy wa Marekani alimteua mdogo wake kuwa mwana sheria mkuu wa serikali! Vipi hapo? Maana mnapendaga kupiga USA!
Ndiyo maana katiba ya Marekani imebadilishwa mara 27. Sasa kwann CCM hawataki tuibadili ya kwetu ikiwa tunaona Kuna mapungufu?
 
US mara nyingi sana wateuliwa wa Rais wamewahi kukataliwa na Seneti au Rais kubadilisha wateuliwa baada ya kugundua Seneti haitawapitisa.
Unataka mifano hapa au unaweza Google mwenyewe?
Je! Hao waliokataliwa na seneti walikuwa na unasaba na Rais?
 
Hivi kwa Trump ilikuwaje
 
Kwa hiyo Yule Jamaa yetu alikuwa Yuko katika raiti tiraki kuteua ndugu na marafiki Siyo? Hasa Ile kanda pendwa?
 
Kwa hiyo Yule Jamaa yetu alikuwa Yuko katika raiti tiraki kuteua ndugu na marafiki Siyo? Hasa Ile kanda pendwa?
Ndiyo. Kwa likatiba letu hili hata angejaza ndugu wa mkewe serikali nzima Ni sawa tu
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…