Huwezi kujua hao wenye katiba nzuri wanakuzidi nini hadi kwanza unue kama hii katiba sio nzuri. Ukishajua hilo ndio unaweza kuelewa.
Jambo la pili, nataka nikupe mfano mdogo tu wa hii katiba ubovu wake ulipo. Kwenye kifo cha Magufuli hapa ndio hii katiba imeonyesha jinsi ilivyo ya hovyo.
Ni ya hovyo kwa msingi kwamba tutaongozwa na mtu ambae hatukumchagua wala kusikiliza sera zake na hoja zake yeye kama yeye kwa miaka 5. Unatakiwa kujua kua kwenye uchaguzi ambae hua anachaguliwa ni rais, makamo wa rais yuko pale tu kama kukamilisha logistics lakini hua sio wa muhimu na ndio maana nchi nyingine anagombea rais mwenyewe kisha akishinda anateua makamo wa rais.
Kwa katiba nzuri tulipaswa kuitisha uchaguzi ndani ya muda flani tuchague tena rais mwingine na sio hii ya kuokota embe kwenye mnazi. Assume hii nchi urais ukiwa miaka 10 term 1, watu wataongozwa na mtu ambae hawakumchagua kwa miaka 10, hiyo ni hatari sana. Ndio maana unaona hata sasa mama hajui anachokifanya maana ni suprise kwake.