Je, Wajua Kwenye Usafi wa Mwili, Waislamu ni Wasafi Zaidi ya Wakristo?. Waislamu Hujiswafi kwa Maji, Wakristo Kwa Karatasi!, Huku Sio Kujipaka?

Hajui huyu. Anataka kutafuta kusifiwa ujinga na upande wa pili. Halafu kutawaza haiwezi kuwa suala la kuwekewa utaratibu. Biblia haijazungumzia kwenye agano jipya kuwa wakristo watumie karatasi. Jamaa amekurupuka. Anatafuta kick.
Amezungumzia ustarabu wa nchi za kiislaam na nchi za kikristo na ushaidi kaweka ila bado ligi ni mbichi.
 
Aliyoyasema mleta mada ni sahihi.
Mwaka 2015 nilisafiri kuelekea Misri kupitia Addis Ababa Ethiopia kwa Ndege ya Ethiopia airline.
Tulivyofika Addis Ababa tulipumzika masaa mawili kwa ajili ya process ya kubadili Ndege basi nikaingia katika vyoo vya uwanja wa ndege kwa ajili ya kukidhi haja na kutawadha .
Nilichokikuta pale Addis Ababa ndicho hiki hiki alichokieleza mleta mada kwamba vyooni wameweka toilet paper halafu nje ya mlango wa choo ndio Kuna sinki la kunawia mikono na mtambo mdogo wa kukaushia mikono kwa sababu kipindi kile Cha mwisho wa mwaka ilikuwa msimu wa baridi.
Kutokana na hali hiyo ni kweli kwamba wasiokuwa waislamu hawana utamaduni wa kujisafisha kwa maji baada ya kujisaidia badala yake wanaelekeza watu wajifute na makaratasi Kisha wanawe mikono baada ya kutoka chooni.
 
Wewe ni muongo!!. Utamaduni wa kujisafisha kwa kutumia maji baada ya kujisaidia umeletwa na waislamu.
Toka tukiwa wadogo tulichofundishwa shuleni kwenye somo la SAYANSIKIMU ni KUNAWA MIKONO BAADA YA KUTOKA CHOONI na siyo kujisafisha baada ya kujisaidia.
Sisi tuliokwenda madrassa ndio tukifundishwa kustanji kwa kutumia maji baada ya kujisaidia haja kubwa na haja ndogo pia.
 
Nje ya mada ila kwa umuhimu:

Muda ni kitu chenye thamani zaidi duniani. Kila muda unapopita akili yako kama mwanadamu inaelekea uzeeni. Akili iliyozeeka haitabiriki. Laiti tungeweza kusimamisha muda wakati ambapo akili si ya kitoto na pia si ya kizee tungetumia nyakati hizo kufanya mengi ya maana, tatizo hatuwezi kusimamisha muda. Ule muda ambao akili yako haijazeeka na si ya kitoto utumie vizuri sana sababu ukipita umepita na uelekeo ni kuwa na AKILI YA KIZEE ISIYOTABIRIKA.
 
Kaka mkubwa kachemsha...

Wakristo wanatumia maji kutawadha...

Wanaotumia TP ni tabia tu za baadhi ya watu ambao kwenye makuzi yao wamelelewa hivyo kutokushika "kinyesi" wakati wa kuchamba
Nakubaliana na wewe ndio maana nikauliza maana nimepata wageni wengi tu kwangu wa dini nyingine na maji ndio yanatumika mimi nadhani asingesema dini ila ingekuwa tu njia ipi bora kwa sisi wa Tanzania ni maji maana hata huko vijijini mtu anaenda chooni na kopo lake la maji tunaona. Mjadala sio dini hapa.
 
Kweli Ethiopia na sehemu nyingi tu hiyo hali ipo ila sidhani kama ni dini bali ni tamaduni. Tanzania na uhakika hakuna choo bila kukuta maji vijijini, mijini hata nyumba za watu bila kujali dini gani. Wazungu ni tamaduni zao sisi sio zetu. Hoja ina mashiko ila sio wa kidini. Hivi vyoo vya makanisani vina maji? mtusaidie kujuwa humu
 
Ukristo unajali zaidi usafi wa kiroho mzebaba
 
Bold ya kwanza pale juu sitakujibu kwa sababu wewe na mnaofanana imani hutaka kila kitu muonekane mmekianzisha nyie,uhuru wa nchi hii mmeuleta nyie pia wengi kiidadi ni nyie so hapo point tatu nimekuachia.

Nikuulize,kwa hiyo Wakristo wanaonawa maji wamesoma madrasa gani?yaani kwa akili zako kabisa unaamini aliyekufundisha kunawa mavi kwa maji ni mwalimu wa madrasa na siyo mama yako mzazi?ulikuwa na mama mchafu duniani hajapata kutokea.
 
Kwa akili za kawaida unadhani inawezekana visiwe na maji?nikisema havina utaamini eti?

Yaani engineer anayejenga bar aweke system ya maji lakini anayejenga Kanisa asiweke hii inaingia akilini?mbona mnakuwa na dharau sana nyie,mna nini cha ziada dunia hii?
 
Labda tuanze na hawa wanaenda na kopo la lita moja ya maji msalani, wanajipaka au wanajiswafi? Maana tunaishi nao wengi kwenye mitaa yetu. Na unapozungumzia usafi nafikiri ungetaja eneo hususa moja maana Daaah ngoja nisiendelee. Ila kama ni swala la kutawaza heko kwao.
 
Suala la kutumia maji au karatasi depends na jamii na malezi na mazingira, ita depend mtu yuko confortable na lipi, si suala la dini

Mzee baba umekuwa unashusha nyuzi iwa kukurupuka, nini kimekupata pascal?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…