Je, Wajua Kwenye Usafi wa Mwili, Waislamu ni Wasafi Zaidi ya Wakristo?. Waislamu Hujiswafi kwa Maji, Wakristo Kwa Karatasi!, Huku Sio Kujipaka?

Je, Wajua Kwenye Usafi wa Mwili, Waislamu ni Wasafi Zaidi ya Wakristo?. Waislamu Hujiswafi kwa Maji, Wakristo Kwa Karatasi!, Huku Sio Kujipaka?

PASKALI I never thought ungekuja na mada ya namma hii.. Well pengine ni aina yako ya uandishi lakini kwa mtazamo wangu utafiti wako una walakini mkubwa

Mimi ni mtembezi sana na nakutana na watu wao kaliba zote.. Wa hali za juu
Was hali za kati
Wa hali za kishua
Wa hali za kawaida
Wa hali za chini
Wa kabila mbali mbali
Wa imani tofauti
Wa mataifa tofauti na mbali mbali
Ishu ya usafi ni swala la binafsi sana lisilohusiana kabisa na dini

Matumizi ya maji kwenye dini kwa ajili ya kujitakasa na kujiswafi ni tofauti kabisa na ulichoandika hapa
Nimeshakutana na watu wengi sana ni wasafi sana wa mwili kiasi kwamba hata akikojoa anajitawadha.. Lakini haohao
Wamefuga minywele ya aina zote
Wana magaga
Hawaogi mwili mzima
Sehemu wanazoishi ni majanga kwa uchafu
Sehemu wanazolala acha tu
Vyoo vyao nknk
Alichoandika Paschal ni kile alichokiona katika viwanja vya ndege vya nchi alizotembelea! Hali ya uwanja wa ndege inatoa taswira ya nchi husika Wana ustaarabu wa aina gani.
Sasa wewe unatutajia watu wasiooga wenye magaga miguuni ambao kiuhalisia ni watu wa vijijini wavaa yeboyebo ambao uchumi wao unategemea aidha ashinde porini akiwinda na au akichunga mifugo yake au ashinde shambani akihangaika na jembe la mkono!
Mtu wa aina hii inapokuwa kiasi kidogo Cha maji anayoyapata anatenga kiasi kwa ajili ya kujisafisha viungo vyake vya siri baada ya kujisaidia ili isije mabaki ya haja ndogo yakabaki kwenye mwili wake na kimharibia ibada yake mtu huyu ni wakupongezwa kwa namna anavyojitahidi kuwa msafi katika mazingira magumu!
Kwa kumaliza nasema kwamba
KWETU SISI WAISLAMU USAFI WA MOYO, MEILI, MAVAZI NA MAZINGIRA YA KUFANYIA IBADA NI SEHEMU MUHIMU SANA YA MAFUNDISHO YA DINI YETU TUNAYOFUNDISHWA MADRASA NA MISIKITINI.
 
Ni kawaida hata nabii huwa hajisifu ila wewe ni miongoni ma GT wachache wa ukweli humu jf.

Issue sio matumizi ya maji na TP, the issue ni dini zote ni watoto wa baba mmoja na na wanatumia sheria moja ya Musa ambayo imeelekeza matumizi ya maji, nchi za Kiislamu zote wanatumia maji, nchi za Kikristo wanatumia TP only kwenye public toilets, why wakati inajulikana wazi usafi ni kwa maji tiririka, hizo tp zimetokea wapi?. Nchi za Kiislamu zina maji na tp, nchi za Kikristo zinashindwa nini kuweka maji na TP ili kuwa consderate kwa Waislamu na watu wenye preference ya kutumia maji?.
P
. 🙏🏾🙏🏾🙏🏾Hapa nadhani matumizi ya maji au TP ni jambo la kimapokea zaidi na sidhani kama ni alama ya usafi katika ujumla wake
Kuna matumizi na matumizi sahihi ya kwenye kila kitu
Kuna watu wanatumia maji na bado wanabaki na uchafu na kuna watu wanatumia TP na wanajisafisha vilivyo
 
Hii ni mbaya zaidi kwa wanawake, wanawake wasiotumia maji wanapokwenda chooni wana harufu mbaya kuliko wale wanaojisafisha kwa maji.
Waislamu sio kwamba hawatumii tishu, wanatumia maji kisha wanajikausha na tishu. Hapo usafi unakamilika
 
Wanabodi,

Kama kawa kila nipatapo fursa, huja na kwa maslahi ya taifa.

Mimi kama mwandishi wa habari, ni muelimishaji umma, ukiona jambo zuri la jamii fulani, waelimishe na wengine wafuate.

Hii ni mada ya swali Je Wajua Kwenye Usafi wa Mwili, kuna uwezekano Waislamu ni Wasafi Zaidi ya Wakristo?. Waislamu Hujiswafi kwa Maji, Wakristo kwa Karatasi!, Huku Sio Kujipaka?.

Jambo la leo ni usafi binafsi wa mwili, baada ya kupunguza uzito, wenzetu Waislamu na nchi za Kiislamu, wanatumia maji kujiswafi, lakini Wakristo na nchi za Kikisto wanatumia karatasi laini, toilet paper, kujiswafi kwa kujifuta baada ya ile shughuli, hapa nauliza ni kujifuta au pia kujipaka?.

Hizi dini kuu zote mbili, Wakristo na Waislamu, ni watoto wa baba mmoja Nabii Ibrahim, Waislamu ni uzao wa mzaliwa wa kwanza, Ismail, na Wakristo wa ni uzao mzaliwa wa pili, Isaka. Sheria ya Mungu wa dini zote mbili ni sheria moja ya Musa iliyoshushwa kwenye torati.

Kwenye sheria hiyo, Mungu alielekeza namna ya kujiswafi, kabla hujaenda mbele zake na kuelekeza kabisa, lazima unawe kwa maji tiririka!.

Ukristo ulipoingia, wakabadili baadhi ya mambo, ikiwemo kutumia karatasi laini kujiswafi baada ya ile shughuli. Katika pita pita yangu nchi nyingi za Kiislamu, kwenye public toilets zao, kuna maji tiririka, lakini kwenye nchi za Kikristo, kuna TP!.

Sisi Tanzania kwasababu nchi yetu haina dini, public toilets zetu zina both, maji tiririka na TP. Ukisafiri kutokea Dar kwenda Dubai, Doha, Muscat, UAE, kote huko kwenye public toilets zao, utakuta maji tiririka, na TP. Ukienda SA, London, Paris, New York, kwenye public toilets zao, kuna TP only hakuna bomba lolote la maji!.

Japo TP inasafisha, kwa vile ni kavu, inasafisha kwa kupaka, huwezi kulinganisha na maji tiririka ambayo yanasafisha kabisa compared to TP.

Kwa vile sheria ya usafi wa mwili imeelekezwa kidini, na ni Waislamu wanaitekeleza kama Mungu alivyoelekeza, hivyo kuna uwezekano kwenye usafi wa mwili, tukubali tukatae, Waislamu ni wasafi zaidi kuliko Wakristo, na kwa kulijua hilo na umuhimu wa usafi, wanawake wa kisasa wenye kujijali, wanatembea na wipes, na nyumba nyingi za kisasa wanatumia maji tiririka.

Kwa wenzetu Waislamu, wale hata wale wenzetu wao, wakiwa kwenye hali fulani ile, huwa hawafungi na hawaruhusiwi kwenda kuswali Masjid au Msikitini, lakini sikuwahi kusikia hili kwa Wakristu, hivyo wenzetu wale, hata wakiwa kwenye ile hali, wanatinga tuu ibadani mbele za Mungu!, hivyo inawezekana kwenye usafi binafsi, wanawake wa Kiislamu ni wasafi kuliko wanawake wa kikristo?.

Tena usikute usafi huu kwa Waislamu sio usafi tuu wa mwili, ni mpaka moyo na roho, ndio maana wanawake wa Kiislamu wanaweza kuvumilia na kustahimili uke wenza, na ingefanywa survey ya ni wanawake gani akiwa mama wa kambo, anatesa watoto wa aliyemtangulia, a wicked stepmother, mngeshangazwa na matokeo.

Kuna vitu vingi wazungu wametupotosha sisi Wakristo ikiwemo hoja ya mke mmoja, sio mpango wa Mungu, ndio maana nilimpongeza yule Blaza wangu na kumshauri "Pongezi Rais Magufuli Kuwa Mkweli Daima. Tuanzishe Church of Africa, Tuoe Wake Wengi, Tuzae Watoto Wengi?"

Nani aliwaambia wazungu na nchi za Kikristo TP tuu inatosha?.

Nimepandisha bandiko hili kufuatia mimi ni mpenda kula kula vyakula locals kila ninaposafiri, Uliwahi kula vyakula gani kutoka sehemu mbalimbali Duniani ukafaidi? sasa sometimes, tumbo linachafuka ukiwa safarini, inakubidi ujiswafi kwa maji tiririka, tumbo linapokutibuka, ukakuta hakuna maji ni TP pekee ni shughuli, hivyo nimekereka sana na hili!. Hawa wazungu vipi?.

WHO wanapaswa watoe muongozo na maelekezo, public washrooms zote lazima ziwe na maji tiririka na TP, ili wale wa kunawa, wawe huru wanawe na wale wa kujipaka, waendelee kujipaka!.

Paskali
Rejea za mleta mada kuhusu Waislamu na Wakristo
Umepimaje kaka
 
Hii story ina walakini, familia nyingi za Kitanzania TP ni luxury, hawana hizo pesa za kuchezea kununua TP
Nazungumzia huko kwetu wilayani Ngara mkoani Kagera.
Wakristo wa maeneo hayo hawakuwa wakitumia maji wala pia hawatumii tp.
Labda mapadri wa kizungu kwa kuwa kule kuna Jimbo kubwa sana la kanisa katoliki.
Wale washubi na wahangaza akishajisaidia anavaa nguo na kusepa kwenda kuendelea na mishe zake. Hana muda wa kujisafisha kwa njia yoyote. Akiwa mwenye kujali sanasana atatumia majani ya miembe.
Sasa ndio baadhi ya vijana wakawa wanawashangaa sana waislamu wanavyoingia na makopo ya maji chooni wakidhani wakimaliza kujisaidia wanakunywa maji huko huko chooni wakati yale yalikuwa maji ya kujisafisha baada ya kujisaidia.
 
waarabu VS wazungu(mabeberu)

***kwamba waarabu ni watu wazuri sana na wazungu ni mabeberu wabaya sana.
***wazungu(ukristo) =wachafu vs waarabu wasafi+wazuri.

HAWA WAZUNGU TUNATEGEMEA SANA MISAADA NA MIKOPO YAO WANAYOTUPATIA
Kwa hisani ya watu wa zungu mpaka vyoo wametujengea kwenye shule zetu baadhi ya maeneo .
Kwenye afya pia wanatusaidia sana ,maneo mengi wamekuwa wakitusaidia kwa miaka mingi hawa WAZUNGU/MABEBERU.
Hata walipotuletea dini UKRISTO walijenga na shule za mission na hospitali za mission ambazo walisoma dini zote waislamu na wakristo na walitibiwa watu wa dini zote mpaka leo.Sasa kama walifundisha watu wasitawaze uchafu mbona dini zote walisoma shule zao za mission na kutibiwa hospitali zao.
 
Wenzenu kutumia maji ni mfumo wao wa maisha wanaofundishana majumbani.
Wenzetu akina nani?! Si ndio hao ambao wamewahi kuniuliza ikiwa waislamu wakifikwa chooni lazima wapate kiu ya maji?! Nina umri wa miaka 47 na miaka 20 nimeishi na jamii ya wakristo huko kwetu Rulenge wilayani Ngara mkoani Kagera.
Mama yangu (Allaah amrehemu) alisilimu miaka michache kabla mimi sijazaliwa kwa hiyo wajomba zangu na familia zao Bado ni wakristo.
Swala la wakristo kujisafisha kwa maji baada ya kujisaidia limeanza siku za karibuni na ni kwa wakristo wanaoishi miji ya pwani kama Dar, ZNZ , Tanga na Mtwara.
Wakristo waliopo Vijijini kama huko marangu Kilimanjaro au Uyole huko Mbeya hawana habari ya kujisafisha na maji.
 
Wanabodi,

Kama kawa kila nipatapo fursa, huja na kwa maslahi ya taifa.

Mimi kama mwandishi wa habari, ni muelimishaji umma, ukiona jambo zuri la jamii fulani, waelimishe na wengine wafuate.

Hii ni mada ya swali Je Wajua Kwenye Usafi wa Mwili, kuna uwezekano Waislamu ni Wasafi Zaidi ya Wakristo?. Waislamu Hujiswafi kwa Maji, Wakristo kwa Karatasi!, Huku Sio Kujipaka?.

Jambo la leo ni usafi binafsi wa mwili, baada ya kupunguza uzito, wenzetu Waislamu na nchi za Kiislamu, wanatumia maji kujiswafi, lakini Wakristo na nchi za Kikisto wanatumia karatasi laini, toilet paper, kujiswafi kwa kujifuta baada ya ile shughuli, hapa nauliza ni kujifuta au pia kujipaka?.

Hizi dini kuu zote mbili, Wakristo na Waislamu, ni watoto wa baba mmoja Nabii Ibrahim, Waislamu ni uzao wa mzaliwa wa kwanza, Ismail, na Wakristo wa ni uzao mzaliwa wa pili, Isaka. Sheria ya Mungu wa dini zote mbili ni sheria moja ya Musa iliyoshushwa kwenye torati.

Kwenye sheria hiyo, Mungu alielekeza namna ya kujiswafi, kabla hujaenda mbele zake na kuelekeza kabisa, lazima unawe kwa maji tiririka!.

Ukristo ulipoingia, wakabadili baadhi ya mambo, ikiwemo kutumia karatasi laini kujiswafi baada ya ile shughuli. Katika pita pita yangu nchi nyingi za Kiislamu, kwenye public toilets zao, kuna maji tiririka, lakini kwenye nchi za Kikristo, kuna TP!.

Sisi Tanzania kwasababu nchi yetu haina dini, public toilets zetu zina both, maji tiririka na TP. Ukisafiri kutokea Dar kwenda Dubai, Doha, Muscat, UAE, kote huko kwenye public toilets zao, utakuta maji tiririka, na TP. Ukienda SA, London, Paris, New York, kwenye public toilets zao, kuna TP only hakuna bomba lolote la maji!.

Japo TP inasafisha, kwa vile ni kavu, inasafisha kwa kupaka, huwezi kulinganisha na maji tiririka ambayo yanasafisha kabisa compared to TP.

Kwa vile sheria ya usafi wa mwili imeelekezwa kidini, na ni Waislamu wanaitekeleza kama Mungu alivyoelekeza, hivyo kuna uwezekano kwenye usafi wa mwili, tukubali tukatae, Waislamu ni wasafi zaidi kuliko Wakristo, na kwa kulijua hilo na umuhimu wa usafi, wanawake wa kisasa wenye kujijali, wanatembea na wipes, na nyumba nyingi za kisasa wanatumia maji tiririka.

Kwa wenzetu Waislamu, wale hata wale wenzetu wao, wakiwa kwenye hali fulani ile, huwa hawafungi na hawaruhusiwi kwenda kuswali Masjid au Msikitini, lakini sikuwahi kusikia hili kwa Wakristu, hivyo wenzetu wale, hata wakiwa kwenye ile hali, wanatinga tuu ibadani mbele za Mungu!, hivyo inawezekana kwenye usafi binafsi, wanawake wa Kiislamu ni wasafi kuliko wanawake wa kikristo?.

Tena usikute usafi huu kwa Waislamu sio usafi tuu wa mwili, ni mpaka moyo na roho, ndio maana wanawake wa Kiislamu wanaweza kuvumilia na kustahimili uke wenza, na ingefanywa survey ya ni wanawake gani akiwa mama wa kambo, anatesa watoto wa aliyemtangulia, a wicked stepmother, mngeshangazwa na matokeo.

Kuna vitu vingi wazungu wametupotosha sisi Wakristo ikiwemo hoja ya mke mmoja, sio mpango wa Mungu, ndio maana nilimpongeza yule Blaza wangu na kumshauri "Pongezi Rais Magufuli Kuwa Mkweli Daima. Tuanzishe Church of Africa, Tuoe Wake Wengi, Tuzae Watoto Wengi?"

Nani aliwaambia wazungu na nchi za Kikristo TP tuu inatosha?.

Nimepandisha bandiko hili kufuatia mimi ni mpenda kula kula vyakula locals kila ninaposafiri, Uliwahi kula vyakula gani kutoka sehemu mbalimbali Duniani ukafaidi? sasa sometimes, tumbo linachafuka ukiwa safarini, inakubidi ujiswafi kwa maji tiririka, tumbo linapokutibuka, ukakuta hakuna maji ni TP pekee ni shughuli, hivyo nimekereka sana na hili!. Hawa wazungu vipi?.

WHO wanapaswa watoe muongozo na maelekezo, public washrooms zote lazima ziwe na maji tiririka na TP, ili wale wa kunawa, wawe huru wanawe na wale wa kujipaka, waendelee kujipaka!.

Paskali
Rejea za mleta mada kuhusu Waislamu na Wakristo
Kwa huu uzi ulivyo na logic yake ni hakika kuwa huyu Pascal Mayalla ana akili ndogo sana 🙄🙄 toilet paper siyo ukristo wala uislam ni mambo ya mageuzi ya kiuchumi kisayansi na kitekinolojia ...wakristo na waislamu wote walikuwa wanatumia maji miaka ya kale ...hivyo mada imekosewa kilogic ilitakiwa kusema wakristo wameacha kutumia maji kujisafisha na kutumia toilets paper wakati waislam wanaendeleza kutumia kutumia maji...mleta uzi kashindwa kujua kuwa zama zimebadilika sikuizi watu wanatumia toilets paper kisha wanatumia na maji pia..... ndiyo maana hata ujenzi wa vyoo vya kisasa kuna kijibomba cha kisasa cha kukishika mkononi cha kujisafishia tofauti na kutumia kopo... hata kwenye vyoo vya sgr kipo hicho kijibomba ....kazi ya toilet paper siyo kujisafishatu bali na kujikausha majimaji hivyo ni sahihi kutumia maji na toilet paper kwa,pamoja ...kanuni ni moja mbili tatu yaani ukishatoka kujisaidia tumia toilet paper kisha maji kisha tumia tena toilet paper kujikausha maji...badala ya kuponda toilet paper ni vizuri kufuata huu mfumo ulio sahihi zaidi ya kutumia maji tu au kutumia toilet paper tu ...hivyo tuwa fundishe wanao tumia maji tu na wanao tumia toilet paper tu kutumia vyote viwili kwa hiyo formation niliyo sema ya 1..2..3

💥💥THREAD CLOTHER📌📌📌📌
 
Back
Top Bottom