Je, wajua mambo haya 10 kuhusu Tundu Antipas Lissu?

Siku akiamua kuhamia ccm tu wote mtamuona mpuuzi na hana la maana lolote,maana yake mnamsifia mtu kwa sababu na kuona ubora wake kwa sababu tu yupo chadema au yupo kinyume na serikali. Leo Lissu anaonekana ni msomi na mwanasheria mzuri kabisa ila ikitokea kwenda ccm au kuwa kinyume na chadema basi hapo ndipo ataonekana hata sheria zenye hajui.
 
Mimi na nyumba yangu nimeamua tutampigia Lissu kura. Nakuomba na wewe uliyeamua kumpigia lissu kura yako. Wengi wameshaamua umebaki wewe
 
Hauna hoja utakuwa unaifaidi mfumo dhalimu
 
Kumbe huyu fani yake ni uwakili. Sasa anarukia urais atauweza?
Ni wazi kuwa wakili yupo tayari kuipindisha sheria ili kukidhi maslah ya mteja wake. Kwa ujumla wakili ni mtu mjanja mjanja (mlaghai) kwakutumia sheria. Mfano Jambazi limekwiba na limeuwa na ushahidi upo lkn wakili anafanya janja janja hadi linaonekana halina hatia.
 
Hauna hoja utakuwa unaifaidi mfumo dhalimu
Nilichokisema kinahusiana vp na kufaidi mfumo? Nimeeleza ukweli kwamba mnamsifia mtu kisa tu yupo chadema au anapingana na serikali. Tumeona watu kibao ambao walikuwa wakisifiwa uhodari wao mbalimbali ila leo hii wanaonekana ni wapuuzi kisa tu wapo ccm au wanaunga mkono serikali.

Hivyo hata Lissu akitaka aendelee kusifiwa hizi sifa anazopewa basi ni lazima aendelee kubaki hapo chadema ila kinyume na hivyo ataonekana kama Dr.slaa au Zitto.
 
Namba mbili imenistua na ikanifanya nifikirie Mara mbili inakuaje lissu anatuhumiwa kua kibaraka wa mabepari!!!?
Mkuu propaganda za ccm ni za kitoto sana kwa kudhani wote sie ni watoto.
Siku moja nikiwa Tarime miaka kama 10 iliyopita niliuliza habari za Lissu, hakika alielezewa kama shujaa hadi niliogopa! Leo watu wale uwapelekee takataka eti Lissu ni kibaraka wanaweza kukutoboa macho.
 
Alafu anatokea mshamba mmoja chato anajiita mzalendo
 
UONGO MBICHI, Tundu Lisu anadai fedha akikupa huduma ya uwakili na kama unabisha ushahidi upo.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…