Wanabodi,
Kama kawa, leo nimepata fursa kuwaletea makala elimishi ya uchambuzi wangu wa muswada huu wa Sheria ya Uchaguzi wa Rais, Wabunge na Madiwani wa mwaka 2023, kwa swali Je Wajua Muswada Sheria ya Uchaguzi wa Rais, Wabunge na Madiwani 2023 ni Batili?. Je muswada huu ni mvinyo ule ule wa zamani, kwenye chupa mpya?. Muswada huu una nini kipya?, nini kilichobadilika tofauti na zamani?. Huu ni ubatili mtupu, ila ndani ya ubatili huu pia kuna baadhi ya mambo ni mambo mazuri!
Naomba nianze bandiko hili kwa utambulisho
Mwandishi ni mwandishi wa habari na mtangazaji wa kujitegemea kwa kujitolea na Wakili wa kujitegemea, ambaye japo ni mhitimu wa LL.B (Hons) ya UDSM, yeye sio wakili msomi, kwasababu haendi mahakamani, huyu ni wakili mtangazaji na muelimishaji umma kuhusu katiba, sheria na haki, kupitia makala za "Kwa Maslahi ya Taifa" zinazotoka humu JF, baadhi ya magazeti na kipindi cha TV na oline
View: https://youtu.be/b67jqx0GWd8?si=ucNR1r5_kd7rZShI
Nimeanza na utambulisho huo, kwasababu kitendo cha wanasheria manguli, wabobezi na wabobevu, wa serikali wametunga muswada, wamejiridhisha uko ok ndio maana wakauwasilisha Bungeni, ambako nako kuna mabingwa wa sheria, wabobezi na wabobevu nao wakaoona uko sawa na ndio maana wakaruhusu uwasilishwe Bungeni na umeisha somwa kwa mara ya kwanza, halafu akaibuka mtu tuu kuukosoa kwa kuwaambia watu muswada huu ni batili!, lazima watu watajiuliza huyu ni nani?, hivyo huu ni uthibitisho kuwa Tanzania tuna wanasheria wa ajabu sana!. Jambo limeishatamkwa na Mahakama Kuu kuwa ni batili, serikali yetu sikivu inawezaje tena kutuletea ubatili huo huo kwenye hii sheria mpya?!. Hii sio mara ya kwanza kwa serikali yetu kututungia sheria batili, na niliwahi kuuliza
Katiba Yetu Ina Matobo: Serikali Ikikosea, Inashitakika. Je, Bunge na Mahakama Zinapowakosea Watanzania Kama Makosa Haya Tunawashitaki Wapi?, hivyo zinapokea fursa za kubadili sheria, tuzibe kwanza paa letu, tuzibe matobo ili tuwe salama.
Jee inakuwaje madudu haya yakafanywa na wanasheria wetu?. Jibu ni moja tuu, sheria ni fani bahari, eneo ngumu kuliko yote kwenye sheria ni eneo la kutafsiri sheria, kwa Tanzania mamlaka pekee ya kutafsiri sheria ni Mahakama Kuu ya Tanzania, ila naomba kusema wazi hata Mahakama zetu zimekosea kutafsiri baadhi ya sheria zinazokwenda kinyume cha katiba.
Ijue Katiba kwa Jicho la Mtunga Katiba: Mtunga Katiba alimaanisha nini aliposema "Katiba ni Sheria Mama"? Ni kweli Katiba ni Sheria Mama?
Ubatili wa muswada huu, sio ubatili mwingine wowote, zaidi ya ubatili ule ule ninaoupigia kelele humu jukwaani kila uchao, wa serikali yetu kutunga muswada wenye vipengele batili vinavyokwenda kinyume cha katiba ya JMT na Bunge letu Tukufu kuupokea huo muswada batili na ubatili wake na waheshimiwa wabunge wetu kujadili kutunga sheria batili kama mazuzu!
Ubatili huu nimeuzungumza hapa
Kwa vile Mkuu wa nchi ni rais wa nchi, hivyo likitokea tatizo lolote, analaumiwa mkuu wa nchi, na madudu yote hayo yalitokea kabla Rais Samia hajaingia madarakani, hivyo nimemjengea indemnity Rais Samia asilaumiwe kwa madudu haya
Madudu ya ajabu ya ubatili wa Katiba yetu, mabadiliko "fake" ya sheria na Tume ya Uchaguzi, Rais Samia asilaumiwe kwasababu yeye sio mwanasheria!.
Kwa maoni yangu, dhulma kuu ya kwanza na ya msingi ni haki ya kupiga kura na haki ya kupigiwa kura, haki hii iyotolewa na katiba ya JMT ya mwaka 1977, ikaja kuporwa kwa sheria batili ya uchaguzi, Sheria ya Taifa ya Uchaguzi Sura ya 343 ya mwaka 1985 na Sheria ya Uchaguzi ya Serikali za Mitaa Sura ya 292 ya Mwaka 1979.
Mchungaji Mtikila akapinga sheria hiyo mahakani, baada ya Mahakama Kuu ya Tanzania kukibatilisha kifungu hicho batili, kwa kwenda kinyume cha katiba, serikali yetu ikafanya jambo moja kubwa la ajabu sana, au kitu cha ajabu sana!, ikapeleka bungeni muswada wa mabadiliko ya katiba kwa hati ya dharura, ikakichomekea kipengele batili ndani ya katiba ya JMT ya mwaka 1977, hivyo ubatili huo ukachomekewa ndani ya katiba!. Kwanini tutunge sheria mpya ya uchaguzi yenye ubatili ule ule?. Kwanini tutunge sheria mpya yenye dhulma ile ile ya haki kwa Watanzania?!.
Rais Samia baada ya kuingia madarakani, tumemlilia sana kuhusu ubatili huu
Kwenye mada hii pia ninaainisha kwa mukhtaasari, sura zote 10 za sheria hii, ili kuwaelimisha elimu ya uraia, sheria na haki ili tuitumie kikamilifu hii miezi 3 ya kutoa maoni na mapendekezo ya maboresho ya sheria hii.
Muswada huu unatunga Sheria ya Uchaguzi wa Rais,Wabunge na Madiwani ya mwaka, 2023. Kwa ujumla, Sheria hii inaunganisha Sheria ya Taifa ya Uchaguzi, Sura ya 343 na Sheria ya Uchaguzi ya Serikali za Mitaa, Sura ya 292. Hivyo sasa masharti ya uchaguzi wa Rais na Wabunge na Madiwani ni sheria moja na kutekelezwa na mamlaka moja ambayo ni Tume Huru ya Taifa ya Uchaguzi. Hapa ninapendekeza chaguzi zote nchini, uchaguzi wa Rais na Wabunge, Madiwani na Serikali za Mitaa, ufanyike siku moja na kusimamiwa na Tume moja Huru ya Taifa ya Uchaguzi. Hili ni jambo jema!.
Muswada huu umegawanyika katika Sura Kumi.
Uchambuzi wangu wa sura kwa sura na maoni yangu
Karibu
Hitimisho
Maadam sheria batili hii imeisha somwa kwa mara ya kwanza, nashauri tutoe maoni yetu, pili hoja hizi zizingatiwe
Hivyo Bunge la February lije na mabadiliko madogo ya katiba kwa hati ya dharura, tuondoe kwanza ubatili huu ndani ya katiba yetu na sheria zetu ndipo tusome kwa mara ya pili muswada huu!.
Hayamambo ya serikali yetu kututungia ubatili, na kulipelekea Bunge letu likaubariki ubatili huu kuwa sheria, tutaendelea nayo hadi
lini?
Watanzania tutaendelea kusubiri mpaka lini Bunge likitunga Sheria batili na kuuchomekea ubatili huo ndani ya Katiba yetu? Tufanye nini?
na nikasema
Watanzania ni maneno maneno na kulialia, Vitendo 0. Katiba ni maneno tu! Je, 2023 tuendeleze maneno matupu na kulialia au tubadilike tufanye kitu?
Hivyo mambo haya yakiendelea, kiukweli kabisa we'll be left with no option but to do something! (ambacho naomba nisikitaje)!.
Mungu ibariki Tanzania
Paskali