Je, wajua Muswada Sheria ya Uchaguzi wa Rais, Wabunge na Madiwani 2023 ni batili? Ni mvinyo wa zamani, kwenye chupa mpya? Why ubatili huu?

Hiki unachosema nadhani kinaweza kuwa na ukweli kwa 100%. Maana kuna mtu wangu wa karibu alikuwa ni msimamizi wa uchaguzi wa 2020, aliwahi kuniambia hivi hivi.

Eti baada ya watu kuondoka kituoni, walijifungia na kupiga kura za kuwapa ushindi mgombea wa urais wa kipindi hicho kupitia chama tawala, mbunge wa chama tawala, na pia diwani.

Na alisema kabla ya kupiga hizo kura, mgombea urais wa upinzani na mgombea ubunge wake na yule wa udiwani; ndiyo waliokuwa wakiongoza kwa kura nyingi tu.

NB:- Bado msimamo wangu hautabadilika. Maana inauma kushiriki hayo maigizo yanayoitwa uchaguzi. Mambo yakibadilika walau kama ilivyokuwa 2015 kurudi nyuma, nitashawishika.
 
Hiyo tu out of 60m kuwa eti 29m waliojiandikisha kupiga kura , ni wendawazimu mwanaume unayesimamisha vizuri kwenda kusomama kwenye mstari wa kura ukisema unachagua viongozi.
 
Uwe na wananchi 60m kisha wapiga kura wawe 40m, yaani watu wenye 18+ wawe wengi kuliko waliochini kisha useme kuna uchaguzi?!
 
Mungu ataingilia kati kama Kwa yule.....
No, kuna baadhi ya mambo ya Kaisari Mungu humwachia Kaisari mwenyewe!, dhulma hii imekuwepo toka 1992, hivyo Mwinyi kaitumia Mungu hakuingilia, Mkapa kaitumia, Mungu hakuingilia, JK kaitumia, Mungu hakuingiliwa, JPM kaitumia, Mungu hakuingilia na hata Samia akiitumia, Mungu hataingilia, ila Samia akiiondoa dhulma hii, atabarikiwa sana!. Samia ni mpango wa Mungu kwa Tanzania: Kwa hili atabarikiwa, Taifa litabarikiwa. Asante Mungu kwa Samia, Mungu mbariki Samia, Mungu ibariki Tanzania!
P
 
Huo ni uongo, kura zenu nyinyi msiojiandikisha na msiopiga kura zilipigwa usiku kucha kabla ya uchaguzi, kesho yake ilikuwa ni kazi ya kuziunganisha tuu ili kuzijazilizia tuu kwenye balot boxes !. Kura zote zinahesabiwa hapo kituoni baada ya kupiga kura na matokeo yanabandikwa kituoni usiku huo huo hivyo hiyo ya kupiga kura baada ya uchaguzi ni uongo!. Kama eligible voters mngejiandikisha na wote mkajitokeza, then hizo mlizopigiwa zisinge pigika!. The game is played kwenye daftari la kupiga kura.
P
 
Mkuu Pascali
Imenichukua nusu kutwa ya leo kusoma na kuchakata hoja hii uliyotuwekea hapa.

Kimsingi nakubaliana nawe kwenye huu ukweli kwamba muswada wa sheria hii ya uchaguzi una kasoro laanifu zinazohitajj kutakaswa kwa kubatilishwa ili zirejewe na kubadilishwa ziendane na maudhui mazima ya hitaji la demokrasia nchini.

Katika issue ya mgombea kudhaminiwa na Chama ninaona siyo sawa.

Je unaonaje mimi na wewe na yeyote yule tukiungana kwenda huko mahakamani kuzuia ama kupinga kupitishwa kwa muswada huu kuwa sheria.

Je Katiba inatulinda kiasi gani kwenye kutetea demokrasia?
 
Mkuu Msanii, kwanza naunga mkono hoja, kwenda Mahakamani, ila sio kupinga kupitishwa kwa muswada huu kuwa sheria, bali kuiomba Mahakama Kuu kutoa tafsiri ya ubatili wa muswada huu. Mfumo wetu wa mihimili kutoingiliana, Mahakama haiwezi kuliingilia Bunge kwenye utungaji sheria, hivyo kwa vile muswada huu bado sio sheria, ni muswada tuu, huwezi kufungua shauri kuushitaki muswada ila ukiisha pitishwa na Bunge kuwa sheria, unaweza kufungua shauri kuupinga sheria hiyo.

Mfumo wetu wa haki hauko vizuri kabisa!, katiba yetu ina matobo kibao!, ni serikali tuu ndio pekee inaweza kushitakiwa Mahakamani isipo tenda haki, lakini Bunge na Mahakama zisipo tenda haki, haziwezi kushitakiwa popote! Katiba Yetu Ina Matobo: Serikali Ikikosea, Inashitakika. Je, Bunge na Mahakama Zinapowakosea Watanzania Kama Makosa Haya Tunawashitaki Wapi?

P
 
Hapa nauliza tuu swali, Je inawezekana baadhi ya Wabunge wetu wa Bunge la JMT ni mazuzu?, wanajadilije muswada wa sheria ya uchaguzi wenye vipengele batili vinavyokwenda kinyume cha katiba ya JMT bila kujijua kuwa kuna ubatili?, huu sio uzuzu?. Nauliza tuu!.
P
 
Mkuu, huko juu zaidi ni wapi?
 
Nalipeleka jambo lako kule juu zaidi, top of the top ambako huko lazima haki ipatikane!.
P
Acha tu nicheke kwa sababu, duh!

Nimeupenda uchambuzi wako, na inaonesha uko vizuri sana kwenye uelewa wa Katiba.

Jambo moja ambalo huwa unaniudhi sana ni wewe kujifanya huelewi kuwa Zanzibar ni nchi na huku Katiba ya Zanzibar imeliweka hilo peupe kabisa kuwa Zanzibar ni nchi na Taifa.
 
Acha tu nicheke kwa sababu, duh!
Mkuu GoldDhahabu ,huwezi amini,hii post ndio nimeiona leo,kucheka rukhsa
Nimeupenda uchambuzi wako, na inaonesha uko vizuri sana kwenye uelewa wa Katiba.
Asante,kiukweli mpaka leo mpaka kesho bado najiuliza yale mazuzu pale Dodoma,kwanini yametufanyia hivi?。Sheria mpya ya uchaguzi ilifuta zile sheria zote mbili za uchaguzi,Sheria ya Taifa ya Uchaguzi Sura ya 343 ya mwaka 1985 na Sheria ya Uchaguzi ya Serikali za Mitaa Sura ya 292 ya Mwaka 1979.

Tulipaswa kufanya uchaguzi huu kwa sheria mpya ya uchaguzi na kusimamiwa na Tume Huru ya Uchaguzi,lakini tunakwendaje kufanya uchaguzi wa serikali za mitaa kwa sheria iliyoisha futwa!。
Jambo moja ambalo huwa unaniudhi sana ni wewe kujifanya huelewi kuwa Zanzibar ni nchi
Kwanza pole kwa kuudhika, sio najifanya sielewi,ukweli ndio huo,Zanzibar sio nchi, nchi ni moja tuu Tanzania ambayo ni JMT,ya muungano wa union ya nchi mbili zimeungana kuunda nchi moja,zile nchi zote mbili zimekufa ikazaliwa nchi moja ya JMT, Zanzibar sio nchi bali ni sehemu ya JMT, yenye utawala wake wa ndani。
na huku Katiba ya Zanzibar imeliweka hilo peupe kabisa kuwa Zanzibar ni nchi na Taifa.
Katiba ya Zanzibar,imejifurahisha tuu kujiita Zanzibar ni nchi, katiba ya JMT,haiitambui katiba hiyo ya Zanzibar。 Kwa vile Zanzibar inajitegemea kwa mambo yake ya ndani,then iko huru kujiita vyovyote as long as katiba ya JMT,haiitambui katiba hii batili ya Zanzibar,na mambo ya ndani ya Zanzibar hayatuhusu,iacheni Zanzibar ijiite vyovyote。
p
 
😀😀😀

Nahisi "hauendagi" Zanzibar!

Na usije ukaenda siku za hivi karibuni, vinginevyo uikane kwanza kauli yako uliyoitoa dhidi ya nchi yao pendwa!
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…