Je, wajua nini hutokea katika Ulimwengu wa Roho wawili wanapoungana katika NDOA Takatifu?

Roho mtakatifu ni mwalimu, ni kiongozi, ni mfariji, anatukumbusha kutubu tunapokosea, hutuombea Kwa kuugua,

Ndomana nakuambia, ukimkatibisha akuongoze, Roho ya mpinga kristo itakukimbia.
Amina
 
Maandiko Yako wazi, Mariam alizaa watoto wa kiume na WA kike na Yusuph. Na Yesu aliwachagua baadhi ya ndugu zake kuwa wanafunzi wake.

Vyakula special vya kuletwa na Malaika hayo ni maelezo Yako yasiyoandikwa kwenye BIBLIA.
Wakristo mnamkosea adabu Bikira Mariamu.
Ngono ni matokeo ya ánguko la mwanadamu.
Baada ya ánguko kuzaa Tena Kwa uchungu ni adhabu aliyopewa mwanamke.
Hawa alikua ni maalumu Kwa ajili ya kumzaa Mwana Wa Adamu . Akaanguka dhambini na kupewa adhabu ya kuzaa Kwa uchungu.
Mariamu Mamaye Yesu hakujamiiana MAISHA yake yote. Kama unaamini kuwa Yesu ni mwana Wa Mungu ondoa Hiyo Imani kuwa Mama yake aliendelea kujamiiana na Joseph. Ni kufuru kubwa sana.
Kuvuviwa na Roho mtakatifu na kupata mimba kimiujiza ni jambo kubwa sana.
Msisome Biblia bila kujua na historia na Imani iliyokuwa ipo kwenye Jamii juu ya kumsubiri Masihi na atakavyotokea.
Bikira Mariamu aliletwa Duniani Kwa KAZI moja tuu ya kumzaa Mwana Wa Mungu basi. Ndio Maana Hata Yesu hakuoa Ili kuendelea uzao mtakatifu mana hakuja Kwa KAZI huyo.


Hivi kwenye Biblia Yako kuna sehemu inayokuonyesha kuwa Esther hakuwahi kufanya mapenzi na Mfalme na ni Kwa nini hakufanya mapenzi Naye ! Na Kwa nini Esther aliingia kwenye historia ?
Na UPI ulikua waraka Wa kuwaua wayahudu? Na Kwa nini ule waraka uliondilewa kwenye Biblia?
 
Huyu hapa mwingine mwenye imani ya "Theotokos"
😅😅😅

Anapingana mpaka na Biblia kusupport "Theotokos"
 
Mkuu,

Nimekunukuu,

"Utaniuliza, kwanini wanawake ni wengi kuliko wanaume, kwamba tukioana mke mmoja, mume mmoja, wanawake watabaki bila waume, Hilo Lina sababu na majibu yake, Si Leo"

Ukipata wasaa wa kujib hii hoja uliyo iibua hapa ni Tag☺️😊
 
Kumbuka kuwa nimekuambia kuwa Joseph alikua na wake wengine Wa ndoa halali ndio Maana Malaika akamwambia kuwa amchukue Mariamu Ili Jamii ile isije ikaamuru auawe mana angeonekana amezaa mtoto Kwa zinaa.
Joseph alikua ni mlezi tuu .
Warumia walimlinganisha Mariamu na Imani iliyokuwa inatazamiwa Kwa Karne nyingi ya kutokea Kwa mwanamke Wa namna ya ajabu na ámbaye amgemzaa Mtoto asiye na baba.
Hiyo ni historia Ilikua inasubiriwa na Jamii nyingi sana wakati huo.
Kwa Elimu kubwa waliyokuwa nayo warumi waligundua kuwa Bikira María ndiye alietimiza utabiri Huo na SIO wale waliokuwa wamewaamini zamani hizo.

Mfano . Leo hii kuna Smart phone Tofauti na Miaka 50 iliyopita. Huwezi kusema kuwa smart phone SIO simu Kwa Sababu tu haikuwepo zamani na haifanani na simu za zamani.
 
Una uthibitisho wa ulichokiandika kama upo...
Nauomba Tafadhali..
Kutoka kwenye Sources yoyote ya kuaminika..

Hakuna Uthibitisho wa Maria kuendelea Kuwa Bikra baada ya kumzaa Yesu...
Wala hakuna uthibitisho kwamba Yusuph alimuacha baada ya Kuzaa...
Ndyo Maria Aliolewa kwenye ndoa ya Mitaala hili nakubali japo ni chungu kwa Wakristo kulikubali hilo
 
Mbona hata kwenye biblia kuna siku Maria alikuja na nduguze kumuona yesu aliozaa na joseph
Jamani Yesu ni Mwana Wa Mungu.
Yesu ni zaidí ya Nabii.
Yesu ni zaidí ya wafalme Wa Dunia .
Yesu ni Zaidí ya Uzao wote Wa Adamu Wa Kale.
Sasa jiulizeni ni Nabii Yupi mkuu alitakiwa na Mwanamke mwenye uzao Wa watoto wengi kwenye Biblia?

Manabii wote wakiotengwa Tangu tumboni mwa mama Zao walizaliwa peke Yao Tena mara nyingine na wanawake walioonekana kuwa Tasa lakini baba Zao walikuwa na Watoto wengine Kwa mama wengine.
Tafakarini. Haya.
Hawataki watu wajue kuwa Joseph alikua ni mume Wa wanawake wengi Wa ndoa Halali Kwa mujibu Wa Mila na Tamaduni za kiyahudi. Kwa Warumi wake wengi haikubaliki ndio Maana hawakuzingatia hiyo historia.
 
Ok, ntajitahidi kuwatag wote walioreply kwenye previous threads Kila ninapoleta new thread.

Ubarikiwe.
 
Afu wanataka lazimisha kuwa Joseph alikuwa mcha mungu kiasi cha kuishi na mwanamke bila kumla mtu alikuwa seremala wanasema kwa enzi hizo ni tajiri
Ibrahim baba wa imani alishindwa vumilia akagonga nje atakuwa joseph
Acha kupotosha Imani Sahihi inayofichwa.
Hujiulizi Ibrahimu angekua na mihamko ya kingono Kwa nini alikaa miaka mia moja bila kuoa Mwanamke Mwingine na kuzaa .?
Kwa nini hakuoa mapema tu akiwa kijana na kuzaa?
Kwa nini alikaa na MKE wake Sara mpaka wakazeeka na hakumsaliti kwenda kuoa MKE mwingine mpaka akafikisha miaka mia moja ? Kwa nini alisubiri mpaka Mkewe ndiye akamlazimisha amwingilie Hause Girl na amzalie mtoto.? Hapo huoni kuwa Yule alikua ni Nabii mwenye Imani sana na mwadilifu Kwa kiwango Cha juu sana.
Unafikiri waliomwita baba Wa Imani walikurupuka tu?

Manabii wakubwa wote walizaliwa na wanawake WASIOKUA na uzazi Wa kuzaa Zaa Watoto wengi ikiwemo Yesu.
Yesu hakuwa na Ndugu Wa mama mmoja zaidí ya Binam zake na Watoto Wa Joseph Kwa mamá Mwingine.
Kwa Mila za kiyahudi watoto Wa baba mmoja ni ndugu halisi Wa Damu. Kama walivyo watoto Wa mama mmoja.
 
Mungu hajaumba ndoa.Mungu aliumba Kuzaa,Kuabudu na kufa.Binadamu akaumba Pesa,ndoa na dini.

Sent using Jamii Forums mobile app
Watakaoingia Mbinguni, WATAKATIFU, wanaitwa bibiharusi wamsubiriao BWANA harusi katika Roho.

Ndo ujue, Ndoa ni ya kiroho kwanza KABLA ya kuwa ya kimwili.

Ubarikiwe.
 
Amen, Amen Mungu nakushukuru kwa kunipa mume bora anayenipenda na mimi nikampenda ndoa yangu imetoka kwa Mungu Baba aliyeziumba mbingu na nchi.
 
Hili la kuoa mke mmoja limetokea wapi ilihali wengi ambao wanaongelewa kwenye biblia walikuwa na wake wengi.
Hata Joseph alikua na wake zaidí ya moja akiwemo Mariam ámbaye aliishi Naye Kwa ajili ya malezi ya Yesu tuu.
Alikua ameshamuacha kisiri Siri. Akaambiwa na Malaika asimwache .
 
Amen, Amen Mungu nakushukuru kwa kunipa mume bora anayenipenda na mimi nikampenda ndoa yangu imetoka kwa Mungu Baba aliyeziumba mbingu na nchi.
Amen ubarikiwe,

Ila hakikisha unampa trust namba moja Mungu ndipo wengine wafuate, mume akiwemo.

Pia imeandikwa mwanamke ni mwombaji, omba sana Ili kumficha mumeo na Hila za shetani, maana hakuna kitu kinawindwa kuvunjwa Kwa Kila namba na shetani na majeshi yake kama ndoa.

Ajua akifanikiwa KUVUNJA ndoa, amejaribu taasisi na nahusiano kati ya Mungu na familia, Ajua pia akivunja ndoa, watoto watakosa Maadili na kujitumbukiza ktk UOVU.

Amen
 
taa yangu inawaka kila sekunde imejaa mafuta mafuta hayapungui maana imeandikwa mwanamke atamlinda mume wake kwa maombi mimi ni mlinzi wa mume wangu kwa ilo sina shaka
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…