Je, wajua nini hutokea katika Ulimwengu wa Roho wawili wanapoungana katika NDOA Takatifu?

taa yangu inawaka kila sekunde imejaa mafuta mafuta hayapungui maana imeandikwa mwanamke atamlinda mume wake kwa maombi mimi ni mlinzi wa mume wangu kwa ilo sina shaka
Ubarikiwe sana,

Pia usisahau kuombea na ndoa za wengine ambapo ndoa zao hazielewiki, zenye nagomvi, waombee na kuwashauri hasa WALIO karibu Yako,

Maana jirani Yako akiwa salama, usalama wako utaongezeka pia.

Lakini nimefurahi Kupata comment ya aina Yako, maana wengi wananishambulia, jambo ambalo linaonyesha kipengele Cha ndoa kina Hali Tete Kwa sasa.

Amen
 

Kwanza umepotosha habari za Miaka ya ibrahimu..
Umepotosha Juu ya Hagari..

Hivi mbona mnapenda kupotosha Sana na huwa mnapotosha kwa faida ya Nani...

Ibrahimu kamuoa Hagar akiwa na miaka 85..
Na ibrahimu kapata mtoto wa Kwanza akiwa na miaka 86..
Labda nikukumbushe kitu..
Hagari alikuwa mtoto wa Mfalme wa Misri ilo kwanza lifahamu..na alipewa Ibrahimu baada ya mfalme kutaka kulala na Sara baada ya kupata majanga ili kumuomba msamaha akampa mali nyingi pamoja na mtoto wake ili awe kijakazi wa Sarai...

Sheria ya Waebrania Mtumwa au Kijakazi huwekwa huru baada ya miaka 10..
Kwahyo Sara kwakuwa hakuzaa aliona Bora ampe Hagari kuwa mke wa ibrahimu..
Na sio kumuingilia kwa zinaa bali kama mke wake..

Nyie huwa mnasoma biblia au mnasimuliwa biblia?

Swala la binamu nafikiri nililijibu ukifatikia post no (#103) kuwa kulingana na maandiko kwa lugha ya Kiyunani Kaka zake na yesu Biblia imetaja kama ἀδελφοὶ" (adelphoi) ns kama unajua kiyunani (Greek) utagundua hiyo ni kwa Ndugu wa damu peke yake yaani ndugu wa wazazi sawa..
na binamu huitwa ανηψιός (anepsiós)
ila kulingna na biblia Bila Tafsiri wale hawakuwa binamu wala watoto wa mama mkubwa wala wa mjomba...

Mi nafikiri Arguments Nzuri ingekuwa hivi wale ni Watoto wa Maria au watoto wa Mke mwingine wa Yusufu?
hapa ningekuelewa na tungeanza kuongea lugha zinazoelekea kufanana ila nakushauri soma
 
Sio Wote Mkuu Usiseme wite sema asilimia kubwa
 
Ni kweli mimi nimepitishwa kwenye ndoa kusudi niweze kuwashauri wengine na kuwaombea pia ndoa inachangamoto kubwa sana ni kuzidi kuomba maana tumeambiwa ombeni bila kukoma kila saa ni kuomba.
 
Yaani ukiongea hivi napenda sana kwa sababu mtu anayeshauri kuhusu Ndoa nampenda na namuona matured iwe kidini (Kama nikisema iwe hivyo) au ki Nature ila kwingine huwa tunapishana ila kuna mambo uko vizuri snaa..
Yoyote Ambaye anapinga Ndoa (Hayuko tu kinyume na Mungu wako) ila pia yupo kinyume na Mazingira na Nature
 
Mkuu Mungu yupo kweli, ila wanadamu ndiyo WANAMUABUDU Mungu ambaye ni wa uongo. Hii mifumo ya kibinadamu kuhusu suala la Mungu achana nayo. Mtafute Mungu wako utampata.
 
Ni kweli mimi nimepitishwa kwenye ndoa kusudi niweze kuwashauri wengine na kuwaombea pia ndoa inachangamoto kubwa sana ni kuzidi kuomba maana tumeambiwa ombeni bila kukoma kila saa ni kuomba.
Mungu azidi kuibariki ndoa Yako, mpate maisha marefu yenye kheri,awape afya njema hata katika Ule umri wa uzee.

Ndoa yenu iwe ya kupigiwa mfano na JAMII yote inayowazunguka,

Na wengi wavutwe Kwa Yesu Kwa ushuhuda wenu.

Amen
 
Mkuu Mungu yupo kweli, ila wanadamu ndiyo WANAMUABUDU Mungu ambaye ni wa uongo. Hii mifumo ya kibinadamu kuhusu suala la Mungu achana nayo. Mtafute Mungu wako utampata.
Tatizo mukiulizwa mnaleta mlivyokalilishwa.
Mungu ni nini? Yuko wapi? Anafanya nini! Namtafuta wa nini! Hamjibu
 
Mungu azidi kuibariki ndoa Yako, mpate maisha marefu yenye kheri,awape afya njema hata katika Ule umri wa uzee.

Ndoa yenu iwe ya kupigiwa mfano na JAMII yote inayowazunguka,

Na wengi wavutwe Kwa Yesu Kwa ushuhuda wenu.

Amen
Ameeeeeeeeeeeeen, Napokea baraka katika jina la Yesu aliye hai Ameeeeeeeeeeeeeeeeeeen
 
Mkuu Ibrahim alikuwa ana pigana miti na Sara daily .angekuwa hataki ngono asingeoa.ila alikuwa mwaminifu sababu ya uchamungu.hata leo kuna wakristo wengi wana mke mmoja tu na hawazai nje nikiwemo mm
 
Huu ujinga mnajaziwaga wapi? Kuna sheli ya pumba na uongo?
 
Swali rahisi tu:

Huko kwenye ulimwengu wa roho ni wapi? Mtu kama mimi ambaye sijaokoka nawezaje kufika huko?
 
Swali rahisi tu:

Huko kwenye ulimwengu wa roho ni wapi? Mtu kama mimi ambaye sijaokoka nawezaje kufika huko?
Umewahi kuota ndoto?

Na unaweza kunisimulia ndoto ulizoota ambazo unazikumbuka ambazo ulipoamka Uliona ni kama tukio halisi kabisa lilitokea?
 
Umewahi kuota ndoto?

Na unaweza kunisimulia ndoto ulizoota ambazo unazikumbuka ambazo ulipoamka Uliona ni kama tukio halisi kabisa lilitokea?
Kama tukio halisi kabisa lilitokea? Mh!

Ndoto zangu nyingi ni za kuruka juu huko na kutua japo mara moja moja huwa napata shida ya kutua hasa nikiwa nimezidisha ugali au kama nimekula kwa kuchelewa sana. Pia kupigana na watu ambao siwajui...mara nyingi nawakanda japo mara moja moja huwa wananizidi naanza kukimbia mbio halafu naamka nikiwa nimelowa jasho hatari huku natweta.

Na mara chache chache niko chuoni au shuleni masomoni mara zali natandikwa viboko au nazusha varangati mpaka nafukuzwa au naambiwa kwenda kuwaleta wazazi.

Ndoto hizi ndiko huko kwenye ulimwengu wa roho? 😳
 
Yakobo aliyekuwa na wake wanne na bado alikuwa rafiki mkubwa wa Mungu ,Sulleiman wanawake 1000
umeandika vitu vingi ambavyo havina uhalisia
hata Musa hakuwa na mke mmoja
 
Ndio,

Ndoto pekee ni Ulimwengu wa Roho.

Mtu ni jumla ya MWILI, NAFSI NA ROHO.

Mtu ni ROHO anayo NAFSI na anaishi ndani ya MWILI.

Ukilala, Roho hupata muda wa kuzurura ipatakapo na hakuna umbali katika Ulimwengu huo wa Roho.

Roho inapokuwa imeenda kuzurura, Huwa Kuna kamba ya Sllver ambayo Huwa imeunganishwa mtu wa ndani (Roho) na mtu wa nje (Mwili).

Ni vibaya sana kumstua mtu aliye usingizini, maana utailazimisha Roho irudi Kwa haraka, jambo ambalo waeza sababisha kamba hiyo kukatika na mtu asiamke mazima.

Kwa kuwa mtu ni ROHO, awe ameokoka au hajaokoka huingia kwenye Ulimwengu wa Roho automatically kupitia ndoto.

Ile ya mawazo ya mchana kujirudia ndotoni, hufanywa na Akili ambayo Iko kwenye NAFSI.

Kuna viwango vya kuingia katika Ulimwengu wa Roho.

Kuingia katika Ulimwengu wa Roho Kwa kudhamiria ni LAZIMA uingie kupitia either Ulimwengu wa Giza au kupitia Ulimwengu wa Nuru.

Ukiokoka, utawezeshwa kuingia huko Kwa uweza wa Roho mtakatifu, macho ya mtu wa ndani yatafunguliwa uone wazi wazi yanayoendelea humo bila hata kusubiri kulala USINGIZI.

Njia ya pili ni kupitia Ulimwengu wa Giza, mchawi akikupania mchana, atasubiri muda ufike na ataficha sura yake Kwa msaada wa Pepo na atakuja kupitia Ulimwengu wa Roho, nawe Kwa kuwa u Roho, utata ndoto za kushambuliwa au kukimbizwa na wanyama.

Wakati naandika haya, napata ufunuo kuwa unayajua zaidi mambo katika Ulimwengu wa Giza kupitia asili na Mila za kikabila na ukoo uliotokea.

Nakusihi, uokoke, umpe Yesu maisha Yako, Ujazwe Roho mtakatifu Ili uwe raia wa Mbinguni.

Uona wazi wazi tena Bure maana Vipawa vya Yesu ni Bure na havina majuto.

Amen
 
Pia umegusia ndoto za kuota uko shuleni.

Mungu ni Roho, husema nawe mchana, na akiona husikii, hukuletea ndoto usiku, Atasema na mtu wa ndani live Kisha mtu wa ndani atakukumbusha ujumbe kupitia ndoto.

Mungu anakukumbusha kupitia ndoto ya mambo ya shule kuwa zipo hatua ambazo hukuzifanya vizuri zamani ambazo ndizo zinaleta mkwamo katika Maisha Yako kiuchumi, kijamii kimahusiano nknk.

Nilipoomba Mungu anipe mke sahihi, Mimi sikujubiwa Kwa ndoto, nilipata maono live, mchana kweupe, nikajikuta katika Ulimwengu wa Roho,nikiletewa picha ya mtu sahihi kwangu iliyokuwa ikifunguka mbele yangu Polepole kama ambavyo picha hufunguka unapoifungua kwenye mtandao.

Jifunze pia kuandika ndoto ambazo ukiamka unajikuta unatoka JASHO, HOFU au kukosa amani, au furaha tele na kuzitafutia majibu Kwa kushare na watu sahihi.
 
Ila ndoa ni chanzo cha utumwa kwetu wanaume. Ndio chanzo cha kutumaliza hata tusiishi miaka mingi duniani. Ndio chanzo cha msongo wa mawazo na tuzeeke vibaya
Hayo humpata mtu endapo atachagua Mke sie sahihi....sifa kuu Moja wapo ya Mke au Mume anayetoka Kwa Mungu hua ni Mcha Mungu mke anakua mwenye kumtii mumewe na mume anakuwa mwenye upendo wa dhati Kwa mkewe
 
Yakobo aliyekuwa na wake wanne na bado alikuwa rafiki mkubwa wa Mungu ,Sulleiman wanawake 1000
umeandika vitu vingi ambavyo havina uhalisia
hata Musa hakuwa na mke mmoja
Soma (Marko sura ya 10-12)

Yesu amefafanua vizuri. Tamaa na Vichwa ngumu vya WANADAMU ndo sababu ya watu Kuoa wake wengi,

Na Musa akaruhusu hayo ingawa haikuwa maelekezo ya Mungu.

Yesu akawajibu Kwa kuwarudisha Edeni, akamwambia Mungu aliasisi NDOA ya mke na mume mmoja baasi, tofauti na hapo ni UZINZI na UASHERATI.

Waislamu wanadai wanaamini INJILI, ila katika suala la NDOA, wameamua kubali kwenye torati.

Yesu ni Mungu, hivyo maelekezo yake ni Amri, sharti tuyafuate.

Amen
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…