Ni hatari sana kupuuzia ndoto, Hasa zile ambazo Mungu huleta ujumbe na maonyo kwako,
Kuna mtu aliota amepata Ajali usiku, na alikuwa amepanga safari kesho yake, alipuuza ndoto na kuanza safari bila kutafuta ufumbuzi,
Matokeo yake, alipata Ajali na kupoteza baadhi ya viungo.
Mwingine , mwanamke aliota ndotoni mumewe amezini na mtu mwingine na alionao tukio Zima ndotoni, kosa lake Akaenda kumuuliza mumewe,
Kilichotokea mume alimwambia hizo ni ndoto tu Wala Si Kweli, wakati katika uhalisia wiki iliyopita, alifanya Kweli UASHERATI Kwa Siri.
Sasa ukiokoka, ukawa na Roho mtakatifu, hata Jirani au adui akipanga ubaya au tukio dhidi Yako, utaona kabla live na kutafuta njia Bora za kuzuia.
Katika Ulimwengu wa Roho hakuna Siri.