Je, wajua nini hutokea katika Ulimwengu wa Roho wawili wanapoungana katika NDOA Takatifu?

Je, wajua nini hutokea katika Ulimwengu wa Roho wawili wanapoungana katika NDOA Takatifu?

Ukiwasoma vizuri utagundua Allah yupo seriously zaidi.
Hawajui Mungu wa kweli ni yupi afu wanataka kutushauri.

Huyo anaesema Yesu ndo Mungu, angekulia uarabuni huko unadhani angekua anasema hivyo?

Achana nao mkuu.
 
Kupitia maombi utamtambua Ukiomba Mungu atakupa ndiyo au maono kukuonesha uyo mtu ni sahihi au sio sahihi
pia inatakiwa ukae kwenye usafi husitende dhambi na kuomwomba Mungu maana Mungu hakai mahala pachafu yeye ni mtakatifu Ni Mungu Mtakatifu na msafi muombe Mungu atakutendea atakupa mwenza wako maana mwenza anaanzia Rohoni kwenye ulimwengu wa Roho na pia ndoa inaanzia Rohoni ndo inakuja mwilini ukiona mwenza wako ulimwengu wa Roho wa Mungu aliye hai unamkubali basi huyo atakuwa ametoka kwa Mungu Ameni
 
Yakobo alikuwa na mke zaidi ya mmoja,Ibrahim alikuwa na wake wawili,suleiman nae hivyo hivyo kifupi manabii wengi walikuwa na wake zaidi ya mmoja...nyinyi wakristo kwanini hamtaki tuwe na wake zaidi ya mmoja?

Ukiachana na hilo dini kabla hazijafika africa mababu zetu walikuwa na wanawake zaidi ya mmoja,kwanini nyinyi wachungaji hamtaki tuoe mke zaidi ya mmoja?
Utaonga sadaka kwa wake zako badala ya kuleta kanisani.mchungaji akale wapi
 
Vijana eleweni, NDOA ni agizo la Mungu.

Kutokuoa ni kudhibiti uzao, au kuleta mtafaruku katika JAMII Kwa watoto kuelewa na mzazi mmoja.

Mungu atusaidie.
 
Vijana eleweni, NDOA ni agizo la Mungu.

Kutokuoa ni kudhibiti uzao, au kuleta mtafaruku katika JAMII Kwa watoto kuelewa na mzazi mmoja.

Mungu atusaidie.
Kwenye Bible Mtume Paulo hakuoa, vivyo hivyo Yesu na Yohana mbatizaji. Unaweza usioe lakini pia usifanye zinaa, Kama huwezi kuvumilia basi jipatie mke utulie
 
Kwenye Bible Mtume Paulo hakuoa, vivyo hivyo Yesu na Yohana mbatizaji. Unaweza usioe lakini pia usifanye zinaa, Kama huwezi kuvumilia basi jipatie mke utulie
Manabii walioweka nadhiri ya Kutoa wapo Hadi sasa, sisi Hilo halituhusu.

Muhimu ni kuwa mada IPO clear.

NDOA ni mpango wa Mungu,

Kutooa, wake wengi,ckuzaa na kuacha watoto wakiteseka, ni mpango wa mwovu,

Tuombe Kwa bidii, Mungu amfunue mke, mume sahihi.

Amen
 
maana tukesema hatuna dhambi twajidanganya
Utakatifu ni vazi apewalo mtu baada ya kumwamini Yesu kuwa BWANA na Mwokozi.

Hivyo aliyeokoka ana vazi jeupe, kutenda dhambi ni kuchafua vazi, hivyo Kila anapoonyeshwa ametoa doa vazi, hukimbia haraka kutubu na kukisafisha Kwa Damu iliyomwagika msalabani ya Yesu Kristo.

Ndipo hapo neno husema, WATAKATIFU hawatendi DHAMBI. Tafsiri ya neno Hilo ni kuwa, waliookoka wanaye mshauri Roho mtakatifu, hawadumu dhambini kama nguruwe.

Mungu akupe kuelewa NENO la Mungu.

Amen
 
Ndio UKWELI,

Si lazima Hadi upate maisha mazuri ndipo uone,la hasha,

Mungu akikujalia kumpata ubavu wako, mkaunganisha vibali,baraka, mtapigwa hatua za haraka sana maishani,

Muhimu, ingia magotini, Mungu akupe na akukutanishe na ubavu wako.

Ubarikiwe 🙏
 
Kitu ambacho kinanipa shida ni;
Kwanini tutumie biblia kama reference,tuna uhakika gani kwamba yaliyoandikwa yanaukweli?

Kama MUNGU anajua maisha yetu tangu kabla ya kuzaliwa mpaka kufa,hii inamaanisha kwamba kivyovyote vile tutakavyoishi i.e katika utakatifu/dhambi hakutabadilisha hatima zetu, niliwa na maana ya kwamba kama MUNGU alipanga wewe ni wa motoni basi hata kama utaishi maisha yako yote pasi na kutenda dhambi still utaenda motoni and vice verse
 
Back
Top Bottom