Je, wajua? - Special Thread

Je, wajua? - Special Thread

Je Wajua ?
Kuna tofauti ndogo sana kati ya neno "Bunge" na "Bangi"

Je wajua?
The Bitoz ni Superstar pekee wa kitaa hapa JF
 
Naamini wengi kama si wote miongoni mwetu tunavifahamu vioo ambavyo vimekuwa na matumizi mbalimbali kwa mwanadamu.

kioo(glass) kina matumizi mbalimbali kama vile kutengenezea vioo vya kujiona{mirrors) milango ya vioo na madirisha kwenye nyumba zetu na kadhalika.

Ili kioo(glass) kiweze kukamilika/kutengenezwa kinahitaji malighafi zifuatazo;

-mchanga(ordinary sand) ambao una kiwango kikubwa cha silica.
-calcium carbonate na
-sodium carbonate.

Ndani ya viwanda vya kutengenezea vioo mchanga huyeyushwa kwa kutumia joto kubwa sana (1700degree centgrade),ili kupunguza joto ambalo mchanga huyeyuka wanauyeyusha pamoja na sodium carbonate.

mchanga ukishayeyuka hupatikana ujiuji ambao una tabia ya ugumu(amorphous solid) wenye sifa ya ku react na maji hivyo mchanga pia huyeyushwa pamoja na calcium carbonate kuzuia usireact na maji.

Baada ya ujiuji kupoa na kuwa mgumu kioo kinakuwa kimeshakamilika kutengenezwa na kioo hiki kinaitwa sodalime-silica glass,ambapo hutumika kwa matumizi mbalimbali.
 
Mkuu M hebu tupe zaidi... ni vifaa,samani au mitambo gani huhitajika kutengeza vioo
Kama unazungumzia malighafi tayari nshazungumzia kwenye uzi.

kama una maana ya mitambo mfano;inayozalisha hilo joto au kitu ambacho huifadhi huo mchanga ili uyeyushwe ntakuja kukujuza mana ni ishu ndefu lakini pia jaribu kwenda kutembelea viwandani utapata kujifunza mengi kuliko ntakayokwambia mimi hapa.
 
Mwaka 1808 Napoleon alivamia nchi ya Ureno ivyo familia ya kifalme ya Ureno ilibidi wajihami na kukimbia Ureno na kukimbilia Brazil kwa kuwa lilikuwa koloni lao.

Hivyo wakawasili mjini Rio de Janeiro na tangia apo Rio de Janeiro ukawa mji mkuu wa Ureno nje ya Ureno.

Rio de Janeiro uliendelea kuwa mji mkuu wa Brazil hata baada ya kupata uhuru mpaka mwaka 1960 serikali ya Brazil ilipoamua kuuhamisha mji mkuu kutoka pwani ya Brazil mpaka interior mwa nchi katika jiji la Brasilia kupunguza population mjini Rio.
 
Mwaka 1808 Napoleon alivamia nchi ya Ureno ivyo familia ya kifalme ya Ureno ilibidi wajihami na kukimbia ureno na kukimbilia Brazil kwa kuwa lilikuwa koloni lao.Ivyo wakawasili mjini Rio de janeiro na tangia apo Rio de janeiro ukawa mji mkuu wa Ureno nje ya Ureno.
Rio de janeiro uliendelea kuwa mji mkuu wa Brazil ata baada ya kupata uhuru mpaka mwaka 1960 serikali ya Brazil ilipoamua kuuhamisha mji mkuu kutoka pwani ya Brazil mpaka interior mwa nchi katika jiji la Brasilia kupunguza population mjini Rio.
Dah Sikujua! Asante kwa Historia!
 
Wengi hujiuliza hivi serikali hutengenezaje ajira mfano ikisema inataka kutengeneza ajira milioni tatu inatengenezaje?

1.Ni kwa yenyewe kuajiri.Ukiangalia mfano sasa hivi vijana polisi na wanajeshi walioajiriwa kwenye majeshi yote ni wengi mno.Ukienda ofisi za serikali nyingi unakutana na vijana wengi watu wazima ni wa kuhesabu iwe walimu,madaktari nk Serikali imeamua kuwaajiri.

2.Kwa kuleta wawekezaji wakubwa.Mfano Alivyoingia vodacom ajira kwa watu wengi mno
Zilizaliwa kama
  • Wafanyakazi wa vodacom
  • wauza vocha na Maagenti wa Mpesa angalia waliosambaa nchi nzima walivyo wengi
  • Maduka kibao ya wauza simu za mkononi
  • Ajira kibao za Mafundi simu
3.Kuweka sera ya biashara mpya: Mfano Serikali waliporuhusu biashara ya boda boda ona ajira nyingi zilivyozaliwa
  • Ajira kibao za maduka ya wauza piki piki
  • ajira kibao za madereva wa pikpiki
  • ajira kibao za maduka ya spea za pikipiki
  • ajira kibao za mafundi pikpiki
  • ajira kibao za waosha pikipiki
4.Kutengeneza miundo mbinu kama ya Barabara nk
Barabara hufungua ajira kibao.Ajira zizaliwazo upya
  • Ajira za watengeneza barabara
  • Huvutia ajira za usafirishaji ambako watu kibao huajiriwa kuendesha magari ya kupitia hizo barabara mfano madereva wa mabasi, malori
  • Viwanda,maHoteli,maduka,masoko mengi hufunguliwa pembeni mwa barabara ambayo hutoa ajira kwa watu wengi mno
Haya ni baadhi tu ya mambo ambayo serikali hutumia kuongeza ajira katika nchi.
Hii ni kuwasaidia wale ambao wakisikia serikali itaongeza ajira huwa wanabeza tu kwa kuwa hawana upeo wa mambo zaidi ya ule wa siasa za majukwaani za kumnadi mgombea.
 
Umeelimisha vizuri sana hao unaodhani wana upeo mdogo ila ungemalizia somo lako bila kukejeli lingekuwa na maana zadi ya hapa.
 
serikali inatengeneza ajira kwa kuweka mazingira bora ya watu kujiajiri na kuajiriwa,kuhakikisha kunajengwa viwanda vya usindikaji kwa mazao na madini yanayopatikaana hapa nchini,kuondoa urasimu kama kusajiri biashara na mambo mengine yanayofanana na hayo,kuboresha miundo mbinu kama barabara, kuboresha na kusaidia upatikanaji uhakika wa umeme,maji kulinda viwanda vya ndani
 
Back
Top Bottom