Wengi hujiuliza hivi serikali hutengenezaje ajira mfano ikisema inataka kutengeneza ajira milioni tatu inatengenezaje?
1.Ni kwa yenyewe kuajiri.Ukiangalia mfano sasa hivi vijana polisi na wanajeshi walioajiriwa kwenye majeshi yote ni wengi mno.Ukienda ofisi za serikali nyingi unakutana na vijana wengi watu wazima ni wa kuhesabu iwe walimu,madaktari nk Serikali imeamua kuwaajiri.
2.Kwa kuleta wawekezaji wakubwa.Mfano Alivyoingia vodacom ajira kwa watu wengi mno
Zilizaliwa kama
- wauza vocha na Maagenti wa Mpesa angalia waliosambaa nchi nzima walivyo wengi
- Maduka kibao ya wauza simu za mkononi
- Ajira kibao za Mafundi simu
3.Kuweka sera ya biashara mpya: Mfano Serikali waliporuhusu biashara ya boda boda ona ajira nyingi zilivyozaliwa
- Ajira kibao za maduka ya wauza piki piki
- ajira kibao za madereva wa pikpiki
- ajira kibao za maduka ya spea za pikipiki
- ajira kibao za mafundi pikpiki
- ajira kibao za waosha pikipiki
4.Kutengeneza miundo mbinu kama ya Barabara nk
Barabara hufungua ajira kibao.Ajira zizaliwazo upya
- Ajira za watengeneza barabara
- Huvutia ajira za usafirishaji ambako watu kibao huajiriwa kuendesha magari ya kupitia hizo barabara mfano madereva wa mabasi, malori
- Viwanda,maHoteli,maduka,masoko mengi hufunguliwa pembeni mwa barabara ambayo hutoa ajira kwa watu wengi mno
Haya ni baadhi tu ya mambo ambayo serikali hutumia kuongeza ajira katika nchi.
Hii ni kuwasaidia wale ambao wakisikia serikali itaongeza ajira huwa wanabeza tu kwa kuwa hawana upeo wa mambo zaidi ya ule wa siasa za majukwaani za kumnadi mgombea.