Je, wakati umefika wa Misikiti kugeuzwa Sunday-school na Gwajima?

Je, wakati umefika wa Misikiti kugeuzwa Sunday-school na Gwajima?

Robert Heriel Mtibeli

JF-Expert Member
Joined
Mar 24, 2018
Posts
28,297
Reaction score
68,017
JE, WAKATI UMEFIKA WA MISIKITI KUGEUZWA SUNDAY-SCHOOL NA GWAJIMA?

Na, Robert Heriel

Miaka mitano nyuma, naam mwaka 2015 Gwajima alionyesha dhamira yake na ndoto yake kubwa ambayo alitanabaisha kuwa anatamani Misikiti kuwa Sunday- School za watoto wa Kikristo, pamoja na masheikh na maimamu wakikimbizana kwenda mbele ya msalaba wa Bwana Yesu. Hii ilikuwa zama zile za ambapo Mzee Lowasa naye alijikita kwenye Dhana ya Ulutheri kuwa moja ya vigezo vya yeyey kuchaguliwa kuwa Rais wa Tanzania.

Moja ya watu waliojitokeza kumpinga Askofu Gwajima, ni pamoja na Imam Bukhary ambaye yupo pichani hapo.

Imamu Bukhary pia alieleza namna Gwajima alivyopinga uwepo wa Mahakama ya Kadhi. Lakini hili hakulitilia mkazo ukilinganisha na tamko la Gwajima linalohusu ndoto yake ya kuwabatiza Masheik nchi nzima, kisha kuigeuza misikiti kuwa Sunday- School ambapo watoto wa Kikristo watajifunzia elimu ya msingi humo.

Sasa Gwajima amepewa nafasi ya kupeperusha bendera ya CCM katika ngazi ya ubunge.

Je, Waislam watakuwa tayari kuona misikiti yao kugeuzwa Sunday-school na wataamua kumchagua Askofu Gwajima atimize adhma hiyo?

Je, Askofu Gwajima aliomba msamaha kwa yale matamko aliyoyatoa 2015, hivyo Waislam wasiwe na wasiwasi na misikiti yao kugeuzwa misikiti?

Je, Masheikh na maimamu wapo tayari kubatizwa na kujisalimisha mbele ya Msalaba wa Bwana Yesu kama Gwajima alivyoeleza 2015?

Je, Gwajima aliomba radhi kwa masheikh na maimamu kwa kauli zake kuhusu kuwapiga maji viongozi hao?

Kama Gwajima hakuomba msamaha kipindi kile ili asamehewe na Waislam, Je akiomba sasa hivi haoni kwamba ataonekana ni kwa sababu anataka kura?

Je Watanzania waishio Kawe wapo tayari kumuunga mkono Gwajima na kumchagua kuwa kiongozi wao licha ya kauli zake za kibaguzi dhidi ya waislam?

Baada ya maswali hayo.

Maoni yangu;

Binafsi Taikon nisingeweza kumchagua Gwajima hata kama ningekuwa nimechanganyikiwa, hata kama ningekuwa nimelewa kwa kunywa pombe, hata kama ningeshikiwa mtutu wa Bunduki.

Mimi ni Mkristo, lakini sipendi mtu mwenye mambo ya kibaguzi ya kidini. Taifa letu nila dini zote. Kwa bahati upande wa Baba yangu karibu wote ni Waislam. Baba yangu ni muislam, mashangazi wote ni Waislma. Kuwabagua waislam ni kubagua Baba zangu. Kuwabagua Wakristo ni kuwabagua mama zangu.

Mimi nisingemuunga Mkono Gwajima hata kama ningeambiwa ninyimwe pepo, ningekuwa tayari. Gwajima hafai kuchaguliwa kuwa kiongozi wa kisiasa.

Ifahamike kuwa, Gwajima ni mtu mzima, anaelimu ya kutosha, hivyo kile akisemacho anajua atahari zake, amedhamiria kwa ndani kabisa. Yeye ni mtu mzima kile akiongeacho ndicho kinachozunguka akili yake, ndicho kilichojaza moyo wake.

Gwajima atashindwa kutimiza lengo lake kwa sababu ya mipaka ya mamlaka lakini kama akiwa na nguvu zaidi anaweza kufanya kile akitakacho.

Wana KAWE Kama walivyo Watanzania wengine hawatakubali kumchagua mtu atakayeleta upuuzi ndani ya jamii. Mtu anapoongea jambo jua anaweza kulitekeleza, akishindwa ni kutokana na kutokuwa na nguvu.

Wakristo wote wenye akili kamwe hawawezi mchagua Gwajima achilia mbali ndugu zetu Waislam, na wale wasioamini katika dini.

Kuhusu msamaha.
Tunaweza kumsamehe, lakini hatutampa uongozi na kama yeye amedhamiria asamehewe basi asijisikie vibaya sisi kutompa uongozi.

Hata hivyo CCM nao wanashangaza mno, hivi wamekosa wa kumpa tiketi yao mpaka wampe Gwajima.

Je, CCM hawajui ubaguzi alionao Gwajima?
Hawakusikia kauli zake za kugeuza misikiti kuwa sunday-school na kuwasilimisha masheikh na maimamu?
Je, wamesahau matusi yake kwa Mzee wetu wa Heshima Kadinali pengo?
Je, hawasikii skendo zake za umalaya Mpaka video za uchi? Je CCM wameamua kuuza jimbo kwa urahisi kwa HALIMA Mdee?

Je, CCM hawakusikia tuhuma za Gwajima kuhusiana na kuchochea ukabila kwa vipeperushi na audio yake akihamasisha wasukuma kuungana na kunada vikundi vya watu 2000, mpaka jeshi la polisi likamkemea na kumuonya?

Je, CCM wanafikiri watamsafisha Gwajima na watu kumuona Msafi kwa kauli zake hizo za ajabu?

Nauliza CCM wameamua kuuza Jimbo tena awamu hii?

Bora wangempa yule dogo aliyeshika namba moja kwenye kura za maoni. Lakini kwa Gwajima atapigwa mapema mno. Kabla Magari ya Mbeya hayajafika IRINGA Gwajima atakuwa ameshachezea.

Niwaombe Watanzania waishio KAWE wasimchague Gwajima, pia na majimbo mengine yenye wagombea wenye historia ya kauli za kibaguzi, iwe ubaguzi wa dini, ukabila, au ubaguzi wa namna yoyote ile.

Hii itakuwa fundisho kwa watu wa namna hii.

Kama kanisani kwake ndiko wanapenda ubaguzi apeleke huko huko.
Kama ni nyumbani kwake apeleke huko.

Asituletee mambo ya hovyo kwenye jamii yetu inayoishi kwa amani na upendo.

Kama alijichafua mwenyewe anapaswa ajisafishe, hakuna wa kumsafisha, yeye sio mtoto mdogo ili asafishwe. Angesafishwa kama angekuwa amechafuliwa. Lakini kwa mdomo wake alijichafua.

Mtu mzima haogeshwi.

HALIMA MDEE jikite kwenye sera kati ya hizi
1. Uhuru na Umoja
2. Upendo na mshikamano
3. KAWE ya watu wote
4. Sote ni ndugu n.k

Hiyo imeisha.

Katika haya Gwajima Mdomo hautakusaidia, pesa zako ni zako, jimbo nila wananchi. Kawe sio ya watu kama wewe.
Katika Hili nimejipambanua, wala sihitaji unafiki, Gwajima asiungwe Mkono, na watu wote waseme Amina.

Robert Heriel
Taikon wa Fasihi
0693322300
 
Hata Sisi wakristo wenzake tunashangaa na kauli za gwajima juu udini wake..... itakuwa ni UJINGA na udini wa Hali ya juu kama huyu mjinga mcheza-porn Kama ataingia bungeni.

Na kama ataingia Bungeni basi tutegemee wabunge wa Viti maalumu kupigwa miti kila siku na huyu shetani
 
Usinikumbushe shetani wa kipindi hicho

Aliyetusababishia Watanzania kuuwana Kwa sababu kutofautiana Imani zetu

Kuchomeana Makanisa na misikiti
Kuchomeana vitabu vitukufu
Shetani wa kipindi hicho tunamlaani Kwa nguvu zote kama Taifa na ashindwe akafie kuzimu

Hizo za GWAJIMA wa enzi wa shetani MLA watu, ndizo zilizokuwa zikichochea vurugu, na sasa tumeshamjua huyo Ibilis, hakupenda kuona tukiushi Kwa Amani na upendo kama Taifa moja, Nia yake alitaka kututwika zigo zito lisilobebeka

Sasa, hatuko kabisa huko, tumeshajitambua na tumegundua kuwa, nchi yetu ni yetu sote, Mwislamu na Mkristo na tunategemeana Sana,

Swala la kueneza dini, nalo sio ugomvi, ni swala la kistarabu, hakuna haja ya kutukanana, kwani Mungu anapenda Amani na watu wote

Sasa Tuna GWAJIMA mpya kabisa, sio wa kipindi cha shetani mweneza chuki

Tanzania ni moja na watu wake wanaishi Kwa umoja

Mungu Ibariki Tanzania
 
Huyo Askofu tapeli mpigeni chini fasta.....

Kwanza yuko bize anaratibu kikundi chake cha kikabila yy na makonda.....

Piga chini mdini na mkabila huyo abaki na hicho kikundi cha kigaidi na waumini wake ambao wapo km mang'ombe
Mkuu, ni wewe?
 
Sio tu wakati muafaka wa kugeuza misikiti kuwa Sunday Schools, bali pia utakuwa ni muda muafaka kwa shule za Kawe kuanzisha Somo la kukuza Mila, Tamaduni na Lugha ya Kisukuma!!

Wana Kawe tunafarijika kupata mgombea ambae sio tu atakuwa anatetea dhehebu letu peke yake na kwa nguvu zote huku akiwachana chana wale wa imani zingine bali ni pia mgombea anayeona umuhimu wa watu wa kabila lake kuwa supported!
 
Jiandae kisaikolojia maana propaganda zako hazitazuia chochote udini wako kaa nao mwenyewe, Gwajima humuwezi wewe ni level nyingine


KAWE sio unavyoifikiria wewe Mkuu.

Gwajima hata angegombea kwa wajinga bado wasingempa.

Naitwa Taikon muona mbele, october tukutane hapa.

Gwajima hawezi kuchukua jimbo la KAWE mimi nikiwepo, kama huniamini, subiri muda utakuaminisha
 
Usinikumbushe shetani wa kipindi hicho

Aliyetusababishia Watanzania kuuwana Kwa sababu kutofautiana Imani zetu

Kuchomeana Makanisa na misikiti
Kuchomeana vitabu vitukufu
Shetani wa kipindi hicho tunamlaani Kwa nguvu zote kama Taifa na ashindwe akafie kuzimu

Hizo za GWAJIMA wa enzi wa shetani MLA watu, ndizo zilizokuwa zikichochea vurugu, na sasa tumeshamjua huyo Ibilis, hakupenda kuona tukiushi Kwa Amani na upendo kama Taifa moja, Nia yake alitaka kututwika zigo zito lisilobebeka

Sasa, hatuko kabisa huko, tumeshajitambua na tumegundua kuwa, nchi yetu ni yetu sote, Mwislamu na Mkristo na tunategemeana Sana,

Swala la kueneza dini, nalo sio ugomvi, ni swala la kistarabu, hakuna haja ya kutukanana, kwani Mungu anapenda Amani na watu wote

Sasa Tuna GWAJIMA mpya kabisa, sio wa kipindi cha shetani mweneza chuki

Tanzania ni moja na watu wake wanaishi Kwa umoja

Mungu Ibariki Tanzania
Kwa taarifa yako Gwajima hapo alipo anatakiwa akatubu, amemkosea Mungu muumba wa mbingu na nchi, alietuasa tusiwe vuguvugu, bora tuwe moto au baridi. Gwajima kwa kukimbilia siasa hapohapo bado ni kiongozi wa kanisa huyu mtu ni vuguvugu, hayupo duniani wala mbinguni.
 
Sio tu wakati muafaka wa kugeuza misikiti kuwa Sunday Schools, bali pia utakuwa ni muda muafaka kwa shule za Kawa kuanzisha Somo la Lugha ya Kisukuma!!

Wanakawe tunafarijika kupata mgombea ambae sio tu mdini bali ni mkabila!
😀 😀 😀 😀 😀
 
Back
Top Bottom