Je, wakati umefika wa Misikiti kugeuzwa Sunday-school na Gwajima?

Je, wakati umefika wa Misikiti kugeuzwa Sunday-school na Gwajima?

Kumekuchaaa, wasukuma tuungane...
Simoooooooo...🏃‍♂️

Nafikiri CCM kwa makusudi hawalitaki jimbo la Kawe. Haya ni maamuzi wengi hatukuyatarajia.

Everyday is Saturday... 😎
 
Wote nyie ni wale wale! Mnataka kura za Waislam kwa maslahi yenu. Waislam sio kondoo wanajitambua!
Hivi hawa waislam, wana mchango gani katika taifa ambao ni zaidi ya Watanzania wengine wasio waislam ambao ni wengi zaidi?

Kwa nini uislam umejaa sensitivity na malalamiko hata pasipo sababu?

Ni mfumo gani ndani ya nchi ambao umewabagua waislam kwa kuwa ni waislam?

Ni nani aliyetendewa vibaya kwa sababu ya kuwa na dini ya uislam?

Historia inaonyesha miaka ya nyumba Tanzania iliwahi kuwa na viongozi wakuu wa nchi Waislam ambao walipigiwa kura na watu wa dini zote na waisokuwa na dini. Kwa nini husemi kwamba walitumia kura za watu wasio waislam kwa maslahi yao?

Naomba utafute maarifa ambayo yanapatikana kwa kumcha Bwana, kuliko kuongozwa na hisia zitokanazo na hofu ya udogo wa kiwango.

Jitahidi kuwa Mtanzania anayejali utaifa badala ya ubinafsi na ubaguzi.
 
Kwa taarifa yako Gwajima hapo alipo anatakiwa akatubu, amemkosea Mungu muumba wa mbingu na nchi, alietuasa tusiwe vuguvugu, bora tuwe moto au baridi. Gwajima kwa kulimbilia siasa hapohapo bado ni kiongozi wa kanisa huyu mtu ni vuguvugu, hayupo duniani wala mbinguni.
😄😄 Sawa mkuu, amekusikia, lkn hii yote ni Kwa sababu kachukua fomu kwenye timu usiyoipenda,

Kama sio wivu tuiteje sasa, rejea ulivyokuwa ukimpamba kipindi cha Lowasa
 
😄😄 Sawa mkuu, amekusikia, lkn hii yote ni Kwa sababu kachukua fomu kwenye timu usiyoipenda,

Kama sio wivu tuiteje sasa, rejea ulivyokuwa ukimpamba kipindi cha Lowasa

Mkuu, mimi sipendi watu wabaguzi.
Mtu akiwa mbaguzi dawa yake ni kumbagua. Wala usijpendekeze naye.

Lowasa nilimchinjia baharini kwa sababu nyingi tuu,
Huyo Gwajima hata angekuwa ndiye Malaika wangu ningemkataa, ningemuambia Mungu ni bora kubaki bila ulinzi kuliko malaika kama Gwajima
 
JE WAKATI UMEFIKA WA MISIKITI KUGEUZWA SUNDAY-SCHOOL NA GWAJIMA?

Na, Robert Heriel

Miaka mitano nyuma, naam mwaka 2015 Gwajima alionyesha dhamira yake na ndoto yake kubwa ambayo alitanabaisha kuwa anatamani Misikiti kuwa Sunday- School za watoto wa Kikristo, pamoja na masheikh na maimamu wakikimbizana kwenda mbele ya msalaba wa Bwana Yesu. Hii ilikuwa zama zile za ambapo Mzee Lowasa naye alijikita kwenye Dhana ya Ulutheri kuwa moja ya vigezo vya yeyey kuchaguliwa kuwa Rais wa Tanzania.

Moja ya watu waliojitokeza kumpinga Askofu Gwajima, ni pamoja na Imam Bukhary ambaye yupo pichani hapo.

Imamu Bukhary pia alieleza namna Gwajima alivyopinga uwepo wa Mahakama ya Kadhi. Lakini hili hakulitilia mkazo ukilinganisha na tamko la Gwajima linalohusu ndoto yake ya kuwabatiza Masheik nchi nzima, kisha kuigeuza misikiti kuwa Sunday- School ambapo watoto wa Kikristo watajifunzia elimu ya msingi humo.

Sasa Gwajima amepewa nafasi ya kupeperusha bendera ya CCM katika ngazi ya ubunge.

Je Waislam watakuwa tayari kuona misikiti yao kugeuzwa Sunday-school na wataamua kumchagua Askofu Gwajima atimize adhma hiyo?

Je Askofu Gwajima aliomba msamaha kwa yale matamko aliyoyatoa 2015, hivyo Waislam wasiwe na wasiwasi na misikiti yao kugeuzwa misikiti?

Je Masheikh na maimamu wapo tayari kubatizwa na kujisalimisha mbele ya Msalaba wa Bwana Yesu kama Gwajima alivyoeleza 2015?

Je Gwajima aliomba radhi kwa masheikh na maimamu kwa kauli zake kuhusu kuwapiga maji viongozi hao?

Kama Gwajima hakuomba msamaha kipindi kile ili asamehewe na Waislam, Je akiomba sasa hivi haoni kwamba ataonekana ni kwa sababu anataka kura?

Je Watanzania waishio Kawe wapo tayari kumuunga mkono Gwajima na kumchagua kuwa kiongozi wao licha ya kauli zake za kibaguzi dhidi ya waislam?

Baada ya maswali hayo.

Maoni yangu;

Binafsi Taikon nisingeweza kumchagua Gwajima hata kama ningekuwa nimechanganyikiwa, hata kama ningekuwa nimelewa kwa kunywa pombe, hata kama ningeshikiwa mtutu wa Bunduki.

Mimi ni Mkristo, lakini sipendi mtu mwenye mambo ya kibaguzi ya kidini. Taifa letu nila dini zote. Kwa bahati upande wa Baba yangu karibu wote ni Waislam. Baba yangu ni muislam, mashangazi wote ni Waislma. Kuwabagua waislam ni kubagua Baba zangu. Kuwabagua Wakristo ni kuwabagua mama zangu.

Mimi nisingemuunga Mkono Gwajima hata kama ningeambiwa ninyimwe pepo, ningekuwa tayari. Gwajima hafai kuchaguliwa kuwa kiongozi wa kisiasa.

Ifahamike kuwa, Gwajima ni mtu mzima, anaelimu ya kutosha, hivyo kile akisemacho anajua atahari zake, amedhamiria kwa ndani kabisa. Yeye ni mtu mzima kile akiongeacho ndicho kinachozunguka akili yake, ndicho kilichojaza moyo wake.

Gwajima atashindwa kutimiza lengo lake kwa sababu ya mipaka ya mamlaka lakini kama akiwa na nguvu zaidi anaweza kufanya kile akitakacho.

Wana KAWE Kama walivyo Watanzania wengine hawatakubali kumchagua mtu atakayeleta upuuzi ndani ya jamii. Mtu anapoongea jambo jua anaweza kulitekeleza, akishindwa ni kutokana na kutokuwa na nguvu.

Wakristo wote wenye akili kamwe hawawezi mchagua Gwajima achilia mbali ndugu zetu Waislam, na wale wasioamini katika dini.

Kuhusu msamaha.
Tunaweza kumsamehe, lakini hatutampa uongozi na kama yeye amedhamiria asamehewe basi asijisikie vibaya sisi kutompa uongozi.

Hata hivyo CCM nao wanashangaza mno, hivi wamekosa wa kumpa tiketi yao mpaka wampe Gwajima.

Je CCM hawajui ubaguzi alionao Gwajima?
Hawakusikia kauli zake za kugeuza misikiti kuwa sunday-school na kuwasilimisha masheikh na maimamu?
Je wamesahau matusi yake kwa Mzee wetu wa Heshima Kadinali pengo?
Je hawasikii skendo zake za umalaya Mpaka video za uchi? Je CCM wameamua kuuza jimbo kwa urahisi kwa HALIMA Mdee?

Je CCM hawakusikia tuhuma za Gwajima kuhusiana na kuchochea ukabila kwa vipeperushi na audio yake akihamasisha wasukuma kuungana na kunada vikundi vya watu 2000, mpaka jeshi la polisi likamkemea na kumuonya?

Je CCM wanafikiri watamsafisha Gwajima na watu kumuona Msafi kwa kauli zake hizo za ajabu?

Nauliza CCM wameamua kuuza Jimbo tena awamu hii?

Bora wangempa yule dogo aliyeshika namba moja kwenye kura za maoni. Lakini kwa Gwajima atapigwa mapema mno. Kabla Magari ya Mbeya hayajafika IRINGA Gwajima atakuwa ameshachezea.

Niwaombe Watanzania waishio KAWE wasimchague Gwajima, pia na majimbo mengine yenye wagombea wenye historia ya kauli za kibaguzi, iwe ubaguzi wa dini, ukabila, au ubaguzi wa namna yoyote ile.

Hii itakuwa fundisho kwa watu wa namna hii.

Kama kanisani kwake ndiko wanapenda ubaguzi apeleke huko huko.
Kama ni nyumbani kwake apeleke huko.

Asituletee mambo ya hovyo kwenye jamii yetu inayoishi kwa amani na upendo.

Kama alijichafua mwenyewe anapaswa ajisafishe, hakuna wa kumsafisha, yeye sio mtoto mdogo ili asafishwe. Angesafishwa kama angekuwa amechafuliwa. Lakini kwa mdomo wake alijichafua.

Mtu mzima haogeshwi.

HALIMA MDEE jikite kwenye sera kati ya hizi
1. Uhuru na Umoja
2. Upendo na mshikamano
3. KAWE ya watu wote
4. Sote ni ndugu n.k

Hiyo imeisha.

Katika haya Gwajima Mdomo hautakusaidia, pesa zako ni zako, jimbo nila wananchi. Kawe sio ya watu kama wewe.
Katika Hili nimejipambanua, wala sihitaji unafiki, Gwajima asiungwe Mkono, na watu wote waseme Amina.

Robert Heriel
Taikon wa Fasihi
0693322300
wewe ndugu ni mpumbavu tu kama walivyo wapumbavu wengine jana lilipotajwa jina la gwajima tu ukaandika unafanya kampeni mtu kwa mtu ili tu asipite kisa mkristo sasa amini usiamini huyo ndiyo mbunge wenu
 
Yaani usione Gwajima ndie mchochea chuki za udini halafu uje uone mleta mada ndie mchochezi? Yaani usiwashangae CCM wanaomteua mtu anayechochea udini na ukabila, unakuja kumuona mleta mada wa JF?!

Hivi nyie watu mmerogwa, au?!
Misikiti kugeuzwa Sunday-school

Kauli ya udini hii mkuu
 
wewe ndugu ni mpumbavu tu kama walivyo wapumbavu wengine jana lilipotajwa jina la gwajima tu ukaandika unafanya kampeni mtu kwa mtu ili tu asipite kisa mkristo sasa amini usiamini huyo ndiyo mbunge wenu

Naomba nisikujibu kuhifadhi heshima ndogo uliyonayo.

Ila ushauri, soma content uielewe ndio uchangie,
Nitashukuru ukinisikiliza kama unayoakili, karibu Mkuu
 
Uzi unachochea watu kama Gwajima wanaoendekeza ubaguzi wa dini na ukabila wasipewe nafasi kuongoza watu.

Uzi huu ni wakichochezi kama ulivyosema, lakini unachochea nini?

Hapo ndio unapaswa kujiuliza
Misikiti kugeuzwa Sunday-school

Kauli ya udini hii mkuu
 
Mie kwangu Gwajima sio; nabii, sio mtume wa Mungu, sio mjumbe wa Mungu hata chembe.
bali hutu mtu ni tapeli, msanii. mdanganyifu na muongo kupindikia!
'wanaosali' kwake ndio nawaonea huruma kwani sidhani kama wanajielewa vyema.
 
Kwa taarifa yako Gwajima hapo alipo anatakiwa akatubu, amemkosea Mungu muumba wa mbingu na nchi, alietuasa tusiwe vuguvugu, bora tuwe moto au baridi. Gwajima kwa kulimbilia siasa hapohapo bado ni kiongozi wa kanisa huyu mtu ni vuguvugu, hayupo duniani wala mbinguni.
Mkuu Gwajima sio mtumishi wa Mungu hata chembe, huyu ni msanii na muongo kama walivyo 'wale wengine'! Siku ya kiama hawa ndio wanakuwa KUNI.
 
Misikiti kugeuzwa Sunday-school

Kauli ya udini hii mkuu

Wewe kauli ya kidini unataka iweje?

Misikiti kazi yake ni nini?
Misikiti wa wanaingia watu gani?

Sunday school kazi yake nini?
Sunday school wanaenda watu wa aina gani?

Mtu akitamka hadharani msikiti ataugezwa kuwa sunday School, tena mtu asiyeingia msikiti, asiyemuislam, huoni analeta mushkeli kwa waislam?

Ulikuwepo 2015?

Kama ulikuwepo basi naomba nisikujibu tena. Kama hukuwepo, basi nasikitika kujadiliana na mtoto
 
Gwajima akimalizana na Masheikh aende kwa Wakatoliki, aeleze kwanini alimsema Kadinali Pengo amekula maharage? hii kauli ilikuwa ya kumdhalilisha mtu binafsi, na taasisi anayoiongoza.
Wakatoliki ni watu wa vitendo zaidi hawana muda wa kujibizana na mtu, wao wanakuadhibu kimya kimya
 
Bishop. Gwajima ndiye mbunge mta
JE, WAKATI UMEFIKA WA MISIKITI KUGEUZWA SUNDAY-SCHOOL NA GWAJIMA?

Na, Robert Heriel

Miaka mitano nyuma, naam mwaka 2015 Gwajima alionyesha dhamira yake na ndoto yake kubwa ambayo alitanabaisha kuwa anatamani Misikiti kuwa Sunday- School za watoto wa Kikristo, pamoja na masheikh na maimamu wakikimbizana kwenda mbele ya msalaba wa Bwana Yesu. Hii ilikuwa zama zile za ambapo Mzee Lowasa naye alijikita kwenye Dhana ya Ulutheri kuwa moja ya vigezo vya yeyey kuchaguliwa kuwa Rais wa Tanzania.

Moja ya watu waliojitokeza kumpinga Askofu Gwajima, ni pamoja na Imam Bukhary ambaye yupo pichani hapo.

Imamu Bukhary pia alieleza namna Gwajima alivyopinga uwepo wa Mahakama ya Kadhi. Lakini hili hakulitilia mkazo ukilinganisha na tamko la Gwajima linalohusu ndoto yake ya kuwabatiza Masheik nchi nzima, kisha kuigeuza misikiti kuwa Sunday- School ambapo watoto wa Kikristo watajifunzia elimu ya msingi humo.

Sasa Gwajima amepewa nafasi ya kupeperusha bendera ya CCM katika ngazi ya ubunge.

Je, Waislam watakuwa tayari kuona misikiti yao kugeuzwa Sunday-school na wataamua kumchagua Askofu Gwajima atimize adhma hiyo?

Je, Askofu Gwajima aliomba msamaha kwa yale matamko aliyoyatoa 2015, hivyo Waislam wasiwe na wasiwasi na misikiti yao kugeuzwa misikiti?

Je, Masheikh na maimamu wapo tayari kubatizwa na kujisalimisha mbele ya Msalaba wa Bwana Yesu kama Gwajima alivyoeleza 2015?

Je, Gwajima aliomba radhi kwa masheikh na maimamu kwa kauli zake kuhusu kuwapiga maji viongozi hao?

Kama Gwajima hakuomba msamaha kipindi kile ili asamehewe na Waislam, Je akiomba sasa hivi haoni kwamba ataonekana ni kwa sababu anataka kura?

Je Watanzania waishio Kawe wapo tayari kumuunga mkono Gwajima na kumchagua kuwa kiongozi wao licha ya kauli zake za kibaguzi dhidi ya waislam?

Baada ya maswali hayo.

Maoni yangu;

Binafsi Taikon nisingeweza kumchagua Gwajima hata kama ningekuwa nimechanganyikiwa, hata kama ningekuwa nimelewa kwa kunywa pombe, hata kama ningeshikiwa mtutu wa Bunduki.

Mimi ni Mkristo, lakini sipendi mtu mwenye mambo ya kibaguzi ya kidini. Taifa letu nila dini zote. Kwa bahati upande wa Baba yangu karibu wote ni Waislam. Baba yangu ni muislam, mashangazi wote ni Waislma. Kuwabagua waislam ni kubagua Baba zangu. Kuwabagua Wakristo ni kuwabagua mama zangu.

Mimi nisingemuunga Mkono Gwajima hata kama ningeambiwa ninyimwe pepo, ningekuwa tayari. Gwajima hafai kuchaguliwa kuwa kiongozi wa kisiasa.

Ifahamike kuwa, Gwajima ni mtu mzima, anaelimu ya kutosha, hivyo kile akisemacho anajua atahari zake, amedhamiria kwa ndani kabisa. Yeye ni mtu mzima kile akiongeacho ndicho kinachozunguka akili yake, ndicho kilichojaza moyo wake.

Gwajima atashindwa kutimiza lengo lake kwa sababu ya mipaka ya mamlaka lakini kama akiwa na nguvu zaidi anaweza kufanya kile akitakacho.

Wana KAWE Kama walivyo Watanzania wengine hawatakubali kumchagua mtu atakayeleta upuuzi ndani ya jamii. Mtu anapoongea jambo jua anaweza kulitekeleza, akishindwa ni kutokana na kutokuwa na nguvu.

Wakristo wote wenye akili kamwe hawawezi mchagua Gwajima achilia mbali ndugu zetu Waislam, na wale wasioamini katika dini.

Kuhusu msamaha.
Tunaweza kumsamehe, lakini hatutampa uongozi na kama yeye amedhamiria asamehewe basi asijisikie vibaya sisi kutompa uongozi.

Hata hivyo CCM nao wanashangaza mno, hivi wamekosa wa kumpa tiketi yao mpaka wampe Gwajima.

Je, CCM hawajui ubaguzi alionao Gwajima?
Hawakusikia kauli zake za kugeuza misikiti kuwa sunday-school na kuwasilimisha masheikh na maimamu?
Je, wamesahau matusi yake kwa Mzee wetu wa Heshima Kadinali pengo?
Je, hawasikii skendo zake za umalaya Mpaka video za uchi? Je CCM wameamua kuuza jimbo kwa urahisi kwa HALIMA Mdee?

Je, CCM hawakusikia tuhuma za Gwajima kuhusiana na kuchochea ukabila kwa vipeperushi na audio yake akihamasisha wasukuma kuungana na kunada vikundi vya watu 2000, mpaka jeshi la polisi likamkemea na kumuonya?

Je, CCM wanafikiri watamsafisha Gwajima na watu kumuona Msafi kwa kauli zake hizo za ajabu?

Nauliza CCM wameamua kuuza Jimbo tena awamu hii?

Bora wangempa yule dogo aliyeshika namba moja kwenye kura za maoni. Lakini kwa Gwajima atapigwa mapema mno. Kabla Magari ya Mbeya hayajafika IRINGA Gwajima atakuwa ameshachezea.

Niwaombe Watanzania waishio KAWE wasimchague Gwajima, pia na majimbo mengine yenye wagombea wenye historia ya kauli za kibaguzi, iwe ubaguzi wa dini, ukabila, au ubaguzi wa namna yoyote ile.

Hii itakuwa fundisho kwa watu wa namna hii.

Kama kanisani kwake ndiko wanapenda ubaguzi apeleke huko huko.
Kama ni nyumbani kwake apeleke huko.

Asituletee mambo ya hovyo kwenye jamii yetu inayoishi kwa amani na upendo.

Kama alijichafua mwenyewe anapaswa ajisafishe, hakuna wa kumsafisha, yeye sio mtoto mdogo ili asafishwe. Angesafishwa kama angekuwa amechafuliwa. Lakini kwa mdomo wake alijichafua.

Mtu mzima haogeshwi.

HALIMA MDEE jikite kwenye sera kati ya hizi
1. Uhuru na Umoja
2. Upendo na mshikamano
3. KAWE ya watu wote
4. Sote ni ndugu n.k

Hiyo imeisha.

Katika haya Gwajima Mdomo hautakusaidia, pesa zako ni zako, jimbo nila wananchi. Kawe sio ya watu kama wewe.
Katika Hili nimejipambanua, wala sihitaji unafiki, Gwajima asiungwe Mkono, na watu wote waseme Amina.

Robert Heriel
Taikon wa Fasihi
0693322300
Acha propaganda, Bishop. Gwajima ndio mbunge mtarajiwa wa Kawe kwa taarifa yako. Upende usipende..
 
Misikiti kugeuzwa Sunday-school

Kauli ya udini hii mkuu
Sasa ni nani alitoa hiyo kauli kama sio huyo huyo Gwajima?! Ndo maana nimekuuliza how come unamshutumu mtoa taarifa badala ya kumshutumu ya kumshutumu Gwajima aliekuwa ameongea hadharani kuhusu ndoto yake ya kugeuza misikiti kuwa sunday schools huku akiapa lazima ndoto itimie?!
 
Back
Top Bottom