Robert Heriel Mtibeli
Platinum Member
- Mar 24, 2018
- 40,153
- 93,069
JE, WAKAZI WA HAI WAMEZIDIWA AKILI NA WAKAZI WA MWANZA?
Na, Robert Heriel
Mambo yanazidi kubadilika kila siku, jana sio leo, juzi sio kesho. Mambo yanabadilika, wa juu anakaa chini, na wachini anakaa juu.
Watu wa Kilimanjaro ni moja ya jamii ya Watanzania waliobahatika kupata wasomi wengi sana hapa nchini kutokana na uwepo wa shule nyingi mkoani humo, Wilaya ya Hai ikiwemo.
Watu wa Kilimanjaro walikuwa wakiheshimika kutokana na sifa zao za uchapakazi, elimu, na utafutaji. Wakazi wa Mikoa mingine walitamani sana kuwa kama Wana Kilimanjaro, ipo mikoa imeiga mazuri ya wanaKilimanjaro na ninathubutu kusema imeweza na inaipita Kilimanjaro.
Pamoja na heshima kubwa waliyonayo watu wa Kilimanjaro lakini miaka ya hivi karibuni mambo yanageuka, shilingi inageuka upande mwingine. Hii ni kutokana na baadhi ya matukio yafanywayo na baadhi ya vijana kutoka mkoa huo.
Nitatumia mfano wa kilichotokea siku ya jana wilaya ya Hai, ambapo vijana wa Hai wameonyesha tukio la kijinga na kipuuzi ambalo wengi wasingedhani kama Wana Kilimanjaro wanaweza kulifanya.
Kuvamia na kuleta fujo kwenye msafara wa Tundu Lisu, sio Dalili njema hata kidogo, ni ishara kuwa zama zimebadilika, ile heshima kwa wana Kilimanjaro inaondoka kwa upesi Mkubwa.
Wana Kilimanjaro wa zamani kamwe wasingeweza hata kufikiri kufanya tukio la kipuuzi kama lile achilia mbali kwenda kabisa.
Vijana wa Hai wamezidiwa akili na vijana wa Mwanza?
Lisu alifika Mwanza, vijana wa Mwanza hawakujitokeza kumuona na kumsikiliza, sisemi hawamtaki au wanamtaka, hiyo ni siri yao. Lakini mbinu walioitumia ilikuwa ni busara, akili na hekima kubwa. Kuliko wangejitokeza kama na kumfanyia fujo zisizo za maana, huku wakijua huko ni kuvunja sheria,lakini pia ni kusababisha uvunjifu wa amani ambao unaweza kugharimu maisha ya Watanzania.
Vijana wa hai ninasema wamezidiwa akili pengine na vijana wa jamii nyingi Tanzania kwa sababu hii ni mara ya pili kwao kufanya matukio ya kipuuzi na kijinga kama haya. Walishawahi kumfanyia Mbunge wao wa Hai, Mhe. Mbowe, huku wakijua kabisa ni mbunge wao, kama wangekuwa na akili walau kidogo, wangefanya mambo hayo kwa utaratibu tuu uliozoeleka ambao ni kutokumchagua siku ya kupiga kura.
Mbona vijana wa maeneo mengine wametulia, wanajua kuwa hata kama mbunge hafai wanasubiri siku ya kura wamtoe madarakani na kumpa mwingine.
Vijana wa hai wameidhalilisha sana Kilimanjaro kwa ujumla, siku zote mtu anayetumia nguvu sana huwa na akili ndogo.
Wameonyesha kuwa ni watu wasio na akili
Wameonyesha kuwa wao ni watu wasio na elimu,
Wameonyesha kuwa wao ni watu wavurugu
Wameonyesha kuwa wao ni watu wasio na uvumilivu.
Ni wazi kuwa, kama matukio haya yakiendelea, heshima ya wana Kilimanjaro itazidi kushuka na wana Kilimanjaro watadharaulika.
Nafahamu, sio vijana wote wa hai wasio na akili, wapo vijana wanaojielewa, wenye elimu, wenye akili, wanaojitambua ambao wameudhiwa na kitendo walichokifanya wenzao ambacho kimedhalilisha wana Hai na wana Kilimanjaro kote Tanzania.
Pengine kuna mtu anayetaka kuishushia jamii ya wana Hai heshima, ionekane ni jamii ya hovyo, jamii isiyostarabika, jamii ya kipumbavu..
Mbona Mwanza walikauka, mbona Mwanza hawakujitokeza kabisa, Hiyo ndio akili.
Kama mtu humtaki usiende kwenye mikutano yake
Kama mtu humtaki usimchague siku ya kupiga kura
Kama mtu humtaki usiwe chama chake,
Mbona ni kazi rahisi tuu,
Na kama vijana hao walipewa heka basi ni wazi hela hizo zimenunua heshima yao.
Wewe ni Mwanachadema, huenda humpendi Magufuli, kwa nini uende kwenye Mkutano wake ukafanye fujo? Huoni kuwa wewe ni kichaa?
Wewe ni mwanaCCM huenda humpendi Lissu, Kwa nini uende kwenye Mkutano wake ukafanye fujo? Huoni wewe ni mwendawazimu?
Mtu kama humpendi achana naye, usijihusishe naye, usijihushe na mambo yake, muadhibu kwenye kura, hakuna atakayekulaumu. Hiyo ndio akili.
Hai imetia aibu
Hai imeidhalilisha Kilimanjaro
Hai imedhalilisha watu tunaotoka Kilimanjaro
Hai imetukosea heshima Watanzania
Hai inafanya Mikoa mingine ione kuwa kumbe inaiheshimu bure Kilimanjaro, kumbe wana Kilimanjaro wenyewe mambo yenyewe ndio hayo ya Utopolo.
WITO:
Kama humpendi Lisu usimchague
Kama Humpendi Magufuli Usimchague
Acha kuvunja heshima yako na amani ya nchi kwa upumbavu wako. Usitukane mtu, usilete vurugu kwa mtu, acha kutuletea uzwazwa wa familia yako. Linda amani, linda nchi yako.
Je, Wakazi wa Hai wamezidiwa akili na wakazi wa Mwanza na wilaya nyingine kwa tukio walilolionyesha? Majibu hapo chini.
Robert Heriel
Taikon wa Fasihi
0693322300