Je, wakazi wa Mbagala wataweza kutunza mabasi ya mwendokasi yenye viyoyozi na WiFi?

Je, wakazi wa Mbagala wataweza kutunza mabasi ya mwendokasi yenye viyoyozi na WiFi?

View attachment 3459127
Mabasi ya sasa.

View attachment 3459132
Hali ya usafiri wa mbagala.

Mabasi ya mwendo kasi njia ya mbagala yasiopungua 150 yameshaingia mjini.
Swali ni je wanambagala watakuwa na ustaarabu wa kuyatunza?
Mbagala huku kwetu tunaiita Sodoma, kule hakuna kabisa kinachoeleweka na watu hawataki maendeleo hata kidogo...wameridhika na kufuga majini tu na kupigiana kelele.
 
1 day, tunafatilia tukio hili kwa karibu sana
 
Sio mbagala tu Ila sisi watanzania ustarabu ni ziro
 
Huyu ni mtu binafsi atalinda vyake ili arudishe mkopo, apate faida, hivyo ukiharibu tegemea kulipishwa.
Wataojitoa ufahamu watajikuta ndugu zao wanalipia
 
Kazi ya kutunza magari ni ya wananchi au kampuni iliyopewa tenda? Waiweke taratibu na wazisimamie
 
Wenye mabasi ndio wanapaswa kutoa taswira au serikali kwa mfano kichora mistari ya watu kusimama kwa folen na unapofika unakaa nyuma ya mwenzako, utaratibu huo nimeuona Japan hata muwe wengi kama mchanga ukifika unaingia kwenye mchoro unaoonesha foleni. Na unaqeza kuta kqma kituo kinahudumia destination nyingi kila sehemu wana mistari yao, mfano kituo yanapita magari ya kimara, mwenge au yenye uelekeo mmoja wanatumia mistari ya uelekeo wao

Tuanze utamaduni wakupanga folen tutalinda sana magari hayo
Walete magari kwanza, foleni ni baada ya magari.
 
Sisi wakazi wa Mbagala tunasema kutunza mabasi sio kazi yetu. Wajibu wetu ni kulipa nauli tu. Tukilipa nauli na mkitupa huduma bora hamtajuta kuhudumia njia hii ila kinyume chake mtajuta. Sisi sio kama hao mazoba wa Kimara. Hivi kwani yale mabasi ya Kimara mbona yamechoka sana na wakazi wahuko ni wa hovyo aka sisi wa Mbagala?
 
Kwa uhaba. Wa usafiri ninao utambua pale mbagala hayo mabasi hayatoshi
 
Back
Top Bottom