Je, Walinzi wa Rais aliyefariki huhamia haraka kwa Makamu ambaye atakuwa Rais au ndiyo itakuwa imeshakula kwao?

Leo CCM imethibisha mwenyekiti wao mpya ni Samia, Ila katibu mkuu hakuwepo na hawajasema hatma ya Bashiru.
Kuna za chini chini nilizosikia kuhusu kutokuwepo Kwake leo hapo, ila kwa sasa naomba nikae Kimya huku nikiendelea Kujiridhisha nalo. Yajayo yanafurahisha / hayafurahishi Ndugu.
 
Wala comment yangu haikukuhusu mdogo wangu wewe ndio unaweza kuwa unawashwa

Wacha nikupuuze
 
Kila nikisoma mwandiko wako nakufananisha na dogo mmoja anaitwa MANASE
 
Acheni ujinga nyie vijana wa sasa.
Kumbe mnamiliki simu ila vichwani mko zero zero!

Kwa taarifa yenu hao ni wajiriwa serikalini na jeshini halafu ni watu wa rank za juu sio makabwela.

Isitoshe kuna wengine wataendelea kuishi chato kwa marehemu mpaka ukomo wa ajira zao yaani kustaafu.

Mishahara na allowance zao tu ni mtaji tosha.

Mleta hoja utakuwa umetokea kwenye hiki kijumba
[emoji116]
 
Kama walifanikiwa kufika hapo sio wajinga kama unavyofikiri kwa wadhfa huo sahau kurudi mtaani kwa dhiki labda kama wastaafu na maslahi watabakinayo.
 
Hiyo ishakula kwao.mama anao walinzi wa kike,isitoshe timu nzima ya walinzi akiwemo bonge watarudishwa makao makuu.ndio maana bonge alilia sana,kwa 2.kwanza kuondokewa na kipenzi cha watanzania,pili ulaji umeondoka.haya ndio maisha yetu wanadamu.sote tunapita njia tu hapa duniani.
 
Yule mrefu ndio alikuwa presidential unit commander(puc)...hawez kubaki na mama samia tena mara nyingi team moja umrinda raisi atakapotoka uingia timu nyingine....Hawa baada ya apa wanakuwa promoted most ov them wanaenda kuwa station security officers wa balozi nje ya nchi, wanaenda kuwa mabosi kwa maana ya appreciation, promotion na kupumzika
 
Tena nimedokezwa hivi sasa anakuja na best cream ya Vijana wa CDF Mabeyo kutoka pale Sangasanga ( Kizuka ) na Ngerengere Mkoani Morogoro ila wamepata Mafunzo ya kisasa kabisa kutoka nchi zilizoiva Kimedani na Kijasusi pia.
CDF hahusiki na kitengo cha kumlinda raisi Wala jeshi...ulinzi wa raisi upo chini ya mkurugenzi wa usalama wa taifa chini ya kitengo cha psu( presidential security unit).....
 
Bora kupumzika tu
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…