Je, Walinzi wa Rais aliyefariki huhamia haraka kwa Makamu ambaye atakuwa Rais au ndiyo itakuwa imeshakula kwao?

Je, Walinzi wa Rais aliyefariki huhamia haraka kwa Makamu ambaye atakuwa Rais au ndiyo itakuwa imeshakula kwao?

Wale walinzi wa kike wa Gaddafi ni makomandoo hasa.
Acha Uwongo duniani kote huwa hakuna Mwanamke Commando na hii ni kutokana na Maumbile yao na Mfumo wao Kibaiolojia.

Isipokuwa huwa wanapewa tu Matunzo ya Kiwango fulani cha Ukakamavu. Ukomando ni Habari nyingine. Mtafute Mwanajeshi yoyote au Mbobezi yoyote wa Masuala ya Kimedani ( Kijeshi ) akuambie.
 
Mpambe wa rais ni lazima awe kanali, sidhani kama
mpambe wa mama samia anacheo hicho
Kiitifaki ni Rais pekee ndiyo huwa anakuwa na Mpambe ( ADC ) huyo wa Kijeshi na Makamu wa Rais yeye hupewa Mlinzi Mwandamizi tu kutoka PSU.

Ila Makamu wa Rais Mama Samia Suluhu Hassan akiapishwa tu na kuwa Rais rasmi Kikatiba basi Kiutaratibu wa Kiitifaki nae atapewa Mpambe ( ADC ) wa Kijeshi ambaye bado atakuwa ni wa Kiume japo kuna uwezekano pia akawa ni wa Kike ( Mwanamke )

Ila hawa Walinzi wa Kike kutoka PSU watakuwa karibu nae ambapo anaweza kubakia huyu huyu Mmoja aliyenae sasa au nae akabadilishwa na akawekwa hapo Mwingine kutokana na Hadhi ya sasa ya Mama Samia.
 
Hujui Kitu Walinzi wa Raisi ni wa Raisi na Sio Makamu so transition power inahama na Walinzi wanabaki kwenye possition zao so Wa Aliyekufa wanamfuata Mother na Wale wa Mother watamfuata atakayeteuliwa Nchimbi 😉
Absolutely Rubbish. Kaa Kimya jifunze kwa waliokuzidi Ufahamu, Maarifa na Uzoefu Hopeless mkubwa Wewe.
 
Yale majamaa ma soldiers yenye combat sijui za nchi gani nitayamiss sana
Wataendelea kuwepo katika sehemu ya Ulinzi thabiti wa Mama akiapishwa. Wanatoka katika Kikosi Maalum cha Ulinzi wa Rais na hizo ndizo Uniforms zao. Siku hizi Idara nayo inazidi Kujiboresha japo huko nyuma (zamani) haikuwa hivi.
 
Kwa hiyo mnataka kutuaminisha Hawa Ni sawa na walinzi wa kk security?
Au mabaunsa wa baa za uswazi acheni uzwazwa wazee.
Anayewafananisha hawa Walinzi wa Rais ( kutoka Kikosi Maalum JWTZ na wenye Mafunzo thabiti ya VIP's Protection kutoka PSU chini ya TISS ) na Walinzi wa KK Security si tu atakuwa ni Mpumbavu Mwandamizi bali pia ana tatizo Kubwa sana la Akili na anatakiwa hivi sasa awe Wodini Mirembe akipokea Matibabu ya Awali.
 
Wale wanyarwanda wanarejea kwao.
Kazi waliyotumwa imeshaota mbawa.
Hatuwahitaji tena, aliyewaajiri ameshakufa.
Hakujawahi kuwa na Kikosi cha Ulinzi wa Rais chenye Askari kutoka Rwanda au Kwingineko. Na hii haitakuja kutokea ila tatizo lenu Watanzania mmekuwa wepesi mno Kuaminishwa Uwongo uliojaa Upumbavu kisha mnauamini 100% na kuanza Kuueneza.

Kusema kuwa Kikosi cha Ulinzi wa Rais wa Tanzania kina Askari kutoka Rwanda ni Kuidhalilisha kupita Kiasi Taasisi nzima ya Usalama nchini ( TISS ) na hata Jeshi la Ulinzi wa Tanzania ( JWTZ ) kwani hizi Taasisi Mbili Kubwa na Muhimu nchini zina Ushirikiano wa Kidhamana kwa Ulinzi wa Amiri Jeshi Mkuu na ambaye ndiyo Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.
 
Mi nitammisi yule jamaa mrefu mweusi ambaye mara nyingi kwenye matukio ya Rais akiwa kwenye watu wengi daima yeye huvaa miwani meusi huku akiwa anaongea na mic ya mkononi.

Afu yule mlinzi mwingine mpemba mwenye sigda, najua anaweza akabaki na Mama Samia kwakuwa wote ni wa njia moja.
Yule alishapewa u DC
 
Back
Top Bottom