GE2025 Je, wanaharakati wana haki ya kuzuia wengine wasipige kura?

GE2025 Je, wanaharakati wana haki ya kuzuia wengine wasipige kura?

Matukio, Taarifa, Habari na Mijadala ya Wananchi WAKATI wa Mchakato wa Uchaguzi Mkuu 2025

Je, wanaharakati wana haki ya kuzuia wengine kupiga kura?

  • Wana haki kuzuia wengine kupiga kura

  • Hawana haki kuzuia wengine kupiga kura

  • Sijui

  • Sijali

Results are only viewable after voting.
Mimi nachokiona hapa ni

Kilichoitwa "haki ya kupiga kura" ni kama matokeo ya mwisho ya mchakato mrefu wa jambo kubwa ambalo limetangulia, lakini huku nyuma kulikuwa kuna fundamentals kadhaa ya mambo ambayo yanaunda hiyo haki.

Naamimi kukiwa kuna mambo ambayo yanakiuka hizo fundamentals hauwezi kusema matokeo ya hicho kitu ni haki au utekelezaji wa hilo jambo ukaita ni haki.

Kwa mfano ikiwa kama itabainika waliokubaliana kusema "kupiga kura ni haki ya kila mtu mwenye umri kuanzia miaka 18" waliamua hayo maamuzi kwa kuangalia mambo ya msingi kama
  • Uhuru wa vyama vya siasa kushiriki bila kubughudhiwa
  • Uwazi na usawa wa tume ya uchaguzi
  • Fursa sawa kwa wagombea wote
  • Uhuru wa vyombo vya habari na wananchi kupata taarifa
  • Ulinzi wa haki za binadamu na usalama wa washiriki
  • Haki ya kuishi kwa kila mtu bila kuwepo kwa matukio ya utekaji dhidi ya wapinzani
Ikiwa misingi hii imekiukwa kwa mfano, vyama vikuu vya upinzani kuzuiwa, wagombea kukatwa bila sababu, au tume kuteuliwa na mgombea mwenyewe, basi haki ya kupiga kura inakuwa ni kivuli tu cha kuficha haki ya kweli.
Sawa.

Lakini wote hamjakubaliana kuwa misingi hiyo imekiukwa, na kama imekiukwa kwa kiasi gani, na je kiasi hicho kinatosha kuugomea uchaguzi, hili ni suala lenye figisu nyingi.

Kuna watu hawana hata taarifa za msingi kabisa.

Yani wewe kuwa na taarifa zaidi, kuwa mwerevu, kujua huu uchaguzi ni maigizo, hakukupi haki ya kumnyima haki ya kupiga kura mtu mjinga asiye na taarifa.

Kwa sababu ujinga haumuondolei mtu haki zake za kidemokrasia za kupiga kura.

Na kwa hiyo, katika mfumo wa demokrasia, mnakuwa mnabishana wote mkiwa na sauti sawa.

Na kwa vile wewe usiyetaka uchaguzi huna sauti zaidi ya anayetaka uchaguzi, huna haki ya kumnyima haki yake.

Bila kujali unachosimamia ni kweli au si kweli.

Kwa bahati mbaya demokrasia haijajengwa kwenye msingi wa ukweli uko wapi, imejengwa katika msingi wa kutafuta consensus, kutafuta majority rule, kutafuta minority rights.

Ndiyo maana mgombea mjinga, mwizi, muongo anayejua kufanya kampeni vizuri anaweza kupita na kuongoza watu, wakati mgombea mwenye busara, muadilifu, mkweli akatupiliwa mbali kwa sababu hajui kufanya kampeni vizuri.

Watu wanafanya kosa la kui confuse demokrasia kuwa ni mfumo wa kupata uongozi bora kabisa, uongozi wenye integrity kabisa, uongozi wenye efficiency kabisa, uongozi wa haki kabisa.

Demokrasia ni mfumo wa kupata uongozi uliokubaliwa na watu tu.

Ndiyo maana nasema kama kweli watu hawaukubali huu uongozi, hata uchaguzi wa figisu ukifanikiwa, watu wanatakiwa kuwa na njia ya kuiangusha serikali tu bila hata kujali mambo ya uchaguzi huu ambao wengi tunajua ni feki tu.
 
Nimeelewa jibu lako zuri sana.

In fact ukivyolijibu ni aina moja ya kuweka hoja ya nsingi ninayoilenga iwe wazi kabisa.

Kwamba, je, ukilazimishwa kufanya usivyotaka katika ichaguzi (kupiga kura kama hutaki kupiga, kutopiga kura kama unataka kupiga) utakubali?

Lakini swali unalolazimisha niulize si nililotaka kuuliza.

Nimeuliza swali nililotaka kuuliza. Na umelijibu vizuri tu kwa kusisitiza kanuni ya individuals roght.
Vipi ukiuliza kama nilivyokushauri unahisi hutopata majibu tarajiwa ambayo yatakidhi haja ya swali lako la thread hii?
 
Vipi ukiuliza kama nilivyokushauri unahisi hutopata majibu tarajiwa ambayo yatakidhi haja ya swali lako la thread hii?

Katika jibu lako umeandika mstari huu

"Lakini maamuzi ya mwisho yatabaki katika nafsi yangu."

Inaonekana wewe ni mtu unayeelewa umuhimu wa kila mtu kuwa na maamuzi yake binafsi na kuachiwa uhuru wa kufanya maamuzi hayo.

Nakuelewa sana, na mimi niko hivyo hivyo.

Na mimi pia napenda kuachiwa maamuzi yangu binafsi kuuliza ninachotaka kuuliza, si kuuliza unachotaka kuuliza wewe.

Swali ukiloshauri niukize ni swali tofauti kabisa na swali ninaloukiza mini na hata sioni unaonaje uhusiano.

Moja linaukiza ntu kama ataenda kupiga kura, lingine l8naukiza kama mtu anaona wasiotambua uhalali wa uchaguzi wana haki ya kuwashurutisha wanaotaka kupiga kura wasipige kura.

Haya ni maswali mawili tofauti kabisa.

Wewe ikiwa unataka sana kuona jibu la swali la "Je, utaenda kupiga kura". Unaweza kuanzisha uzi wako ukaliweka swali hili, watu watajibu.

Kuanzisha uzi hapa JF ni bure.

Katika uzi huu, mimi sina interest ya kujua kama watu watapiga kura au hawatapiga kura.

Interest yangu ni kujua kama watu wanaona wanaharakati wanaotaka kuzuia wengine wasipige kura wana haki hiyo au hawana.

Sasa kwa nini unataka nisiulize swali ninalotaka kuuliza mimi, unataka niulize swali unalotaka wewe?

Kwa mtu ambaye unaelewa uhuru wa mtu binafsi vuzuri sana kiasi hukubali wanaharakati wawanyime wanaotaka kupiga kura haki yao hiyo, huoni kuwa na wewe unaniingilia katika haki yangu ya kuuliza swali ninalotaka mimi, unanipangia swali unalotaka wewe ambalo mimi sijataka kuuliza?
 
hao ndio wanaharakati wabongo, wanajifanya wapigania demecrasia lakini kwa upande wao tu, wanajafinya wanapigania human right lakini ziwe kwa upande wao tu.
Hao sio wapigania demecrasia bali na wapigania maslahi yao kisiasa. niliwshtukia zamani sana mimi huwa nawapuuza tu, kwanza wana khulka za kibinsfsi sana, halafu hawawezi criticization hata kidogo, ukiweka comment wasioipenda kwenye page zao subiria block. wakati wao maisha yao yote ni ku criticize wenzao na wanajiona always wapo sahihi.
 
Mkuu,

Nimeandika tangu bandiko la kwanza kuwa kuandamana ni haki ya kikatiba na kibinadamu na hapo hakuna mjadala.

Watu wana haki ya kuandamana, mjadala wangu haupo hapo.

Mjadala wangu ni, je, wasioukubali uchaguzi wana haki ya kuwanyima wanaoukubali na wanaotaka kupiga na kupigiwa kura haki yao ya kupiga na kupigiwa kura?

Bila kujali uchaguzi ni halali au si halali, kuna watu wameukubali na wana haki ya kupiga na kupigiwa kura.

Je, wasioukubali uchaguzi huu ni halali wana haki ya kuwazuia waliokubali kupiga na kupigiwa kura na kuwafanya wasitumie haki yao hiyo ya kura?

..lakini sasa hivi wanaotishiwa ni wale wanaotaka kuandamana. Majeshi yote yameelekezwa kuwadhibiti wanaotaka kuandamana. Wanaotaka kupiga kura wao wana ulinzi. Sasa wanaotaka kuandamana wanalindwa na nani?
 
1.Hilo ni swali tofauti.

2. Nimelijibu hapo juu, kama haki ya kikatiba na kibinadamu wanatakiwa kulindwa na Polisi. Kama watalindwa hivyo hilo ni suala tofauti mimi sina mamlaka ya kuamua hilo.

3. Hujajibu swali la uzi huu umeweka swali lako tofauti ambalo nimelijibu unarudia kuliuliza.
 
..kauli za mamlaka ni kwamba watakaoandamana watauwawa. Na watakaopiga kura watalindwa.
 
..kauli za mamlaka ni kwamba watakaoandamana watauwawa. Na watakaopiga kura watalindwa.
Hizo tunazijua, tumezilaani, tumezijadili sana, na hata kwenye swali lako nimeshakujibu na kukupa msimamo wangu.

Ila, uzi huu haujajielekeza huko umejielekeza kwenye swali la juu hapo.

Ambalo mpaka sasa hujalijibu.
 
Mimi mara ya mwisho kupiga kura 2015(Nilikuwa nina imani kidogo na NEC) .......2020 sijapiga ,2025 sipigi(NEC iliyounganishwa na mifumo ya nida na sisiemu ,siendi kupiga).

Kwanini sijapiga 2020 na sitapiga 2025? Hakuna uchaguzi bali ni kupoteza muda tu maana kura yangu haina maana maana uchaguzi na matokeo tayari wanayo kwenye latop zao wanachofanya ni formality tu.
 
hao ndio wanaharakati wabongo, wanajifanya wapigania demecrasia lakini kwa upande wao tu, wanajafinya wanapigania human right lakini ziwe kwa upande wao tu.
Hao sio wapigania demecrasia bali na wapigania maslahi yao kisiasa. niliwshtukia zamani sana mimi huwa nawapuuza tu, kwanza wana khulka za kibinsfsi sana, halafu hawawezi criticization hata kidogo, ukiweka comment wasioipenda kwenye page zao subiria block. wakati wao maisha yao yote ni ku criticize wenzao na wanajiona always wapo sahihi.
Mkuu,

Hili suala la wanaharakati wa Tanzania kutaka demokrasia pale inapowafaidisha wao tu, ikienda tofauti na ajenda zao hawaitaki, naliona sana.

Hata kwenye hili suala la kuwalazimisha watu wengine wasipige kura naliona hili.
 
..demokrasia ya kweli ni faida kwa Watanzania wote, na sio kwa wanaharakati peke yao.
 
Mimi nachokiona hapa ni

Kilichoitwa "haki ya kupiga kura" ni kama matokeo ya mwisho ya mchakato mrefu wa jambo kubwa ambalo limetangulia, lakini huku nyuma kulikuwa kuna fundamentals kadhaa ya mambo ambayo yanaunda hiyo haki.

Naamimi kukiwa kuna mambo ambayo yanakiuka hizo fundamentals hauwezi kusema matokeo ya hicho kitu ni haki au utekelezaji wa hilo jambo ukaita ni haki.

Kwa mfano ikiwa kama itabainika waliokubaliana kusema "kupiga kura ni haki ya kila mtu mwenye umri kuanzia miaka 18" waliamua hayo maamuzi kwa kuangalia mambo ya msingi kama
  • Uhuru wa vyama vya siasa kushiriki bila kubughudhiwa
  • Uwazi na usawa wa tume ya uchaguzi
  • Fursa sawa kwa wagombea wote
  • Uhuru wa vyombo vya habari na wananchi kupata taarifa
  • Ulinzi wa haki za binadamu na usalama wa washiriki
  • Haki ya kuishi kwa kila mtu bila kuwepo kwa matukio ya utekaji dhidi ya wapinzani
Ikiwa misingi hii imekiukwa kwa mfano, vyama vikuu vya upinzani kuzuiwa, wagombea kukatwa bila sababu, au tume kuteuliwa na mgombea mwenyewe, basi haki ya kupiga kura inakuwa ni kivuli tu cha kuficha haki ya kweli.
Scars mara nyingi watu wanacheza na maneno ya vifungu vya sheria, kanuni au muswada kutokana na nia zao.
Nchi nyingi zilizokuwa na mfumo wa utawala fulani halafu ukabadilisha mfumo mwingine huwa na mapengo mengi katika ufanisi wake wa kiutendaji, kwani watu watakaokuwa wamepewa mamlaka ya kutunga hizo sheria kwa kiasi kikubwa hujipendelea wao kwa maslahi yao au wafuasi wao kuliko kuweka maslahi mapana ya nchi. Ni kweli Tanzania inahitaji katiba mpya na hili jambo liwe katika taratibu zetu katika dira yetu ya maendeleo tuwe na nafasi ya kubadilisha sheria na kanuni kutokana na hitajio la wakati huo kwa uwazi na uweledi wa hali ya juu. Tukiweka vitu vya msingi mahala pake basi mambo mengine yatakuwa yanafanyika yenyewe bila ya tatizo na huko ndipo tutakapokuwa na taasisi imara zenye kufanya mambo yake bila ya kuingiliwa katika uendeshaji wake.
 
Back
Top Bottom