Kiranga
Platinum Member
- Jan 29, 2009
- 89,019
- 156,726
- Thread starter
- #121
Mfano wako ni logical non sequitur fallacy kwa sababu suala la collaborators South Africa halikuwa na utata mkubwa.Kwanza kuweka rekodi sawa ni kwamba South Africa kulikuwa na collaborators wengi tu wa makaburu wakati wa apartheid, baadhi ya hao collaborators walikuwa ni machifu kama Zwelithini, watumishi na umma, jamii kama za Transkei, Ciskei, Venda and Bophuthatswana waliopewa uhuru ili wasipambane na makuburu.
Collaborators wa wakandamizaji huwa wanakuwepo katika kila harakati, iwe Zimbabwe wakati wa vita vya ukombozi, Kenya wakati Maumau movement au US katika harakati za civil rights movement.
Collaborators pia hutokana na mambo mengi ikiwemo maslahi ya kazi au biashara, uoga, ujinga, indoctrination, propaganda, ukabila, udini n.k Hata hivyo kuunga mkono oppressors kwa sababu zozote zile bado haiwezi kuwa justified kwa utetezi uliouweka hapa.
Ilikuwa vigumu sana kwa mweusi kusema ana support ubaguzi wa rangi kufalsafa tu, yeye si collaborator.
Suala hilo Tanzania lina utata mkubwa.
Mtu anaweza kusema yeye ana support CCM kifalsafa tu, si collaborator. Anaamini CCM inapitia a rough patch itajirekebisha na kwenye wapinzani hakuna uongozi bora kama inaoweza kuoat8kana CCM.
Huo ni msimamo w akifalsafa, ana haki ya kuwa na msimamo huo.
Mtu anaweza kusema ha support CCM yeye ana support chama cha upinzani na anaona upinzani unahitaji viti hata vichache bungeni kuichemsha CCM.
Huyo si collaborator wa CCM. Hiyo ni mpinzani.
Sasa mtu anayetaka upinzani uwepo bungeni kuichemsha CCM utamuitaje collaborator wa CCM?
Mfano wako ni logical non sequitur fallacy.
Unalinganisha vitu visivyolinganishika.
Kwa nini unajiona wewe ndiye mwenye monopoly ya ukweli na wengine wote wakiwa tofauti na wewe hawana haki?
Kwa nini inakuwa vigumu kukubali kuwa demokrasia inakutaka ujenge ushawishi, ukishindwa kujenga ushawishi watu wengine wana haki ya kuamua wanavyotaka bila kujali maamuzi yao ni sahihi au si sahihi?
After all, demokrasia si ni pa.oja na uhuru wa kufanya maamuzi yasiyo sahihi?
Au demokrasia ni lazima mtu afanye maamuzi sahihi, akikosea inakuwa si demokrasia?
Je, demokrasia inatoa haki ya watu kukosea?