Mkuu hujajibu swali, huko juu umewalazimisha watu wajibu swali lako bila kujali muktadha, uhalisia au contradictions za swali lenyewe sasa na wewe kuwa muungwana pia ujibu swali.
Una mtazamo gani kuhusu ANC kushughulika na Waafrika collabarotors wakati wa harakati za kupambana na makaburu wa apartheid Africa Kusini?
Swali lako ni logical non sequitur fallacy.
Kwanza kabisa South Africa watu weusi karibu wote walikuwa wameungana kupinga utawala dhalimu wa makaburu, kulikuwa na ubaguzi wa rangi, hakukuwa na argumentative debate kuhusu mtu mweusi anayewaunga mkono na kuwasaidia makaburu kuwa ni mtu mbaya.
Tanzania mambo hayako clearcut hivyo.
Kuna very complex issues, kuna Watanzania wanaona CCM imeleta mabadiliko despite matatizo mengi kuwa yapo, wanataka kuichagua CCM kwa sababu wao wanaona kuwa, kwa mujibu wao, kuna afadhali.
Inawezekana hawa hawana high standards kama zako za kukataa utekaji, kukataa ufisadi, lakini wanaona wamejengewa daraja, wameletewa umeme.
Hawa hujaungana nao kwenye mambo mnayoyataka, wanayoyataka wao ni mambo simple na wewe unayoyataka pengine ni makubwa sana kwao.
Sasa unalazimishaje kuwaita hawa collaborators? Wengine hawajioni kuwa wanapigia kura CCM iwateke, wengine wajinga hawaamini CCM inateka watu. Hawajui ufisadi unaoanikwa na Mange. Hawajui hata kufuatikia mambo.
Sasa utawaitaje collaborators watu hawana hata information, hawana priorities kama zako?
Don't you see tgat you could be blaming the victim here?
Haya, kuna wengine wanaamini kuishinda CCM ni lazima uingie kwenye uchaguzi. Bila kujali hoja hiyo ni sahihi au si sahihi, ni hoja yao, wana haki ya kuitumia haki yao ya kupiga kura kuitimiza hoja hii.
Sasa hao wanaoamini wanaweza kuitoa CCM kwenye uchaguzi, wrongly or rightly does not matter. What matters is wanaamini hivyo, utawaitaje collaborators?
Unamhita mtu collaborator kwa sababu ana falsafa tofauti na wewe?
Na yeye akikuita wewe collaborator wa CCM kwa sababu unaisaidia CCM kushinda uchaguzi kirahisi bila hata kufanya kazi kubwa kwa sababu umesusia uchaguzi, utasemaje?