GE2025 Je, wanaharakati wana haki ya kuzuia wengine wasipige kura?

GE2025 Je, wanaharakati wana haki ya kuzuia wengine wasipige kura?

Matukio, Taarifa, Habari na Mijadala ya Wananchi WAKATI wa Mchakato wa Uchaguzi Mkuu 2025

Je, wanaharakati wana haki ya kuzuia wengine kupiga kura?

  • Wana haki kuzuia wengine kupiga kura

  • Hawana haki kuzuia wengine kupiga kura

  • Sijui

  • Sijali


Results are only viewable after voting.
Kwahiyo sasa hivi ata tukimaliza ibada tunaanz akuongelea uchaguzi?

Tukimaliza kuzika ni uchaguzi?

Sio kwamba kila mahali watataka kusikia hizi habari!
Kwani kuna mtu kakulazinisha kuchangia uzi huu?
 
Hivi kua mwana harakati ni kosa huyu jamaa anafanya wana harakati waonekane ni watu wabaya shame on you kiranga
Mkuu hili neno wanaharakati nashindwa kufahamu huwa unamaanisha kina nani. Juzi ulikuja na habari kutoka kwa page ambayo hakuna anayejua ni ya nani lakini ukaipa jina la mwanaharakati.

Naomba unijuze hao wanaharakati wanaosema wana haki ya kuvuruga uchaguzi. Ikiplendeza uweke na rejea za hao wanaharakati waliosema hivyo
 
Kama lengo ni kulinda haki ya kila mtu, basi maandamano hayawezi kufanyika siku yoyote.

Yakifanyika 1 disemba, bado kuna watu watanyimwa haki ya kutumia barabara na mambo mengine

Nadhani hapa itumike kanuni ya kuangalia faida kubwa au manufaa zaidi.
 
Ukienda kwenye uchafuzi 2025 ni either
1. Masikini wa mali na akili.
2. CCM maslahi
3. Umeshikishwa mshiko , umenunulika kwa vipande vichache vya fedha.

Otherwise huu ni UCHAFUZI na sio UCHAGUZI.
 
Hoja si maandamano. Maandamano tushakubali ni haki ya kikatiba na kibinadamu.

Mimi siona mjadala kwenye maandamano.

Hoja ni wanaharakati kuzuia watu kupiga kura.

Ni sawa au si sawa?

Umeelewa tofauti?

Hoja si uchaguzi una maana au hauna maana.

Hata kwenye uchaguzi usio na maana.

Je, wanaharakati wana haki ya kuzuia watu kupiga kura ikiwa watu wameamua kupiga kura katika uchaguzi usio na maana?
Je hawa wana haki ya kuzuia wengine kuandamana wanaopiga maandamano marufu wana haki hiyo?
 
Hakuna atakaeweza kumzuia mtu kipiga kura, Hawa Nyumbu wa mtandaoni hawawezi hata kuua sisimizi siku hiyo
 
Hakuna atakaeweza kumzuia mtu kipiga kura, Hawa Nyumbu wa mtandaoni hawawezi hata kuua sisimizi siku hiyo
Sawa.

Swali si wanaweza au hawawezi.

Swali ni, wana haki ya kuzuia au hawana haki hiyo?

Kuweza na kuwa na haki ni masuala mawili tofauti.

Inawezekana usiweze kununua gari, lakini ukawa na haki ya kununua gari.
 
Sawa.

Swali si wanaweza au hawawezi.

Swali ni, wana haki ya kuzuia au hawana haki hiyo?

Kuweza na kuwa na haki ni masuala mawili tofauti.

Inawezekana usiweze kununua gari, lakini ukawa na haki ya kununua gari.
Suala la kupiga kura ni haki ya kikatiba kumzuia mtu kupiga kura au kumshawishi asipige kura ni kosa, kwahiyo hawana haki.
 
Hakuna mwenye haki ya kunilazimisha kupiga kura wala kutopiga kura, ila kuna wale wenye uwezo wa kunishawishi kwanini nikapige kura au kwanini nisiende kupiga kura! Lakini maamuzi ya mwisho yatabaki katika nafsi yangu.

Nafikiri swali lilipaswa liwe utaenda kupiga kura? Uweke NDIYO na HAPANA then angalia nafsi za watu wasiolazimishwa wamefanya maamuzi gani.
 
We takataka ya maccm kwan ni nani kazuiliwa kupga kura? Nyie si ndo mko busy na viongoz wa chadema hata hamtaki waende misibani wanaojpanga kuandamana si ni watz na si wanachadema pekee sa hz hisia znatoka wp..
 
Mkuu,

Nenda Clubhouse Clubs za mtu anaitwa Abihudi kamsikilize anafundisha wafuasi wake kufanya violent disruption,kutumia silaha, kutengeneza Molotov cocktail bombs.

Zaidi, tunaweza kuzungumzia hoja kwamba jambo hili ni sahihi au si sahihi, si lazima kitu kifanywe na mtu ili tuweze kujadili usahihi wake.

We can think in the abstract now, can't we?

Abihudi ndo wanaharakati? Your entire thread is based on a false premise.
 
Abihudi ndo wanaharakati? Your entire thread is based on a false premise.


1. Abihudi ni mwanaharakati, amehusika katika harakati nyingi na mpaka sasa anahusika bado. Anachangia vyama vya siasa na movements nyingi, kuanzia pesa mpaka tactics.

2. Pia, thread haijaandikwa kwa premise ya Abihudi tu. Kuna wanaharakati wengi wanasema ni haki yao kuvuruga uchaguzi, si kuandamana tu.

3. Zaidi, nimeandika hapo juu na hata kwenye original post kuwa napenda kufanya mazungumzo ya kifalsafa na kidhahania.

Kwa point hii, mazungumzo haya hayajali kama waharakati hao wapo au hawapo ila yanajali kwenye dhana kuwa hii haki ipo au haipo.

Mfano mtu anaweza kuwa anataka kuamua avuruge uchaguzi au asivuruge, kwa kuangalia haki iko wapi, uzi huu unaweza kumpa mambo ya kujielimisha haki iko wapi hata kama hakuna mwanaharakati hata mmoja ambaye anaenda kuvuruga uchaguzi.

Tatizo la watu wengi wa aina yako ni kuwa hamna uwezo wa kufanya fikra dhahania.

Na hili nililijua tangu nabandika original post ndiyo maana nikasisitiza naomba mazungumzo yawe ya kifalsafa na kidhahania.

Ila umefeli mtihani huu wa kufanya mazungumzo ya kifalsafa na kidhahania.

You and many other like you here have proved that you are incapable of a philosophical and abstract exchange.
 
Cha kwanza watakao zuia watu wasipige kura siyo wanaharakati bali ni sisi wananchi na tarehe 29 tunakiwasha

Tumeshaandaa mipango yote ya kuchoma kituo cha kura kilichopo hapa mtaani na hata mwenyekiti wa mtaan anajua
Kituo gani hicho mkuu?

Tuweke rekodi sawa baada ya uchaguzi turejee kuangalia kama kituo kimechomwa moto kweli au haya ni maneno ya mitandaoni tu.
 
Umekosa uelewa kichele tu mzee, Mwanaharakati hajasema kuwa hatopiga kura bali anasema kuwa hakuna uchaguzi bila reforms sasa kama Reforms hamna wewe unaehisi kura kupiga kura bila Reforms ni haki yako utuambie umejipanga vipi kuilinda kura yako nje na hapo means unasupport mfumo mbovu uliopo... Na kiukweli nafasi ya kukudunda ikipatikana naunga mkono.
 
Back
Top Bottom