Nyangumi
JF-Expert Member
- Jan 4, 2007
- 507
- 18
To me the question is, tunajuaje kilichobora ambacho chapaswa kuchukua nafasi badala ya CCM na viongozi wake? Je tunatafuta chama au watu?
Kama mfumo wa CCM ungekuwa unaruhusu kupatikana kwa watu safi, kisha wakatuongoza Watanzania bila kuwa influenced na maslahi ya Chama au kundi la watu ndani ya Chama then tatizo lingekuwa dogo.Lakini mfumo unaotumika kuwapata,kuwaingiza viongozi wa CCM madarakani ni mchafu, hakuna msafi atakayepatikana.
Watanzania tunatafuta watu na si chama, lakini ni vizuri pia tukaelewa watu hawa bora tunaowahitaji hawapatikani ndani ya chama kibovu,kichafu ,kilichokwisha oza(CCM).Mkebe wa kufyatulia keki yetu ni mbovu, hivyo hata tukifyatua keki ingine kwa mkebe uleule dosari itakuwa palepale.Tunahitaji keki isiyo na dosari na hii itapatikana kwenye mkebe usiokuwa na dosari.