Wahuni kwa maana ipi?Hii mada ndipo ilipofikia, kuwa shoga sidhani.
Ki ukweli malezi ya watoto ni suala mtambuka. Nakumbuka wakati nakua miaka ya tisini mwanzoni nilikuwa na kampani ya wahuni wahuni tu ambao walikuwa wanawaza HipHop na kutoboa maisha kama Black Americans.
Wengi wa washikaji zangu walizamia mamtoni, wamezamia kama wana 10+ hadi leo haijulikani kama wapo hai au wamekufa.
Wawili tu ndio tunawasiliana, mmoja yupo Ujerumani mwingine yupo Norway. Nilikuwa na kampani ya wahuni pale Upanga kabla ya kuhamia Ilala mwaka 1993.
Hahaha , hawa madogo wanatakiwa mboko sana😁'Bila Kunyukwa'😀 ishakuwa Imani tena. Nahisi tunahitaji huduma ya ushauri nasihi
Kupiga mtoto at first hand naona haijakaa sawa isipokuwa tu kwenye attempts za uzembe. Mtoto alishafanya kosa hilo hilo mara mbili au zaidi hizo ni signs of negligence of which sio tabia nzuri kwa mtoto kukua nazo. Mara zote ulishamkanya ila anakuwa mzito kuelewa ni lazma umshtue kidogo.
Africa genetically tuna hizo element za kufanya mambo ya uzembe ikiwa hakutakuwa na gharama za maumivu kwa namna fulani.
Wazungu wao wana condition watoto in another way round. Hawa impose physical disturbance ila psychologically kama ku deny mtoto kufanya michezo flani kama way of punishment. Hawaruhusiwi kupiga ila adhabu wanatoa.
Sure wanakuja kuishi maisha ya hatari na magumu mno...Niliwahi kukutana na jamaa wakati tunasoma dingi yake alikuwa balozi nchi za SADC huko ,sijajua nini kilitokea nilikuja kukutana nae amechoka balaa,amevaa sagula sagula wakati zamani alikuwa anapiga high brands ,chini amepiga yebo yebo za buku 2 mia tano,anatembea kwa mguu kama yule mtu ambae anatafuta mishe ya kufanya yeyote apate hela ya kula.Hawa watoto wanaolelewa hivi ndio mwisho wazazi wakipata ajali ghafla wakafa huishia kutaabika sana na dunia
Acha kabisa, mimi kuna dogo mzee wake alikuwa kaimu pale TPA miaka ya 1990s ile. Jamaa alikuwa na mawe sana yani af maza alikuwa business woman. Ogopa dogo anasoma chekechea za ada laki 6 miaka ile. Mpaka kufikia 2003 story ikaflip back. Maza alidanja late 2001 na mshua 2002 kesi ikiwa ni umeme. Kama unavyojua kilovolt za miaka ile ilikuwa ni miez 6 tu watu wanafunga hesabu.Sure wanakuja kuishi maisha ya hatari na magumu mno...Niliwahi kukutana na jamaa wakati tunasoma dingi yake alikuwa balozi nchi za SADC huko ,sijajua nini kilitokea nilikuja kukutana nae amechoka balaa,amevaa sagula sagula wakati zamani alikuwa anapiga high brands ,chini amepiga yebo yebo za buku 2 mia tano,anatembea kwa mguu kama yule mtu ambae anatafuta mishe ya kufanya yeyote apate hela ya kula.
Ewaaaaa!!!!Kutoa huduma ni kufuga mtoto. Ni sawa na mbwa unampa chakula na chanjo ila anajiongoza mwenyewe😁
Kuna nchi duniani zimeondokana na adhabu ya kuwachapa watoto iwe shuleni au nyumbani. Yaani ukimchapa mtoto ni at your own peril. Na hii inatokana na studies mbalimbali kwamba kumpiga mtoto ni ku'induce' violence kwenye hisia zake ili na yeye akikua aweze kuwa 'violent'. Ndiyo maana watoto ukiwaacha pamoja utaona baadhi yao ni wapole, lakini wengine ni violent - wanapenda kuwapiga wenzao, kunyakua vitu vyao au kuziharibu bila sababu.Kwa nchi yetu Tanzania vipigo kwa watoto inaonekana ni jambo la kawaida sana, na huku baadhi wakipongeza jambo hilo kwa kuona ndio msingi bora wa malezi kwa watoto unaowafanya kuwa na maadili, hofu, kusikiliza na kutekeleza maagizo ya wazazi aidha kwa kutaka au kutokutaka kwa kuogopa kuadhibiwa kwa vipigo.
Mkuu, sisi ni waafrika tena watanzania, mimi nalea vile naona ni sahihi kwangu, mambo ya wageni waje watoto waanze kumwsga vyakula kisa hawapigwi hapana kwa kweli lazima mtoto ajue mipaka yake kwake na watu wanaomzunguka au hata watu wapya kwake mtoto ukimchekea lazima akuendeshe tu mnasahau nyie ndio wahenga mkasema samaki mkunje angali mbichi?Ahsante Sana kwa neno. Nadhani pia, katika kutoa adhabu kwa watoto, wengi wetu hatuna kabisa ufahamu kuhusu hata Sheria ya mtoto inasemaje na tafiti kuhusu mengi kwenye malezi na makuzi. Mara ingine tunasahau kuwa, huenda kuna watoto wagumu kwa Sababu zingine ambazo zinahitaji mtaalamu kuzibaini, kuna wenye shida ya afya ya akili, utapiamloa ulioathiri makuzi ya mifumo ya akili, kuna wazazi na Walezi pia Wana dhida zao vilevile, yaani unaweza Kuta mambo ni vurugu na mtoto haelewi na mzazi haelewi na vipigo vikizidi mtoto anakimbia nyumbani anaingia mtaani anajifunza mabaya zaidi basi mzazi naye anasema nimemsusa.
Mara ustawi wa jamii wakimchukua wakimpeleka kwenye program za marekebisho ya tabia mtoto anasimulia mambo makubwa, hatimaye anafunguliwa anarekebishika, kumbe tunaweza kutoa adhabu fulani za kiwango cha mtoto na ikishindikana basi tukumbuke kuna sayansi nyuma ya malezi na makuzi ya mtoto na kuna program za marekebisho ya tabia kitaalamu. Ngoja niwape hapa kipande cha Sheria kwa wale wanao amini kwenye ukibisha nakupiga tu Bora nifungwe👇 naamini itafunguka.
Ajabu sanaa hii....ila kwa Kila kinacholetwa na Hawa watu...nyuma yake kuna ajenda ambazo kwetu zitaja tugharimu tuNashangaa sana sijui ni lini tutaanza kujiamlia na sisi mawazo yetu. Kama na kuleta napo tufundishwe Nini maana ya kuwa mzazi sasa.
Swadakta ndugu... Hiki ndio mtu ambacho nawaambia Hawa wazazi wa kisasa wanaojikuta wazungu.Kama mnaona mboko hazifai futeni na magereza.
Swadakta ndugu... Hiki ndio mtu ambacho nawaambia Hawa wazazi wa kisasa wanaojikuta wazungu.
Kama mtoto haitaji kuchapwa au kuadhibiwa kinguvu kwa namna yoyote ile basi hakuna haja ya kuwa na vyombo vya dola kama police ambavyo vinatumia nguvu kwenye kutekeleza majukumu yao maana hata kumwelekeza mtu mtu kwa mdomo na asifanye maovu inatosha kabisa...
Na hayo magereza pia ni upotevu wa mpesa tu kwa sababu binadamu haitaji matumiz ya nguvu kumrekebisha tabia.....
Haya Hawa jamaa hoja zao zinafungua mjadala mpana sana ambao nna uhakika hawana uwezo wa kuujadili na ukafika mwisho wenye mantiki.
Lazima bila kuwa na akili zetu waafrika tutapelekwa sana. Hawa tunao amini ndo viongozi wetu na wasomiAjabu sanaa hii....ila kwa Kila kinacholetwa na Hawa watu...nyuma yake kuna ajenda ambazo kwetu zitaja tugharimu tu
Kinachonishangaza huyu Dkt.Gwajima na wenzake hapa wanasema zipo njia na programs mbali mbali za malezi ambazo ni Bora zaidi ya adhabu ya viboko, lakini hata hawazisemi hizo njia zenyewe.mkuu, sisi ni waafrika tena watanzania, mimi nalea vile naona ni sahihi kwangu, mambo ya wageni waje watoto waanze kumwsga vyakula kisa hawapigwi hapana kwa kweli lazima mtoto ajue mipaka yake kwake na watu wanaomzunguka au hata watu wapya kwake mtoto ukimchekea lazima akuendeshe tu mnasahau nyie ndio wahenga mkasema samaki mkunje angali mbichi?
Kuna mwanazuoni mmoja aliwahi kuniambia kuwa hapa duniani mwafrika ni mtu ambaye ataendelea kudharuliwa na binadamu wa race zingine zote na ni haki yake kumdharauliwa..Wala sio kwamba wanapenda ni hivi kuna nguvu inawapush {hela}za mashirika ndio maana wanakaza mafuvu yao humu.
Hizo ni kampeni mkuu huanza hivi hivi badae litaenda bungeni na kuptishwa. kama wanaamini binadamu ni kuelekezwa tu bila fimbo magereza na huku nzito hadi kunyongwa za nini?
Waache tamaa za pesa
Nunua vitu vya jumla weka ndani acha kumtuma mtoto vitu rejaja dukani mara sukari robo, mara kiberiti kimoja, mara chumvi pakiti moja n.k
Wakati unampa hili pendekezo Dkt.Gwajima wa kufuta viboko mashuleni, mpe na alternativeya viboko kabisa hapa hapa na sio eti unamwambia aende akijifunze kwenye shule za watu binafsi, na vipi kama maisha wanaishi hao watoto wanasoma shule za Tibaijuka hayaendani na maisha ya watoto wengi wa kitanzania??? Je, umewaza Hilo au wewe akili yako imejikita kwenye matokeo tu unayaona kwenye hizo shule za Tibaijuka??Nashukuru hapa tuko na mama Dkt. Gwajima D atusaidie kupeleka muswada bungeni wa kufuta sheria ya viboko mashuleni, tena iwe ni kosa la jinai kumpiga viboko mtoto akiwa shule.
Kama hawawezi kufundisha watoto bila kuwararua na viboko ni HERI HIZO SHULE ZIFUNGWE KABISA.
Kuna shule za binafsi nyingi zikiwemo zinazomilikiwa na Mh. Anna Tibaijuka zinaendeshwa bila viboko na zinafanya vizuri tu kimaadili na kitaaluma. Tuige hiyo model, nendeni mkafanye utafiti kujua wamewezaje.
Viboko havijengi maadili, vinajenga NIDHAMU YA WOGA.
Waziri tunaomba mkafute ile sheria ya kikoloni.
Wakati unampa hili pendekezo Dkt.Gwajima wa kufuta viboko mashuleni, mpe na alternative ya hiyo njia ya viboko kabisa hapa hapa na sio eti unamwambia aende akijifunze kwenye shule za watu binafsi, na vipi kama maisha wanaishi hao watoto wanasoma shule za Tibaijuka hayaendani na maisha ya watoto wengi wa kitanzania??? Je, umewaza Hilo au wewe akili yako imejikita kwenye matokeo tu unayaona kwenye hizo shule za Tibaijuka??Nashukuru hapa tuko na mama Dkt. Gwajima D atusaidie kupeleka muswada bungeni wa kufuta sheria ya viboko mashuleni, tena iwe ni kosa la jinai kumpiga viboko mtoto akiwa shule.
Kama hawawezi kufundisha watoto bila kuwararua na viboko ni HERI HIZO SHULE ZIFUNGWE KABISA.
Kuna shule za binafsi nyingi zikiwemo zinazomilikiwa na Mh. Anna Tibaijuka zinaendeshwa bila viboko na zinafanya vizuri tu kimaadili na kitaaluma. Tuige hiyo model, nendeni mkafanye utafiti kujua wamewezaje.
Viboko havijengi maadili, vinajenga NIDHAMU YA WOGA.
Waziri tunaomba mkafute ile sheria ya kikoloni.
Hicho unachoona wewe mateso na komwe lako Kama harage hichi nawakati umezaliwa tandale kwa tumbo jirani na mzee chilemba mwingi wa maniiKwa nchi yetu Tanzania vipigo kwa watoto inaonekana ni jambo la kawaida sana, na huku baadhi wakipongeza jambo hilo kwa kuona ndio msingi bora wa malezi kwa watoto unaowafanya kuwa na maadili, hofu, kusikiliza na kutekeleza maagizo ya wazazi aidha kwa kutaka au kutokutaka kwa kuogopa kuadhibiwa kwa vipigo.
Kuna baadhi wamekuwa wakijisifu kuwa wao hawacheki na watoto kwani wao ni fimbo mkononi huku wakirejea maandiko kutoka kwenye vitabu vya dini kuwa Usimnyime mtoto mapigo na hivyo kuona kaaa walipewa ruksa ya kuwadunda watoto vilivyo kutoka kwa Muumba wao.
Hali hiyo imekuwa ikifanya watu wanaolea watoto bila kuhusisha vipigo kutuhumiwa kuwa wanawaharibu watoto, wanawadekeza na kwamba wanafata utamaduni wa wazungu ambao hauwezi kufanya kazi kwa watoto wa kiafrika hususani Watanzania, Wazazi wa aina hiyo wamekuwa wakituhumiwa kuzalisha watoto watakaokuja kuwa wa ovyo wasio na maadili wenye matendo mabaya.
Je, watu wote wasio na maadili waliopo ni zao la wazazi ambao hawakuwapiga watoto wao?
Je, hakuna watoto waliopigwa na hawakuwa na maadili licha ya vipigo vikali?
Ni kweli kipigo ndio suluhisho la maadili na usikivu kwa watoto?
Ni kweli hakuna watoto wanaolelewa bila vipigo na kuja kuwa watu wema?
Pamoja na yote wanaosifu vipigo kwa watoto huwa hawataki kabisa kuzungumzia athari hasi ya vipigo hivyo kwa watoto, na pengine hawatambui kuwa zipo. Je, hakuna namna ya kuweza kuwalea watoto bila kuhusisha vipigo?
Pia soma: Je, ni kweli Adhabu ya Viboko inasaidia kuongeza Nidhamu na Uelewa kwa Mtoto?