Je, Watoto wanaolelewa bila vipigo hawana maadili?

Siku ya kwanza kwenda shule mzazi anakuambia uwe makini wasije wakakuibia .

Hapo ukiangalia unaenda boarding school πŸ€”πŸ€”πŸ€—πŸ˜ maadili sisi hatuna
Mkuu ninao marafiki zangu huwa wanatamani sana wawe kama sisi , ndio maana nchi nyingi za ulaya na America kwa sasa wanavutiwa ki mahusiano na watu kutoka Africa sababu ni hiyo ya maadili.

Mume kupewa pole au kuulizwa kama amekula ,hiyo kwa wenzetu ni kituko sisi bado tupo kwenye reli mkuu😁😁😁
 
Watoto wanatofautiana sana. Ni ngumu wote kufit kwenye mfumo mmoja.

Nawafahamu watoto kadhaa ambao hawajawahi kuchapwa na wana maadili mazuri kuliko watoto wanaochapwa. Hao ni watoto wa marafiki zangu ambao ni wazungu waliooa wabongo.

Tatizo kubwa la wabongo wasiochapa ni kuwa wanadekeza. Mtoto haambiwi limits zake. Anajihisi malkia au mfalme ndani ya nyumba.

Wenzetu hawachapi lakini hawadekezi, wengi wao wako firm na wana rules za familia wanafuata.
 
Hizo nchi ambazo watoto hawachapwi zina mmonyoko mkubwa wa maadili pia ,sisi tunajiona hatuna maadili ila ukitembelea kwa wenzetu utaona bado sisi tuna maadili sana😁
Nimeishi na waarabu hawana tabia hizo za kuchapa na watoto wao wamenyooka balaa! Wajapani nao pia hawana tabia hizo ila ndio wanaongoza duniani kuwa na discipline. Mi nadhani waafrica hatutaki kutoka nje ya box kifikra kufikiria njia mbadala za malezi isiwe lazima fimbo pekee yake. Halafu pia si waafrica muda wa kukaa na watoto wetu sometimes unakuwa ni changamoto sana nadhani hii pia inachangia
 
Hahaha inaleta maana mkuu, kuna siku tulitembelea hifadhi fulani tukaona sokwe anamchapa mwanae bakora za kutosha😁😁
 
Waafrika wengi kutumia akili na kufikiri nje ya box ni kama kujichosha na kupoteza muda
 
Kuna watu wanachapa hadi wake zao na hawaelewi ukiwaambia mwanamke hatakiwi kuchapwa!🀣
Kwa kina FaizaFoxy maustadh wanatembeza mboko vibaya sana madrasa!
 
Waafrika wengi kutumia akili na kufikiri nje ya box ni kama kujichosha na kupoteza muda
Sie waafrika kukuta baba amerudi nyumbani mapema anawaita watoto wake na kuwauliza wana changamoto gani wanazopitia huwa ni nadra sana! Huwa ni mwendo wa amri na vipigo tu! Kumbe sometimes kuna changamoto watoto wanapitia zinazofanya wawe na tabia za ajabu.
 
Fimbo kwa watoto ni tabia za kijima za karne ya 17, ni jambo la hovyo sana kumchapa mtoto, wanaochapa watoto wenyewe wengine ni walevi wa kupindukia, mafisadi, wachepukaji, wakwepa kodi n.k
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…