Je, Watoto wanaolelewa bila vipigo hawana maadili?


MkΓ»u Kwa Sisi tuliosoma Saikolojia tunajua fimbo ni hatua ya mwisho Kabisa na ya juu Kabisa Kwa Mzazi kuitumia Kwa Mtoto.
 
Kupigwa tumepigwa sana tukiwa wadogo, hata kwa kosa dogo sana ambalo unaweza kulielewa unadundwa tu
Mkuu kumbuka wazazi wetu ukoroni uliwaathiri sana babu zetu walio tulelea baba zetu na mama zetu.hivyo kupiga waliona ni haki kutoa kipigo kisicho na formula lkn kipigo kiasi nisawa.

sema hizi agenda zinaletwa kimtido badae iwe koswa kumpiga mtoto ukimpigwa unafungwa. haya yatafika muda sio mrefu.
 
MkΓ»u Kwa Sisi tuliosoma Saikolojia tunajua fimbo ni hatua ya mwisho Kabisa na ya juu Kabisa Kwa Mzazi kuitumia Kwa Mtoto.
Ndio nakubaliana nawewe shida iliyopo ni kila kosa fimbo hapo ndo wazazi wanakosea. lakini kukanusha kama ulivyosema wewe tutakuwa na taifa bovu sana.
 
Kwa mujibu wa biblia,(Mithali 29:15;23:13 na Mithali 22:8)kiboko ni muhimu,
cha kuzingatia wazazi unapomrudi mwanao kwa fimbo
fanya hivyo kwa nia njema na siyo udhalilishaji au kumkomoa inaleta kisasi kwa mtendewa.
 
Ni kweli mkuu wengi hawakubali na kusema ooh tunawadekeza hell no
Mtoto kuonywa na kupigwa kidogo ni sawa ila sio mpaka unamchoma moto mikono kisa kadokoa nyama au kaiba mia
Kuna wazazi washenzi mkuu na hao ndio sikubaliani nao kabisa

Unamfunga kamba mtoto masaa na kumfungia chumbani siku nzima
Mkuu kuna ukatili wa watoto we acha tu
Hata humu unaweza kukuta watu wanapiga hivyo
Tuendelee kutoa darasa ili nao wabadilike
Mzazi hata siku moja hutembei barabarani na mwanao bali kuwakunjia uso tu
Akikuomba buku unamtukana
.aisee tunaona mengi sana mitaani
Wengine wanasema wazungu hawapigi sio kweli wakiwa wadogo wanawapiga kwa kuwafundisha ingawa wanajua wanaweza kunyang"anywa watoto
Ila nidhamu ipo
Kina mama kwa afrika ndio wanaongoza kwa ukatili wa watoto sasa sijui kisa mimba za nje ya ndoa sijui
 
Kulea kunataka subrah, maombi plus tabia njema za wazee.
Kuna wazee wanapiga ili kuwafundisha watt wao maadili ambayo hata wao unapowaangalia hayo maadili hawana.
 
Kumnyima mtoto kipigo ni dhambi
Wewe waache tu, eti wanaangalia vitabu vinavyosema na uzungu mwingi. Mtoto anatakiwa kuchanganyiwa radha. Nasaha vikombe vitatu, kipigo kijiko cha chai. Kaa sivyo unavuga shoga
 
Aisee kuna watu wanapiga ht vitoto vichanga.
Wengine wanataka wtt wadogo wa act km watu wazima mtt asifanye utundu hata kdg anachapwa.
Wengine mtt akiwa na ufaham mdogo juu ya jambo fulani, wanachapa na matusi juu.
Mie adhabu ya kuchapa naipinga vikali mno
 
Vyote vinatakiwa balance kwenye malezi. Mimi hapa nitafuata malezi ya wazazi wangu kwa 100%. Nitaorodhesha mambo machache ambayo naona wazazi wangu walipatia mno.

1. Baba na mama walikuwa wanatoa kichapo ila sio kupiga makofi, ngumi au fimbo za kupiga mwili mzima. Ilikuwa haina tofauti na shuleni. Ilikuwa ni fimbo za kawaida sana bila kuleta madhara. Sema mama alikuwa ana utaratibu wa kufinya.

2. Ni wazito mno kutukana. Sikumbuki ni lini baba au mama alishaniita "Mbwa wewe" kama wazazi wengi wanavyofanya. Mimi ukinitukana ni ugomvi mkubwa mno.

3. Pamoja na ukali ila kila siku jioni lazima tule chakula mezani familia nzima kwa maana ya watu wote watakaokuwepo nyumbani siku hiyo. Na baada ya msosi huwa ni neno la Mungu na stori sana. Mzee ni wa mastori balaa. Mtacheka kinoma kama vile sio yeye wakati mwingine anajikataa na kukushushia kipigo.

4. Hawakutulea kama watoto wa geti kali. Miaka ya 93 na 94 nakumbuka baba mwenyewe alikuwa akitupeleka kutazama Sinema usiku. Walituachia kiasi chake tuifahamu dunia. Hata saa nyingine tukitaka kwenda sehemu ruhusa walikuwa wanatupa ila omba sana giza lisikukute nje yaani utajua hujui.

5. Hawakuwa wanatuadhibu tunapofeli mitihani. Walikuwa wanatupa tu ushauri na kutusihi tufanye jitihada. Ila nilikuja kumshtukia dingi alikuwa anapunguzia hasira zake kwa mtu aliyefeli kwenye makosa mengine. Ukiwa umefeli darasani halafu ukajikuta kwenye kosa lingine utakutana na hasira kali sana za baba.

7. Hawakutaka tuwe wafia dini. Kanisani tulikuwa tunaenda bila kukosa ila yale mambo ya mikesha na kempu za vijana hawakuwa wakitaka tujihusishe sana.

8. Mambo ya Tuition hayakuwepo kabisa. Nikiwa O - Level kulikuwa na shughuli maalum kila likizo kutoka kwa mshua mwenyewe. Hadi likizo iishe unarudi shule na sugu za kutosha. Nilivyomaliza form 4 nilipangiwa usimamizi wa kilimo cha vitunguu kuanzia kuandaa shamba hadi kuvuna. Siku tunavuna tayari ilikuwa ishafika tarehe ya kwenda form five.

9. Kwa upande wa watoto wa kiume baba alikuwa anatukazia zaidi. Akikukuta umekaa kizembe lazima akupangie kazi ambayo hata hukuifikiria. Tulikuwa tukimwona yupo maeneo lazima tukae mbali asituone.

10. Mimi huenda nisingemaliza chuo kwa jinsi nilivyokuwa na kiu ya kuwa mjasiriamali. Baba alisimama kidete kuhakikisha napata degree kwanza ndo nianze ishu za biashara. Nakumbuka karibu akosane na rafiki yake aliyekuwa anaona niko sawa kufanya biashara huku nasoma.

11. Kuhusu kuchagua mchumba wazazi huangalia tu tabia za mama wa binti. Kama mama haeleweki huwa ni NOO hata kama demu hana shida.
 
😁😁😁😁😁😁shida ni moja tunaishi kwa mazoea maana unaweza mlea mtoto bila shouting wala viboko na akawa mtoto mwema ila akitoka nje ya imaa anakutana na waliomzungua na wanakua nje ya maadili
so hapo hapo ndipo viboko vimatake place kwa sababu kuna vinimambo ame adapt outside
 
Nunua vitu vya jumla weka ndani acha kumtuma mtoto vitu rejaja dukani mara sukari robo, mara kiberiti kimoja, mara chumvi pakiti moja n.k
 
Kwa mujibu wa biblia,(Mithali 29:15;23:13 na Mithali 22:8)kiboko ni muhimu,
cha kuzingatia wazazi unapomrudi mwanao kwa fimbo
fanya hivyo kwa nia njema na siyo udhalilishaji au kumkomoa inaleta kisasi kwa mtendewa.
Kama mzazi haamini biblia vipi?
 
Nashukuru hapa tuko na mama Dkt. Gwajima D atusaidie kupeleka muswada bungeni wa kufuta sheria ya viboko mashuleni, tena iwe ni kosa la jinai kumpiga viboko mtoto akiwa shule.

Kama hawawezi kufundisha watoto bila kuwararua na viboko ni HERI HIZO SHULE ZIFUNGWE KABISA.

Kuna shule za binafsi nyingi zikiwemo zinazomilikiwa na Mh. Anna Tibaijuka zinaendeshwa bila viboko na zinafanya vizuri tu kimaadili na kitaaluma. Tuige hiyo model, nendeni mkafanye utafiti kujua wamewezaje.

Viboko havijengi maadili, vinajenga NIDHAMU YA WOGA.

Waziri tunaomba mkafute ile sheria ya kikoloni.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…