Je, Watoto wanaolelewa bila vipigo hawana maadili?

Nunua vitu vya jumla weka ndani acha kumtuma mtoto vitu rejaja dukani mara sukari robo, mara kiberiti kimoja, mara chumvi pakiti moja n.k
Mkuu hivyi unadhani ulivyo wewe namimi tunalingana kiuchumi?

Hujui Kuna familia Kila siku hununua mafuta 300 na sabuni ya kufulia na kuogea ndo hiyo hiyo? Kwa comment Yako inaonyesha wazi hujui hata uchumi wa watanzania walio wengi
 
Ninyi mnapinga viboko peleke kwenye shule ambazo hazipigi Watoto. Kwanza Kila siku wanapewa mkate na mayai huko na uji wa blue band pelekeni huko sisi tupeleke kwenye mboko.

Badala ya kushauri apeleke mswaada wa katiba mpya

Kama mnaona mboko hazifai futeni na magereza.
 
Hii hafai kabisa yanaitwa mateso na manyanyaso makubwa Kwa mtoto.

Mbona kiasi yafaa sana
 
Sijawahi kuwapiga watoto wangu kwa sababu nimepigwa sana na ninaona kuna wakati nilikuwa napigwa hata nikitoka kucheza mpira
Hayo walikuwa wanafanya wazazi kudhani kuwa tutakuwa na nidhamu
Ila wengi waliharibika mpaka kuwa nunda, hata mimi nina watoto wakubwa na wengine wamemaliza vyuo ila wananipa heshima ya hali ya juu na upendo juu
Sina mtoto mwizi wala muongo kwa sababu nimewafundisha kama nilivyofundishwa ila bila fimbo

Najua kuna wazazi humu wanaona kupiga ni njia rahisi ya kumnyamazisha mtoto
Jamani hata mbuzi wadogo huwa wanakimbia kimbia wakiwa wadogo
Watoto wakicheza tushukuru Mungu wana afya njema na wanahitaji michezo
Kuna mwanangu alivunja kikombe alishtuka sana nikamwambia kaa mbali na hapo na ni ajali usijali
Sasa ukute mwingine atapigwa siku nzima na hata baadae haombwi msamaha kwa hasira za kijinga
Kikombe tu unamtoa mpaka damu mtoto daa
Wanangu wanalala wakiwa na furaha na lazima nihakikishe hilo
Na wakitoka shule ni kuwapokea kwa heshima bila maswali mengi hujui wamepata nini huko shule na pia wamechoka

Nakuomba uwaelimishe sana wanaopiga badala yake kuwa karibu na kuwafundisha
 
Au labda shoga?
Hii mada ndipo ilipofikia, kuwa shoga sidhani.

Ki ukweli malezi ya watoto ni suala mtambuka. Nakumbuka wakati nakua miaka ya tisini mwanzoni nilikuwa na kampani ya wahuni wahuni tu ambao walikuwa wanawaza HipHop na kutoboa maisha kama Black Americans.

Wengi wa washikaji zangu walizamia mamtoni, wamezamia kama wana 10+ hadi leo haijulikani kama wapo hai au wamekufa.

Wawili tu ndio tunawasiliana, mmoja yupo Ujerumani mwingine yupo Norway. Nilikuwa na kampani ya wahuni pale Upanga kabla ya kuhamia Ilala mwaka 1993.
 
Unazo pesa za kumpeleka mtoto wako shule wanayokula mkate, mayai na uji wa blue band?
 
Mkuu hivyi unadhani ulivyo wewe namimi tunalingana kiuchumi?

Hujui Kuna familia Kila siku hununua mafuta 300 na sabuni ya kufulia na kuogea ndo hiyo hiyo? Kwa comment Yako inaonyesha wazi hujui hata uchumi wa watanzania walio wengi
Boreshini uchumi sasa muache kudunda watoto kwa sababu wamepoteza buku ya sukari.
 
Huko mamtoni unaweza kuta wana maisha mazuri tu ambayo hapa bongo labda wasingekaa wayapate lakini ndio hivyo wameamua kujitenga na wanoko na wengine ambao wangekuwa tegemezi tu kutaka kutumiwa remittance money kila wakati.
 
Bila fimbo Mtoto wa kibongo haendi Ila sio kila kitu unatumia fimbo,muadhibu Kwa mafundisho Mazuri upendo na fimbo Ila kadiria asiwe nunda! Si mnaona watoto wenu mnaowafundisha kizungu wanatukana Hadi watu mtaani! Analelewa kizungu anaishi kiswahili
 
Mkuu kiukweli hao wanatumia maandiko ya Dini wanatumia vibaya maandiko wengi wao:Kwanza maandiko yanasema kweli tuwape watoto kipigo Tena ukiwa huna hasira na si kila kosa ni Lazima kipigo!Hivi sasa vipigo sio kwa ajili ya kumwadabisha mtoto,Bali ni mtu ana stress zake huko, mtoto akikisea hasira zake anammbebesha mtoto.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…