Je, Watoto wanaolelewa bila vipigo hawana maadili?

sio kua mtoto anapigwa kila dakika au kila kosa, kuna kosa unaona kabisa hapa bila kumkanda huyu hatutasikilizana vizuri ili iwe wakat mwnegine akikosea ukimwambia anaelewa, ukimlea mtoto akakosea ukawa unasema tu ntakupiga ntakuchapa utanitambua huyu anakua anajua huna cha kumfanya zaidi ya maneno matupu kiboko sometimes ni kizuri.
Je mkuu Una Elimu sahihi ya malezi (parenting Education) au unatumia mfumo wa kuwa Mimi nilichapwa na Mimi nabidi kuchapa.?

Ni vizuri ukadeal na AKILI ya mtoto na sio mwili wake.
 
Hizo nchi ambazo watoto hawachapwi zina mmonyoko mkubwa wa maadili pia ,sisi tunajiona hatuna maadili ila ukitembelea kwa wenzetu utaona bado sisi tuna maadili sana😁
kabisa, halaf sio kila kosa mtoto anakandwa mimi naongea mwisho mara mbili akirudia the same mistake namkanda kidogo akija kufanya kosa extra large namkanda vizuri sana hata akienda kwa bibi yake unapata pongezi mtoto unamlea vizuri anakusikiliza ukimwambia jambo hajui naleaje.
 
Je mkuu Una Elimu sahihi ya malezi (parenting Education) au unatumia mfumo wa kuwa Mimi nilichapwa na Mimi nabidi kuchapa.?

Ni vizuri ukadeal na AKILI ya mtoto na sio mwili wake.
mimi silei mtoto kama nilivyolelelwa kwa sababu hata mm stiki nilizilamba vizuri sana na kwanamna flani zilinisaidia sasa mm nalea lakini akinikosea kosa naona kabisa anastahili kupigwa nampiga kwa kweli
 
kabisa, halaf sio kila kosa mtoto anakandwa mimi naongea mwisho mara mbili akirudia the same mistake namkanda kidogo akija kufanya kosa extra large namkanda vizuri sana hata akienda kwa bibi yake unapata pongezi mtoto unamlea vizuri anakusikiliza ukimwambia jambo hajui naleaje.
Wenzetu hao tunaowataka kuwaiga , wao wenyewe wanatamani waishi kama sisi , kukuta toto linamwambia mzazi kwamba ni shoga kwa wenzetu ni kawaida sana ,hii mambo sioni kama kwetu ina afya🤔
 
mimi silei mtoto kama nilivyolelelwa kwa sababu hata mm stiki nilizilamba vizuri sana na kwanamna flani zilinisaidia sasa mm nalea lakini akinikosea kosa naona kabisa anastahili kupigwa nampiga kwa kweli

Unawajengea nidhamu ya uwoga watoto wako .

Ikiwa hawawezi kukusikiliza mpaka utumie viboko basi ujue hata wakikusikiliza ni kwakuwa wanaogopa viboko.
 
Wenzetu hao tunaowataka kuwaiga , wao wenyewe wanatamani waishi kama sisi , kukuta toto linamwambia mzazi kwamba ni shoga kwa wenzetu ni kawaida sana ,hii mambo sioni kama kwetu ina afya🤔
kizazi cha sasa watu tunaendeshwa na mfumo wa kisasa, mambo ya kuiga,hivi unamnyimaje mtoto kiboko? ameshaona madhara ya kunyima mtoto kiboko? asilimia kubwa ya watoto wasiopigwa japo sio wote wakiwa wakubwa wengi huwapanda wazazi wao vichwan na ukute mtoto huyo alilelewa na mzazi mmoja tu hilo ndio balaa, lea mtoto kama vile kesho hautakuwepo awese kuishi mazingira yoyote yale.
 
Wenzetu hao tunaowataka kuwaiga , wao wenyewe wanatamani waishi kama sisi , kukuta toto linamwambia mzazi kwamba ni shoga kwa wenzetu ni kawaida sana ,hii mambo sioni kama kwetu ina afya🤔
Hiyo Ajenda ya ushoga mnaitumia Kama defense mechanism Ila mnashindwa kutazama upande chanya wa wenzetu

Hao wenzetu wefanikiwa kuzalisha watoto bora ambao wapo productive tangia wakiwa wadogo hauwezi ukalinganisha na sisi

Ila nyie kila mada mnakimbilia muchomekea Ajenda ya Ushoga
 
Unawajengea nidhamu ya uwoga watoto wako .

Ikiwa hawawezi kukusikiliza mpaka utumie viboko basi ujue hata wakikusikiliza ni kwakuwa wanaogopa viboko.
tupo jamii ya changanyikeni, asilimia kubwa ya watoto wasiopigwa kwao ndio watovu wa nidham hasa wakiwa wanacheza pamoja na wenzao wanaokandwa na unaiona tofauti
 
Hiyo Ajenda ya ushoga mnaitumia Kama defense mechanism Ila mnashindwa kutazama upande chanya wa wenzetu

Hao wenzetu wefanikiwa kuzalisha watoto bora ambao wapo productive tangia wakiwa wadogo hauwezi ukalinganisha na sisi

Ila nyie kila mada mnakimbilia muchomekea Ajenda ya Ushoga
No mkuu nmetolea mfano tu , mmonyoko wa maadili ni mkubwa sana kwa wenzetu tofauti kabisa na kwetu , pia hata wao wanapenda sana jinsi sisi tulivyo naongea kitu ninachokijua na sio nilichosikia mkuu .
 
Waafrica na wazungu

Kuhusu maadili hatuwafikii

Ebu tazama tu viongozi wetu wanaiba mpaka unaogopa sasa unajiuliza maadili ya MTU mweusi ni yapi hayo

Sisi ni wahuni Sana hatuna maadili yoyote

Tumebaki kusema kuwa hatufanyi ushoga basi hayo ndo maadili
 
😁😁😁😁😁Sisi umaskini tu ndio unatusumbua.

Njaa huwa ina tabia ya kuja na maelekezo mkuu😁😁😁😁
 
Inategemea na aina ya mtoto. Nina watoto wawili, wa kwanza sikumlea kwa fimbo maana hakuwa anakupa sababu ya kumchapa. Nilimchapa mara moja tu au mbili kama sikosei. Yupo vizuri anajiendesha mwenyewe bila kuendeshwa, anajua nini anafanya.
Huyu mwingine jamani ee mungu nisaidie.
 
Back
Top Bottom