Je, Watu waliokufa wana nguvu kuliko walio hai?

Je, Watu waliokufa wana nguvu kuliko walio hai?

Kujifungia kwenye box la ukosefu wa maarifa sio kosa lako.
Huo ujinga kwenu ndio maarifa?!!
Aisee!!
Kweli tunatofautiana. Endeleeni kuyasubiri hayo maisha ya baada ya kufa.

Duh.
 
Kwa mujibu wa Biblia na Quran tukufu.
Hakuna connection Kati ya waliohai na waliokufa, isipokuwa ni michezo ya shetani kupitia mizimu Ili apate kuwapotosha watu.
Kinachokufa ni mwili na sio roho na nafsi. Mwili uoza kaburini, nafsi na roho urudi KWA Muumba kusubiria hukumu.
Ooh
 
Kwa kifupi tuanze kujadili dhana ya kifo ninayoiamini "Kifo ni kuondoka taratibu kutoka Sasa Hadi zamani. Yani kutoka kuto kuwepo na kuwepo(kuzaliwa) kutoka kuwepo na kutokuwepo Tena(kufa).
Madondoo ya miongozo ninayoiamini

-Kufa ni namna nyingine ya kuishi ya binadamu
- Mtu hafi akapotea (MTU mwema hafi akapotea mpaka pale watu watakapoacha kumkumbuka.

Je nikweli MTU akifa anakuwa na nguvu uhai kubwa kuliko mtu aliye hai.
Kwa mujibu wa FALSAFA za kiafrika nguvu uhai ipo katika mioangilio huu
MUNGU
|
WAHENGA
|
MIZIMU
|
WAGANGA
|
BINADAMU

Kama mpangilio huu upo sahihi Basi watu waliokufa wanaweza kuwa na nguvu zaidi kwakuwa wapo karibu na mwenye mamlaka mweza wa yote "MUNGU"

MAMBO YA KUYATAZAMA

1. Kwa waafrika sio ajabu kusikia watu wakiomba misaada kwa mababu wao wa zamani ambao walikwisha Kufa

2. Watu walio hai wanaogopa Sana watu walio kufa Mizimu na wahenga na watu hudhani kuwa watu waliokufa huweza kuwadhuru watu walio hai hasa Kama wakiacha laana na n.k

3. Baadhi ya dini huwaomba watu waliokufa zamani wanaosadikika kuwa na matendo mema ambao huitwa watakatifu ili wawaombee kwa Nguvu uhai kubwa kuliko zote ambayo ni Mungu

Bada ya hayo je Watu waliokufa wanayo Nguvu uhai kubwa kuliko watu walio hai?
Ni mizimu ama uchawi ndo wenye nguvu ila si Mareham
 
Nauliza sijibiwi, wakati yesu anaomba milimani kipindi fulani alitokewa na watu watu watatu, Mussa, Elia, na mwingine nimemsahau wale walikuwa nani.Na kama yeye alikufa akafufuka alifufuka kama nani?Tafadhali mkuu mkumbushe anijibu.
 
Kwa tafsiri ya kanisa, Shetani ni nini?pepo shetani na mzimu ni vitu vitatu vyenye tafsiri zinazojitegemea.
Shetani ni mwakilishi mkuu wa mambo yoote ya giza, pepo ni watumishi wake (wavurugaji), mizimu ni aina za majini yanayosimamia taratibu za koo,familia flani.
 
Shetani ni mwakilishi mkuu wa mambo yoote ya giza, pepo ni watumishi wake (wavurugaji), mizimu ni aina za majini yanayosimamia taratibu za koo,familia flani.
mkifahamu shetani hasa ni nini hamtapoteza muda kukemea vitu vilivyawazunguka na kuacha kupambana na nadharia za kufikirika.
 
mkifahamu shetani hasa ni nini hamtapoteza muda kukemea vitu vilivyawazunguka na kuacha kupambana na nadharia za kufikirika.
Ukimfahamu aliyekuweka gundu usipate ajira ungeachana na nadharia zinazokutesa
 
Back
Top Bottom