Je, Waziri wa Utawala Bora, Mohamed Mchengerwa ni mkwe wa Rais Samia?

Hehehehe
 

Hata ingekuwa ni Hawara yake ( kwa Mfano ) kama Kiutendaji ni Mtu angemteua wala nisingehoji kwani naangalia Kazi na si mengineyo. Huwezi Kumfurahisha kila Mswahili ( Mtanzania ) hasa ukiwa ni Rais ( Kiongozi ) nchini Tanzania.

Mlivyo Wanafiki mbona hamhoji Marais wenu waliopita ambao kuanzia Hayati Baba wa Taifa Mwalimu Nyerere, Mwinyi, Mkapa na Kikwete nao pia hawakuteua tu Wakwe zao bali walienda mbali zaidi na Kuteua Ndugu zao, Watoto wao wa Nje, Mashemeji na hasa hasa Mahawara zao wengi tu?

Tuhoji tu Mambo yenye Tija Kiutendaji.
 
Mimi huwa na jiuliza swali hili siku hizi. Zamani na mimi nilighafilika niliposikia matendo ya watoto wa Sadam Hussein kwa mfano.

Swali lenyewe ni hili, "Mbona hatuulizi watoto wa walimu, wafanyabiashara, Madaktari nk nk. Wanapofata nyayo za Wazazi wao. Kwa nini Watoto wa wanasiasa tu ndio iwe nongwa?

Tusione shida yeyote kama ni mtoto wa Mwanasiasa na ni mtu wa maadili, haki na kweli acha afuate nyayo za mzazi wake. Tusiwe watu wa dabali standadi.

Jambo la muhimu wasiwe wakina Uday Saddam ama wauza nganda, hilo tu.
 
Kwa hiyo jamaa anaenda kumlinda mama mkwe pale...pelekeni pua zenu sasa muone atakavyowatoa ufung'unyura.
Haahaa bado mawifi watakuja.Hii tabia ya viongozi wetu kutumia mamlaka kwa maslahi binafsi inaudhi Sana.Je akivurunda atamkanyaje? Hapana
 
Haahaa kwa hyo hiyo nafasi alisubiriwa mama mkwe awe rais ndipo apewe? Haahaa
 
Kama ana uwezo wa kutumikia majukumu yake vyema tumuache atutumikie tu
 
Haahaa kwa hyo hiyo nafasi alisubiriwa mama mkwe awe rais ndipo apewe? Haahaa

Nafasi hiyo inataka mtu unaye muamini pia. Mkwe ana aminiwa na Mama Mkwe sioni tatizo. Vilevile tumeambiwa nafasi yake kabla ya kuteuliwa hivyo ni mtu mwenye uwezo.

Tatizo ni pale kama jamaa akikutana na changamoto za kazi akaenda kutolea hasira kwa mkewe labda.
 
Haahaa kwa kweli uzalendo uliondoka na nyerere, hapo Kuna conflict of interest.Kiuadilifu hapo ni zero.Kiapo Cha rais kinakataa hayo madudu
 
Haahaa kwa kweli uzalendo uliondoka na nyerere, hapo Kuna conflict of interest.Kiuadilifu hapo ni zero.Kiapo Cha rais kinakataa hayo madudu

Kigezo cha kuwa mkwe hakiwezi kufunika hizo sifa nyingine alizo nazo labda utoe ushahidi wa kuonesha safari nzima ya utumishi wake na usomi ilikuwa ni ya mbereko.
 
Mbona hii ipo hata majuu?Donald Trump alimteua Jared Kushner,mkwe wake kuwa''Senior Advisor To The President Of The United States''
 
Sioni tatizo kama Ana uwezo. Ni mtanzania Ana haki ya kuwatumikia wananchi.
 
Sasa mnataka ndugu wa rais wao wasipate kazi sababu ni ndugu wa rais?

Kikubwa utendaji tuu
 
Nepotism-the practice among those with power or influence of favouring relatives or friends especially by giving them jobs.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…