Je, wazungu sio wakazi asilia wa hii dunia?

hamu alimkosea Baba yake Nuhu. hamu alizaa Kushi ambae Ni Nubi,Misri,puti na kanaani. Nuhu alimlaani kanaani hakumlaani kushi au hamu.Kushi ipo Kati ya Ethiopia na Sudan kama sijajosea
 
Apana labda kule kwenye prymid za giza
 

Mzungu ni nani na katokea wapi? je kipindi ambacho yesu anazaliwa huko mashariki ya kati wale akina kaisari amabao walikua ni watawala wa ufalme wa kirumi walikua watu gani kama sio wazungu? swala la kuwapondea ni wivu wetu tu sisi watu weusi na hali ya kukosa ubunifu na akili za kukabiliana nao..... ikumbukwe kua hata hizo dini mnazojifichia akazileta huyohuyo mzungu na ndio aliowafundisha ustaarabu pamoja na kuuleta ukoloni na badae kusaidia harakati za mapambano dhidi ya biashara ya utumwa na baadae ukoloni...

kama kweli mtoa mada unadai sisi ni watu wa mungu iweje hao tunaowasema vibaya wapendelewe kua na maendeleo pamoja na utajiri uliotukuka?
hayo ni maneno tu ya mfa maji....walishatutangulia kutokana na matumizi yao sahihi ya akili zao.....
na huyu Mungu mnaemuongelea pengine sio mungu mkuu na ndio maana wao wazungu kama wana mungu wao amekua anawasaidia sana na mambo yao yanakwenda vizuri.
 
Bw. Mshana Jr asante kwa mada tajwa, naomba kupingana nawe.

Maelezo yako si tu kwamba hayana ushahidi wala mashiko (kisayansi au kihistoria) lakini pia ni potofu.

Naanza kuona madhara ya mythology na spirit-ism. Katika hali ya kawaida na kwa hadhi yako hapa JF, dhana yako ya Wazungu ni wavamizi "aliens" imejengwa kwenye imani ya mambo ya hadithi za kimizimu lakini ktk akili ya kawaida na uhalisia ni hoja mfu kabisa.

Historia inaonyesha na kuthibitisha kuwa binadam wa kale (Adam-Nuhu) waliishi kwenye dunia ya wakati huo. Historia inaonyesha baada ya Gharika ya Nuhu, jinsi jamii, watu na mataifa ya ulimwengu (uliofuata baada ya Gharika) walivyoishi na kutawanyika. Historia imejaa ushahidi na taarifa za makabila, lugha na tamaduni za mataifa ya ulimwengu wakiwemo Wazungu. Sayansi pia inaonyesha Mzungu ni binadamu kama Mwafrika, Mu-Asia, Mlatino yeyote kwa 100%. Suala la rangi yao (ukizingatia wana tofautiana hata wao kwa wao) halina mashiko kwa vigezo vyako hapo juu.

Kwa vile Mzungu ni binadam (wa kawaida) ndio maana anahusika na madhara na uharibufu katika dunia hii na sio ktk sayari nyingine. Unataka kuniambia matatizo tuliyo nayo leo ni Tanzania ni mkono wa Mzungu tu? Ni upi mchango wa jamii nyingine kama Waafrika, Waasia nk kwenye matatizo yetu?

Hebu nikuulize yafuatayo:-

1) Mzungu amemzidi nini (kimaumbile, kiumuundo) Mwafrika au Mlatino au Mu-Asia?

2) Hao Wazungu "aliens", wana mfumo gani hasa wa maisha?

3) Je wanazaa, wanaugua na kufa?
 

 

Sijui una maana gani kuweka pamoja mchango wangu na wa BL.

Lakini nisisitize tu, you're planting a bad & evil seed which once brought to harvest.....breath... the havoc will be unimaginable.

Unaweza kuona jinsi kuna watu wamemeza kichwa kichwa maneno yako bila hata kujiuliza. Wengi wao ni kwa kusukumwa na hisia (hatred, prejudice) na ignorance. Lakini wewe unayewa expose kwa kuwalisha "sumu" you will not remain innocent.
 

Mkuu wala usihofu nadhani bwana mshana anaeleza matokeo ya fikra zake sasa ni wajibu wetu kumuuliza na kuutafuta ukweli ambae utapatikana kwa kupitia maswali na majibu ila ninachokiona hapa mtoa hana majibu ya maswali mengi ambayo yanatokana mada yake.
 
Am sorry kwa hilo lakini nilitaka kujibu kwa pamoja ila reply yangu haikuonekana
Nimeweka hii mada kama hoja jadilika na ili iweze kuleta ushawishi ni lazima niwe na upande (mtazamo wangu unaweza kuwa na pingamizi nyingi) lakini mwisho wa siku ni kujifunza na kupanua ufahamu

Sipendi kuwa rigid kwenye mjadala labda tu iwe ni kwa jambo linalonihusu direct lakini si kama kwenye dhana kama hizi ambazo ndani yake kuna mengi yakudadavua
 
Mmh usitoe hukumu kwa haraka kiasi hicho mjadala bado uko hai usihofu
 
Hivi, huwa wanapata Mrejesho gani...!! pale wanapo jaribu kupima au kuchukua vipimo vya DNA (vinasaba) kwa viumbe wa kale (hii inaweza kuwa ni Siri) ili kujua chimbuko na asili MZUNGU alipotokea..!

Kwa sababu, kama anavyo sema Mshana Jr, hakuna vitabu vya Dini, wala vile vya Wanazuoni wa kale, vinavyo mzungumzia Mzungu na Asili ya kule alipotokea..

Yapo mengi (Mzungu) anayojaribu kwa juhudi kubwa, kuyafunika ama kuyapoteza, kwa nia ya KUFICHA alipo tokea.
 

Asante Mshana Jr, sasa kama ulikusudia kuleta mjadala fikirishi (yaani wewe usiwe mjibuji) basi nafikiri ungeuleta kivingine kidogo.

Samahani kwa kusema hivi, lakini ukitazama wachangiaji wa mwanzo kwa sehemu kubwa walichukua kama facts na kumeza tu.
 

Kabla ya kukujibu naomba kukuuliza, je wewe mpaka sasa umesoma au kupekua vitabu gani mpaka ukapata majibu uliyoondika hapa?

Nauliza kwa nia nzuri ya wazi hivyo uwe huru kueleza
 
Naona mambo ya NATURAL SELECTION
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…