Nimekuelewa mkuu, kwa maelezo yako hapo juu inaonyesha tumbo lililozaa ndio miliki ya mtoto. Je kwa uelewa wako kati ya baba na mama nani mmiliki halali wa mtoto? Nipe facts za kimaandiko na kisayansi pia kama utaweza
Don't jali mkuu, hapa hatuko kubishana wala kuonyesha nani anajua zaidi ya mwenzake. Tupo kufunzana na kuelekezana, we andika vile kadri ya ulivyofunuliwa/maarifa yako. Nipo hapa kujifunza toka kwako pia
Kwa uelewa wangu ,mi naona wote wawili ni wamiliki halali!
Nimekuelewa mkuu, kwa maelezo yako hapo juu inaonyesha tumbo lililozaa ndio miliki ya mtoto. Je kwa uelewa wako kati ya baba na mama nani mmiliki halali wa mtoto? Nipe facts za kimaandiko na kisayansi pia kama utaweza
Don't jali mkuu, hapa hatuko kubishana wala kuonyesha nani anajua zaidi ya mwenzake. Tupo kufunzana na kuelekezana, we andika vile kadri ya ulivyofunuliwa/maarifa yako. Nipo hapa kujifunza toka kwako pia
Yaani nawaza namna ya kupost hili gazeti,ila utamisamehe tu ,we najua utalisoma tu...
Kibiblia
Biblia haijawahi kabisa kuainisha umiliki wa watoto kwa wazazi kwamba watoto ni miliki ya nani na kama iliwahi basi ni kisheria si ki Mungu yaani kwa Mungu hakuna umilikishaji wa mtoto kwa mzazi mmoja... Hiyo ni kwasababu
1. Mungu hajawahi taka mke na mume kuachana hivyo anachojua yeye kwamba ninyi si wawili ila ni mmoja yaani kwa Mungu anajua swala la mke na mume na hao ni mmoja si wawili hivyo watoto hapo si wawili ila ni wammoja ambaye ndiye ninyi.... Mungu hajawahi anzisha habari za mzazi mwenza au singo mama/baba sijui n.k hapo itahusika sheria si Mungu....
2. Mungu hajawahi kuumba mfumo wa mmoja kuzaa pekee bila kumtegemea mwenzake... Yaani ili mtoto azaliwe inawategemea wote wawili mbegu si mtoto ni mbegu tu wala yai si mtoto ni yai tu ila ukiviweka pamoja ndio mtoto anatengenezwa hivyo wote wawili kwa umoja wenu mna haki (si umiliki) juu ya mtoto...
3. Ki Mungu unaposema mtoto unamaanisha ni ile roho na sio mwili maana mtu ni roho kwa hiyo hapo utagundua kuwa hakuna mzazi anaye lweza kuwa na umiliki wa roho hapo tunasema mtoto kwasababu ni mtu na mtu ni roho basi mmiliki wa huyo ni Mungu hakuna mtu awezaye kumiliki mtu ila wazazi wamepewa dhamana tu ya kuhudumia mwili ambao mwili huo umetengenezwa ki bailojia kwa nguvu za asili tu alizoweka Mungu mwenyewe....
Ki sayansi utagundua kuwa umiliki wa mtoto ni kupitia DNA na baba na mama na mtoto wote wa DNA zinazofanana hivyo wote ni wamiliki ila kwenye nani amiliki pekeyake hapo itakuja sheria sasa.
Nyakati za Biblia lazima tu kulikuwa na sheria ambazo si za kimungu ni za utawala/serikali zilizoweka mgawanyo wa umiliki wa watoto ikiwa baba na mama wameachana ingawa zinaweza zikawa hazijaandikwa...
Ila kwasasa hatuwezi kuzitumia sheria hizo kwakuwa hazikuwa za Mungu na kwasababu pia kwasasa tupo kwenye serikali ambayo nayo ina sheria zake juu ya umiliki wa watoto ikiwa mmeachana...
Ukitaka kwenda Kimungu juu ya umiliki wa mtoto baki hapa na ujue hili kwamba....
WEWE NA MKEO/MUMEO NI MMOJA NA KWAPAMOJA KAMA MMOJA MMEPEWA DHAMANA NA MUNGU YA KUMTUNZA TU NA MSIACHANE NA IKITOKEA MMEACHANA MJUE MMEMUUDHI MUNGU ILA MTOTO MMEPEWA JUKUMU LA KUMTUNZA WOTE KWA UMOJA....