Je, wewe ni "Mungu"?

Je, wewe ni "Mungu"?

Girland

JF-Expert Member
Joined
Jan 24, 2016
Posts
2,489
Reaction score
4,253
MOJAWAPO ya maswali magumu, ambayo mwanadamu amekuwa akitafuta majibu ni MIMI NI NANI, JE MUNGU NI NANI, n. k

Tumesikia pia, nchini Tanzania mwanamama anayejiita "Mfalme Zumaridi " akijiita "mungu "!.Viongozi wa dini mbalimbali wamejitokeza kumpinga na kusema kuwa anakufuru kujiita "mungu ".Je nani yuko sahihi?

MUNGU AMEAGIZA TUSIABUDU MIUNGU MINGINE, katika amri kumi alizopewa Musa, Mungu alimuelekeza kuwa utamuabudu BWANA Mungu wako Pekee na usiabudu "miungu" wengine.

Hapa kuna jambo la kujiuliza:

1)Mungu anatuthibitishia uwepo wa "miungu wengine " na anatukataza "kuiabudu "?
Je miungu hii ni ipi??

2)Mheshimiwa Kabudi aliwahi "kuteleza ulimi " na kumuita Mwendazake "Mheshimiwa mungu " je huko ndio kuabudu miungu mingine?

BIBLIA INASEMAJE Katika Zaburi 82:1 tunaambiwa "MUNGU asimama Kati ya kusanyiko la miungu anahukumu "
GOD standeth in the congregation of the mighty he judgeth among gods " .Miungu hii inayozungumziwa ni ipi?

Katika Zaburi 82:6 Inasema "Ndinyi miungu, na wana wa aliye juu!

Je, hii haitufanyi kuwa "miungu "?

MTOTO WA NYOKA NI NYOKA!
kama mwanadamu ameumbwa kwa sura na mfano wa Mungu je, hii haimfanyi kuwa "mungu"!

WAJUVI KARIBUNI MTUSAIDIE
 
Allan Watts n Andrew Hubberman, Beau Lotto, N'Tesla...... We are Gods.
 
Unatamani cheo halafu huwezi hata badili jiwe kuwa mkate, sifa ya Mungu ni miujiza we unayo?
Mungu anaishi milele je hutakufa?
Mungu hapangiwi je wewe hupangiwi?

RUDISHA SIMU YA SHEMEJI KAKOJOE ULALE
Huyo aliyeweza kubadili jiwe kuwa mkate ni nani ? Lete ushahidi
 
Biblia imetuita hivyo mkuu?
 
Sema yeye Mwenyezi Mungu ni wa pekee

Mwenyezi Mungu mkusudiwa

Hakuzaa wala hakuzaliwa

Na wala hana anaye fanana nae hata mmoja

(Suratul ikhalas)

Karibu katika uislamu dini ya haki
 
Sema yeye Mwenyezi Mungu ni wa pekee
Mwenyezi Mungu mkusudiwa
Hakuzaa wala hakuzaliwa
Na wala hana anaye fanana nae hata mmoja
(Suratul ikhalas...)
Karibu katika uislamu dini ya haki
Kwenye Bible Mungu alimuumba mtu kwa sura na mfano wake!
 
Unatamani cheo halafu huwezi hata badili jiwe kuwa mkate, sifa ya Mungu ni miujiza we unayo?
Mungu anaishi milele je hutakufa?
Mungu hapangiwi je wewe hupangiwi?

RUDISHA SIMU YA SHEMEJI KAKOJOE ULALE

Nani anayeweza badili jiwe kuwa mkate?
 
kila mwanadamu ana uungu ndani yake

ile pumzi aliyompulizia mwanadamu ni pumzi ya Mungu Mwenyezi

Ila sisi hatujitambui kutwa kucha kwa waganga wakati uwezo tushapewa tunao wenyewe

Kutwa kucha kubadilisha dini eti uombewe na nabii wa Mungu

Wakati sisi wenyewe tuna connection ya kuongea na Mungu Mwenyezi

Kumbuka Yesu alisemaje kuhusu kumuomba Mungu Mwenyezi

Hakusema kwenda kanisani/sinagogi ni lazima bali alisema INGIA NDANI KWAKO UOMBE HIVI

Sala ya Baba yetu aliye mbinguni hiyo ndio sala kubwa mno ukiwa na imani Mungu anajibu aisee
 
Hauwezi kupata udhibitisho wowote wa uwepo wake Mungu njee yako .
 
Unatamani cheo halafu huwezi hata badili jiwe kuwa mkate, sifa ya Mungu ni miujiza we unayo?
Mungu anaishi milele je hutakufa?
Mungu hapangiwi je wewe hupangiwi?

RUDISHA SIMU YA SHEMEJI KAKOJOE ULALE
Hapa naweza nikakubishia, lete hilo hiwe lako hapa halafu huyo Mungu wako alibadili kuwa mkate mbele yetu na sio stori tu abunuwasi katika sheria za asili hakuna jiwe kuwa mkate iwe na Mungi wala nani zaidi ya stori.

Mungu anaishi milelw ni kweli hata binadamu anaishi milelel kinachokufa ni mwili tu (kasha) but roho haifi milele, Mungu hapangiwi wapi?

Na mimi napangiwa wapi ,mbona hapa nilipo sijapangiwa na mtu
 
Biblia imetuita hivyo mkuu?
Mwanadamu ni mungu lakini ni mpaka akipata full potentials zake zote...namaanisha akiweza kufungua senses zake zote...hadi za higher dimensions.

Wale miungu wengine wamezifungua hizo higher dimensions lakini kwa njia zisizo za Mungu (negative forces), na ndio maana watahukumiwa.
 
Back
Top Bottom