Kwa bahati mbaya tuna katiba ya zamani ambayo imepitwa na wakati na ndio maana kila kitu ni kubahatisha tu. Mara utasikia watu wanasema tunahitaji kiongozi mwenye kufanya maamuzi magumu utadhani nchi imetoka vitani! Nchi hii tuliopewa na Mungu ni nzuri sana kwani hata watu wake ni wastaarabu na wanaheshimu misingi muhimu ya amani lakini wanaangamia kwa umaskini.
Nchi iliyojaa kila kitu (ardhi, bahari, mito, maziwa makubwa, misitu, mbuga za wanyama, milima mirefu) ila bado watu wake ni maskini wa kutupwa kwa sababu ya kukosa uongozi thabiti (wenye kutengeneza na kuheshimu mifumo) tumeng'ang'ania kuona watu (viongozi) wenye nguvu kuliko nchi yenye nguvu!
Mungu ibariki Tanzania, Mungu ibariki Afrika.
Landson Tz