Je, zawadi za pesa kwa magoli zinakiuka kanuni za CAF?

SAYVILLE

JF-Expert Member
Joined
Mar 25, 2010
Posts
7,895
Reaction score
12,975
Leo kuna jambo nilikuwa nafuatilia na katika kupekuapekua huko mitandaoni, nikawa napitia kanuni na sheria za mashindano ya CAF nikakutana na kitu kilichonifanya nijiulize maswali kuhusiana na zawadi za magoli za Muheshimiwa Rais Samia Hassan.

Katika document ya CAF inayoitwa "Regulations of the CAF Champions League", document hii inatoa miongozo mbalimbali ya jinsi mashindano yake ya Ligi ya Mabingwa yatakavyoendeshwa ndani na nje ya uwanja.

Katika Article 1 ya document hii inaelezea taratibu za utoaji zawadi kwa wachezaji na timu zinazoshiriki. Kifungu cha 6 katika Article hii kinasema:

Any person, physical or moral, who wishes to present a prize or an award to players or teams on the occasion of CAF competitions, must formulate a request to CAF at least 15 days before the date of the competition. The agreement of CAF in this respect is a pre-requisite to any prize presentation.

The players and teams of Member Associations taking part in CAF competitions cannot, under any circumstances, receive prizes or awards without the authorization of CAF, except those presented by their clubs or associations.

Ningependa kupata ufafanuzi kama hiki kifungu kinahusu hatua zote za mashindano na pia kama motisha aliyotoa Rais Samia inahusika katika kanuni hii.

Kama majibu ya maswahi haya ni ndiyo, ningependa kujua kama hatua stahiki zilifuatwa kwa mujibu wa sheria za CAF.

Muhimu: Mada hii ni kwa ajili ya kuelimishana na kupata ufafanuzi ili kuongeza uelewa wa mambo yanayohusiana na soka. Hakuna nia nyingine yoyote.
 
Attachments

Hata kidogo! Hii motisha haiusiani na hizi Sheria..Rais hausiani na CAF..
 
Authorization ipo hapa kwenye hii exception

"Except those presented by their clubs or associations"
Lakini hizi zinazotolewa za magoli ni wazi siyo za kutoka kwenye klabu wala TFF.
 
Mi najua hilo neno association halikusudii shirikisho la soka peke yake, ni neno ambalo lina wigo mpana ambayo inatoa ruhusa kwa raisi kuweka zawadi kwa vilabu vyetu
Associations wanaitumia kumaanisha vyama vya soka.

Na mtu kama Rais au cheo chake amejumuishwa katika maneno ya mwanzo "Any person, physical or moral, who wishes to present a prize..."

Hayo ni maoni yangu lakini.
 
Leo kuna jambo nilikuwa nafuatilia na katika kupekuapekua huko mitandaoni, nikawa napitia kanuni na sheria za mashindano ya CAF nikakutana na kitu kilichonifanya nijiulize maswali kuhusiana na zawadi za magoli za Muheshimiwa Rais Samia Hassan.

Katika document ya CAF inayoitwa "Regulations of the CAF Champions League", document hii inatoa miongozo mbalimbali ya jinsi mashindano yake ya Ligi ya Mabingwa yatakavyoendeshwa ndani na nje ya uwanja.

Katika Article 1 ya document hii inaelezea taratibu za utoaji zawadi kwa wachezaji na timu zinazoshiriki. Kifungu cha 6 katika Article hii kinasema:

Any person, physical or moral, who wishes to present a prize or an award to players or teams on the occasion of CAF competitions, must formulate a request to CAF at least 15 days before the date of the competition. The agreement of CAF in this respect is a pre-requisite to any prize presentation.

The players and teams of Member Associations taking part in CAF competitions cannot, under any circumstances, receive prizes or awards without the authorization of CAF, except those presented by their clubs or associations.

Ningependa kupata ufafanuzi kama hiki kifungu kinahusu hatua zote za mashindano na pia kama motisha aliyotoa Rais Samia inahusika katika kanuni hii.

Kama majibu ya maswahi haya ni ndiyo, ningependa kujua kama hatua stahiki zilifuatwa kwa mujibu wa sheria za CAF.

Muhimu: Mada hii ni kwa ajili ya kuelimishana na kupata ufafanuzi ili kuongeza uelewa wa mambo yanayohusiana na soka. Hakuna nia nyingine yoyote.
Kuna ukweli hapa
 
Associations wanaitumia kumaanisha vyama vya soka.

Na mtu kama Rais au cheo chake amejumuishwa katika maneno ya mwanzo "Any person, physical or moral, who wishes to present a prize..."

Hayo ni maoni yangu lakini.
Nimerudi kusoma upya tena nimebaini hapo kinachozungumziwa ni zawadi ya mshindi wa mwisho na sio katikati ya mashindano kwenye ahadi ya kutoa hela kama hamasa timu ifanye vizuri.

Na ndio maana ukisoma hapo juu kifungu namba 5 wameweka mchanganuo kuwa mshindi anapokea medali ya dhahabu na mshindi wa pili anapokea medali ya silver

Halafu sasa kwenye huo ufafanuzi wa hiyo medali ndio kuna hiyo sheria ambayo inakataza mtu mwingine kutoa hiyo medali isipokuwa CAF wenyewe au kwa kibali maalumu
 
Ninavyojua mimi kwenye mambo ya sheria, ingekuwa hivyo vifungu vinaingiliana au kimoja kinatoa ufafanuzi zaidi kuhusu kifungu kingine, kifungu cha 6 kingekuwa ndani ya cha 5, kama vile 5.1 (nadhani kwenye Katiba wanatumia lugha kama IBARA) ila lugha iliyotumika na mpangilio wa hivi vifungu ni kama vifungu hivi vinavyojitegemea.

Wataalamu wa sheria waje watusaidie.
 
Back
Top Bottom