Sasa mbona kama umeongea kinyume chake sehemu ambayo yanga anafika akiwa na kikosi bora simba ana uwezo wa kufika akiwa na kikosi kibovu, refer msimu jana simba ilikuwa na kikosi kibovu ambacho karibu kila shabiki alikikatia tamaa, lakini bado wakafika robo kama ninyi tu mliodai mna kikosi bora na mkaishia robo
Na msimu juzi mlifika fainali cafcc kwa fluke tu maana robo na nusu mlipangiwa vibonde kina rivers na marumo ambao walikuwa wanaelekea kushuka daraja, ila mlipofika fainali mkakutana na wenye kombe lao usm alger ndio uwezo wenu ukaishia hapo, na mlikuwa na kikosi bora mna striker kama mayele ila bado mkashindwa kuchukua kombe lile mmebaki kujisifia medali tu
Sasa mngekutana na zamalek na berkane wenye michuano yao kwenye hatua ya robo sidhani hata kama nusu mngefika, sasa jiulize kama mna kikosi mnachosifia kuwa ni bora na hamna kombe lolote la kimataifa siku mkiwa na kikosi kibovu kama cha simba je itakuwaje, simba na kikosi chao kibovu wameenda robo cafcl mara tano mfululizo wamevuna pesa nyingi na points zilizo wapandisha rank huko kimataifa katika list ya timu bora africa wamewaacha mbali sana