Jela miaka 30 kwa kuzini na Mwanae wa kumzaa

Jela miaka 30 kwa kuzini na Mwanae wa kumzaa

Girl in the basement

Ni stori ya kweli
Hii?
1743052969454.jpg
 
Mahakama ya Wilaya ya Temeke Jijini Dar es salaam imemhukumu ALLY SELEMANI IDDI kifungo cha miaka 30 jela baada ya kupatikana na hatia ya kosa la Kuzini na Maharimu (mtoto wake )

Hukumu hiyo imetolewa tarehe 25 Machi, 2025 na Hakimu Mkuu wa Mahakama ya Wilaya ya Temeke Mhe. Janeth Kaluyenda baada ya kuridhika na ushahidi uliotolewa kutoka upande wa Jamhuri.

Katika kesi hiyo ya Jinai namba 273/2023 Mtuhumiwa ambaye ni mkazi wa Wilaya ya Temeke Jijini Dar es salaam alikuwa anakabiliwa na shtaka la kuzini na maharimu kinyume na kifungu cha 158(1),(a)cha Sheria ya kanuni ya adhabu,(Sura ya 16 kama ilivyorejewa mwaka 2022).

Mshtakiwa alitenda kosa hilo katika mwaka 2022 na 2023 mwezi Agosti katika eneo la Mbagala Mianzini, wilaya ya Temeke ,Dar es salaam ambapo inaidaiwa alimwingilia kimwili mwanawe wa kumzaa na kumpa ujauzito kisha alimpa dawa za kutoa mimba.

Sio kila mwili umebeba roho ya binadamu; miili mingine imebeba mizimu na mashetani
 
Hii iinahhusishwa na nini? Ushirikina au kiu
Ushirikina mnausingizia....haya mambo huanza na mazoea ya kijinga baina ya Baba na mtoto.... mazoea haya huondoa adabu, heshima na stara baina yao.......

Mtoto hatambui uwepo wa baba yake katika misingi ya ubaba bali 'ushikaji'

Na kama mtoto anakuwa hana adabu ya mavazi ndio mambo yanakuwa rahisi zaidi......

Kwa kawaida mwanadamu anaporuhusu tamaa za kimwili zimtawale fahamu huwa zinakaa pembeni na hurejea pale unapokuwa umeshamaliza kusudio la tamaa zako na hapo ndipo huzaliwa majuto....
 
Back
Top Bottom