Mahakama ya Wilaya ya Temeke Jijini Dar es salaam imemhukumu ALLY SELEMANI IDDI kifungo cha miaka 30 jela baada ya kupatikana na hatia ya kosa la Kuzini na Maharimu (mtoto wake )
Hukumu hiyo imetolewa tarehe 25 Machi, 2025 na Hakimu Mkuu wa Mahakama ya Wilaya ya Temeke Mhe. Janeth Kaluyenda baada ya kuridhika na ushahidi uliotolewa kutoka upande wa Jamhuri.
Katika kesi hiyo ya Jinai namba 273/2023 Mtuhumiwa ambaye ni mkazi wa Wilaya ya Temeke Jijini Dar es salaam alikuwa anakabiliwa na shtaka la kuzini na maharimu kinyume na kifungu cha 158(1),(a)cha Sheria ya kanuni ya adhabu,(Sura ya 16 kama ilivyorejewa mwaka 2022).
Mshtakiwa alitenda kosa hilo katika mwaka 2022 na 2023 mwezi Agosti katika eneo la Mbagala Mianzini, wilaya ya Temeke ,Dar es salaam ambapo inaidaiwa alimwingilia kimwili mwanawe wa kumzaa na kumpa ujauzito kisha alimpa dawa za kutoa mimba.