Eh jamani ifike mahali hii hyper ya Diamond itulie. Kila kitu imekuwa ' kwa mara ya kwanza.....' au ' haijawahi kutokea sijui nini ' . Kwanini tunakuwa hivi?
Hizi sifa za kupitiliza ndio zinapelekea hata tunakuwa hatu perform zaidi kwa kulewa ulabu wa sifa.
Hebu maisha yaendelee na tuachane na huu nadiriki kuuitw ' ushamba' na ulimbukeni.
Ni kweli , kwa kiasi kijana anajitahidi ( na wala sina wivu maana huko aliko sio genre yangu kabisa , nina kazi yangu na vipaji vingine) lakini hii sifia ya kila saa mpaka tunakosea kumbe hatuna data za kutosha za nyuma. Mtu unasema ni mara ya kwanza kumbe wewe umeanza kutumia luninga au mtandao si muda mrefu na unafikiri ulichokiona tangu macho yako yamefunguka ndio mwanzo wa dunia/matukio kumbe vitu vipo tu.
Mwisho japo si kwa umuhimu, naomba kusema hivi, kutambulika kidunia ni vizuri lakini kwanini kuendeleza huu utumwa kuwa ukionekana BET au sijui kwenye TV gani umeula? Hivi ni lini tutafunguka akili jamani? Mtu akienda Ulaya , eti kaukata. Akienda Marekani huyo sio mwenzetu. Kwanini isiwe akienda KATAVI? au Tunduru?
Tubadilike.
Na nawatakia siku njema