Jemedari Said: Simba anacheza mashindano bora kuliko Yanga, Magoli yake yana thamani kubwa kuliko ya Yanga

Tusimu-attack mzungumzaji but tuangalie hoja zilizotolewa zina ukweli...???
 
Vigezo vipi unatumia kupata thamani ya goli? Na ni vigezo vilivyo thibitishwa na FIFA au mtu anajiamulia tu?

Udogo wa mashindano unapimwa kwa nini?
Ubora wa timu, timu zinazoshindwa mabingwa ndio zinatupwa shirikisho, mfano Yanga na Tp Mazembe ambao wote walikuwa mabingwa ila wakaboronga wakashushwa daraja
 
Ubora wa timu, timu zinazoshindwa mabingwa ndio zinatupwa shirikisho, mfano Yanga na Tp Mazembe ambao wote walikuwa mabingwa ila wakaboronga wakashushwa daraja
Kwahiyo timu Bora haifungwi?
 
Ile Simba Haina uwezo wa kumfunga yeyote kwenye kundi la yanga,hata kupata sare tu haiwezi
Simba imemfunga Vipers(mbabe wa Mazembe) nje ndani, ndio ingeshindwa hawa vibonde akina na mazembe kweli?
 
Kwahiyo timu Bora haifungwi?
Kipimo pekee cha timu bora ni matokeo ya uwanjani, kama umecheza na timu home and away na kote huko hukuweza kuitoa, maana yake imekuzidi ubora

Au unataka kusema timu za ligi daraja la kwanza ni bora kuliko za ligi kuu?
 
Bado hujanijibu kule juu Vipers alimfunga mazembe magoli mangapi?
Kwa hiyo haikumtoa? Mazembe alitupwa Shirikisho kwa kuonewa?
Yanga mlionewa kwa kutupwa shirikisho pia?
 
Kipimo pekee cha timu bora ni matokeo ya uwanjani, kama umecheza na timu home and away na kote huko hukuweza kuitoa, maana yake imekuzidi ubora

Au unataka kusema timu za ligi daraja la kwanza ni bora kuliko za ligi kuu?
Mbona unaongea vitu irrelevant kabisa sasa maswala ya daraja la kwanza yanatoka Wapi?

Kufungwa kwa timu sio lazima uzidiwe ubora
 
Vigezo vipi unatumia kupata thamani ya goli? Na ni vigezo vilivyo thibitishwa na FIFA au mtu anajiamulia tu?

Udogo wa mashindano unapimwa kwa nini?
Wewe ubora wa timu zilizipo ligi kuu na zilizo ligi daraja la kwanza unapimwa kwa nini? Ukijibu hilo swali una jibu la swali lako
 
Kwahiyo Simba haiwezi kucheza shirikisho.Man United,Arsenal na Barcelona je sio timu bora duniani.wachambuzi wetu wapo kichawa sana kuliko kuwa wachambuzi halisi wa mpira.Muda sio mrefu watu wataacha kuwafatilia wamekuwa mashabiki kuliko kufanya kazi zao.
 
Mbona unaongea vitu irrelevant kabisa sasa maswala ya daraja la kwanza yanatoka Wapi?

Kufungwa kwa timu sio lazima uzidiwe ubora
Ni mfano unaoendana, timu ikifanya vibaya ligi kuu inashushwa daraja, ndio kama CAF ikifanya vibaya ligi ya mabingwa inashushwa daraja na kupelekwa Shirikisho
 
Wewe ubora wa timu zilizipo ligi kuu na zilizo ligi daraja la kwanza unapimwa kwa nini? Ukijibu hilo swali una jibu la swali lako
Hatuongelei maswala ya ligi kuu hapa na hata tukiamua kuyaongelea wewe ulifungwa na mashujaa je walikuzidi ubora?
 
Kwanba mashindano ya Champions League na Confederation yanalingana ubora?
 
Ni mfano unaoendana, timu ikifanya vibaya ligi kuu inashushwa daraja, ndio kama CAF ikifanya vibaya ligi ya mabingwa inashushwa daraja na kupelekwa Shirikisho
Unaelewa maana ya kushushwa daraja?

Yaani unalinganisha ligi yenye mechi zaidi ya 32 na mashindano ambayo ukicheza mechi 12 ushafika fainali?
 
Hatuongelei maswala ya ligi kuu hapa na hata tukiamua kuyaongelea wewe ulifungwa na mashujaa je walikuzidi ubora?
Yote ni mashindano ya mpira ambayo timu ikifanya vibaya inashushwa level ya chini yake, au unataka nikutolee mfano wa UEFA na EUROPA ndio utaelewa, yanalingana ubora yale?
 
Unaelewa maana ya kushushwa daraja?

Yaani unalinganisha ligi yenye mechi zaidi ya 32 na mashindano ambayo ukicheza mechi 12 ushafika fainali?
Unaelewa nini maana ya daraja kwanza? Au unafikiri madaraja yapo kwenye ligi za ndani pekeè?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…