Jenerali Mabeyo: Tulimpoteza Rais Magufuli, tulisimama kidete kama Jeshi kulinda Katiba

jinga kubwa wewe. kila kitu mnaingiza siasa.
Jinga wewe usiyejua kuwa hata jeshi lipo chini ya wizara ya ulinzi inayoongozwa na mwanasiasa…. Muulize CDF kwanini anampigia salute mwanasiasa….
 
Uko sahihi 100%
Huo ni wajibu wao
Hata Sisi walimu tunasimama kidete kuwafundisha wanafunzi
Hatupaswi kusifiwa kwa kufundisha ila tunapaswa kusifiwa kama tukiendesha magari au tukibeba bunduki na kupigania vita
 
Mambo yapo hayo tusiyopaswa kuyajua??
Bunge la Marekani sasa hivi wako kwenye kikao maalum kujadili jinsi Trump alivyotaka kupindua serikali na kila aliyehusika anahojiwa hadharani.
Kwa nini unataka ufafanuzi? Mambo mengine ni siri za nchi na vizuri yabaki kuwa siri za nchi. Wananchi nyie shukuruni nchi ilivuka salama maisha yanaendelea. Siri za nchi, usalama wa nchi waachieni wahusika.
 
chuma hiko bwana!dah mama kiongezee hata mwaka mmoja!!
 
kwani kuna mtu alitaka kuvunja katiba
 
Katiba ya Tanzania ni kifungu gani kinasema Rais lazima awe na degree..

Mbona mbowe hana degree ila anagombea urais ?

Ni wapi Mbowe anagombea urais? Mbowe aliwahi kugombea urais kabla sheria hiyo haijawekwa, kama hujui kitu kaa kimya dogo.
 
Yaani inachekesha na kusikitisha, CDF anasema alikutana na wakati mgumu eti kwa rais kufia madarakani, hivyo akalinda katiba. Ni mara ngapi katiba imevunjwa huku akiangalia? Kimsingi viongozi wa nchi hii wanakaa madarakani kwa kutegemea vyombo vya dola, sasa ni ugumu gani alikutana nao wakati yeye ndio msimamizi wa kiongozi kuingia madarakani?
 
Kwa nini unataka ufafanuzi? Mambo mengine ni siri za nchi na vizuri yabaki kuwa siri za nchi. Wananchi nyie shukuruni nchi ilivuka salama maisha yanaendelea. Siri za nchi, usalama wa nchi waachieni wahusika.

Hamna lolote, ilivuka salama kwenye nini labda? Huo uhuni ndio mnaita siri za nchi?
 
Ahahahah tutajie huyo MTU mkuu
 
Mkuu wa Majeshi ya Ulinzi Tanzania (JWTZ) anayemaliza muda wake, Jenerali Venance Salvatory Mabeyo ametaja kifo cha Rais wa awamu ya tano Hayati Dk. John Magufuli kama moja kati ya changamoto kubwa alizokabiliana nazo katika kipindi cha utumishi wake.

Mabeyo ameeleza hayo katika kipindi cha Dakika 45 kilichorushwa na kituo cha televisheni cha ITV.

Amesema hiyo ilikuwa ni mara ya kwanza kwa Tanzania kumpoteza rais aliyekuwa madarakani hivyo kilikuwa ni kipindi kigumu lakini kama Jeshi walisimama kidete kutimiza wajibu kwa mujibu wa katiba wa kuilinda nchi na katiba.

"Naamini kwamba tunaendelea vizuri, nchi iko salama mpaka sasa. Wananchi wako watulivu, wanaendelea kufuata miongozo kama inavyotolewa na Serikali,” amesema Mabeyo.

Rais Magufuli alifariki dunia Machi 17, 2021, kutokana na matatizo ya moyo jijini Dar es Salaam.

Mkuu wa Majeshi ya Ulinzi na Usalama Tanzania, Venance Mabeyo anatarajia kustaafu wadhifa wake mwisho mwa mwezi Juni, 2022

Mabeyo aliteuliwa kushika nafasi hiyo Februari, 2017 na hayati Magufuli.

Source: #MtanzaniaDigital
 
Nchi hua ina jeshi moja tu. hapa bongo ni JWTZ, hizi nyingine hua ni taasisi, Ila bongo utasikia jeshi la polisi, sijui magereza, mara uhamiaji, mara jeshi usu. Yani kazi kuchanganya watu tu. Siasa mbaya Sana.
kama unaamua kujilisha upepo hata hilo moja utakuja kuona halitoshi kuitwa jeshi.

kama kuna sehemu umesoma jeshi la polisi au magereza linalinda mipaka ya nchi na katiba ndipo uchanganyikiwe.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…