Jenerali Muhoozi Kainerugaba ni dhahiri sasa amelewa madaraka. Ni kweli kwamba hajui madhara ya kauli aliyotoa kuhusu kuivamia Kenya?

Jenerali Muhoozi Kainerugaba ni dhahiri sasa amelewa madaraka. Ni kweli kwamba hajui madhara ya kauli aliyotoa kuhusu kuivamia Kenya?

Nahisi atakua amedukuliwa maana ana tweet upupu tu. Ila kama yupo serious,Wacha tuone ajue sumu haionjwi hata siku moja.
Muhozi kama unafuatilia account yake ya Twitter ni muda mrefu na mara zote huwa anapost ujinga Hadi unajiuliza huyu MTU ana akili.

Nenda kwenye account yake ya Twitter urudi nyumA hata miaka mitatu utaona huwa anapost ujinga tu

Sent from my SM-A032F using JamiiForums mobile app
 
Mkuu T14 Armata Ni ya kweli haya? Mwongozo please
Tuanze na Nigeria na Ethiopia hatusogei. Hata Angola yenyewe hatuiwezi. Unapigana kwa silaha, idadi ya wanajeshi, mafunzo, uzoefu na deployments. Sasa unapiganishaje nchi ambayo iko dormant kwenye ulinzi dhidi ya nchi zenye vita na mikiki mara kwa mara kiasi kwamba wamejipanga.

Kuna sababu kwa nini nchi za NATO huungana kufanya operations hata kama zinapigana na adui dhaifu. Sio unalala tu miaka zaidi ya 30 hakuna hata kamanda mmoja ashacommand unategemea ujue dunia inaendaje kiulinzi.

Huwezi linganisha Kenya inayofanya deployments Somalia, inatuma attack helicopters, inafanya landings, inafanyiwa ambush, inatuma armmoured vehicles zinashambuliwa na maroketi na IEDs, inategua mabomu na kuwa macho kambi zake zisivamiwe na magaidi, inapigwa na adui inalaumiwa na raia kisha serikali inaingia gharama kununua silaha na kufanya mafunzo kuhakikisha suala kama hilo halijirudii. Jeshi kama hilo haliwezi enda sawa na jeshi la nchi iliyotulizana
 
VITA sio mchezo jamani..........hususan kwenye hivi viji nchi duni vya omba omba vya Africa!!!

Huyu kijana amefura kichwa, ameshindwa na cha kufanya, kafika mwisho wa vyeo jeshini, sasa nini tena!

Mimi naona kijana ndie atafyatua huyo babake.........ana uchu sana!!!!
 
Tuanze na Nigeria na Ethiopia hatusogei. Hata Angola yenyewe hatuiwezi. Unapigana kwa silaha, idadi ya wanajeshi, mafunzo, uzoefu na deployments. Sasa unapiganishaje nchi ambayo iko dormant kwenye ulinzi dhidi ya nchi zenye vita na mikiki mara kwa mara kiasi kwamba wamejipanga.

Kuna sababu kwa nini nchi za NATO huungana kufanya operations hata kama zinapigana na adui dhaifu. Sio unalala tu miaka zaidi ya 30 hakuna hata kamanda mmoja ashacommand unategemea ujue dunia inaendaje kiulinzi.

Huwezi linganisha Kenya inayofanya deployments Somalia, inatuma attack helicopters, inafanya landings, inafanyiwa ambush, inatuma armmoured vehicles zinashambuliwa na maroketi na IEDs, inategua mabomu na kuwa macho kambi zake zisivamiwe na magaidi, inapigwa na adui inalaumiwa na raia kisha serikali inaingia gharama kununua silaha na kufanya mafunzo kuhakikisha suala kama hilo halijirudii. Jeshi kama hilo haliwezi enda sawa na jeshi la nchi iliyotulizana
.Katika mtazamo huo wa nchi kuwa 'dormant ' kiasi inapelekea kukosa uzoefu wa kivita,vp kwa South Africa? In tofauti gn na Tz ktk swala la kutopata mikiki mikiki na kutojihusisha na operation za kivita?
 
Mtoto wa Museveni, Muhoozi Kainerugaba anasema haitachukua wiki mbili kwa Uganda kuiteka Nairobi.

View attachment 2376765
Na siku ajaribu,maana nchi ya Uganda ina laana, shida kubwa ni watawala wa nchi iyo wamilikisha watoto wao vyeo vya juu jeshini na kuwapa nafasi nyeti hata KWa Amin yuliyaona,

Sasa ajaribu pale ndo atajua USA yupo apo,atakutana na HIMARS mpaka atajuta,
 
.Katika mtazamo huo wa nchi kuwa 'dormant ' kiasi inapelekea kukosa uzoefu wa kivita,vp kwa South Africa? In tofauti gn na Tz ktk swala la kutopata mikiki mikiki na kutojihusisha na operation za kivita?
Hiyo sio kigezo tu. Switzerland haijawahi pigana vita miaka zaidi ya 200 ila ina silaha kali na budget ya kutosha hadi wameidhinisha kununua F-35 jets. Miaka ya Cold war walikuwa na maandaki ya kuwatoshea raia wote nchi nzima plus 10% ya population kama wageni au ongezeko la ghafla la raia. So walijipanga vikali ingawa hawashiriki vita.

South Africa hata silaha wanatuuzia mfano MRAPs kama za Mamba wanauza kwetu, Uganda, Kenya, West Africa uko. Anti tank missiles kama Mokopa wanauza nje ya Africa na iko very effective. Wameuza anti air missiles kwenye corvette ya Finland. Waliwahi kuwa na Rooivalk attack helicopters wakakosa wateja kimataifa kwa figisu za Marekani. Makampuni yao kama Denel yanauza silaha nyingi tu. Sasa uwalinganishe na sisi.

Ndio maana kazi za helicopters kwenye majeshi ya kulinda amani Afrika mara nyingi wanapewa wao. Wengine wanabaki na infantry tu
 
Huyu kijana nilishataka kuweka uzi humu kuwa kuna siku akipata madaraka anaweza kuja kuzusha vita nyingine, cha kwanza hana hekima wala ustaarabu na cha pili anajiamini kupitiliza na ni mtu wa choko choko
Kama ni kweli Muhoozi kasema hivyo msiwe na Hofu kwani Mwezi Mmoja uliopita Rais Museveni ( Baba yake Mzazi ) aliwaita Marafiki zake Wawili ( Wazee Wawili wa Kitanzania ) sasa ni Wastaafu ila walikuwa wakihidimu Taasisi ya Ikulu na Nyeti Awamu ya Baba wa Taifa Mwalimu Nyerere na katika Mazungumzo yao Mzee ( Rais ) Museveni aliwaomba Wazee hawa Wamuite Muhoozi huku Tanzania waongee nae na Wamkanye juu ya haya ayafanyo kwani hata Baba yake ( Rais ) Museveni yanamkwaza pia.

Kuhusu huyu Mtoto wa Rais Museveni aitwae Muhoozi Kainerugaba kutaka au kutamani kuja kuwa Rais wa Uganda GENTAMYCINE nawahakikishia kuwa hatokuja kuwa Rais kwani Baba yake halitaki hilo na anasema Uganda si Himaya ya Kifalme bali ni Taifa linaloheshimu Utu na Misingi Kisiasa na Kidemokrasia.

Mmoja wa hawa Wazee Wawili ( ambao ni Marafiki wakubwa na wa karibu na Rais Museveni waliolelewa vyema na Hayati Baba wa Taifa Mwalimu Nyerere na hata Muhoozi anawajua kwani walimlea pamoja na Dada yake Natasha walipokuwa wakiishi Upanga Ghorofani jirani na Muhimbil Hospital ) anategemea kwenda nchini Uganda ambapo licha ya kuonana na Rais Museveni ila pia ana appointment ya Kukutana na huyu Kijana Mtoto wa Rais Muhoozi ili kwa Niaba ya Mzee Mwenzake atakayemuacha Dar es Salaam ( Tanzania ) ampe 'Vipande' vyake hivyo huenda akaanza Kubadilika.

Hata hivyo pamoja na Rais Museveni ( Baba yake Mzazi ) leo Kukerwa na akifanyacho Mwanae Muhoozi MImi kama GENTAMYCINE nampa lawana nyingi Rais Museveni hasa kwa Kumpandisha Vyeo vya Kijeshi haraka haraka, kumpa Madaraka hasa Kikosi chake cha Ulinzi SFC ( zamani PPU ), kumruhusu aunde Jeshi lake binafsi la Kumtii ( ndani ya Jeshi Mama ) la UPDF na hivi karibuni Kumteua kama Mkuu wa Kikosi cha Ardhini.

Vitu vyote hivi Rais Museveni alivyomfanyia Mwanae huyu ( Muhoozi ) automatically vilimpa Jeuri na Kiburi Mwanae kiasi cha kuona na kudhani kuwa baada ya Baba yake Mzazi ( Rais Museveni ) Kung'atuka Madarakani anayefaa kuwa Rais ajaye wa Uganda ni Yeye tu Muhoozi.

Nina mengi juu ya hili, hawa ( Rais Museveni na Mwanae Muhoozi) nchi ya Uganda, Siasa zake, machache ila ya Muhimu kuhusuTaasisi zake za UPDF na ile ya CMI na kinachotokea sasa, ila kwa sasa naomba niishie tu hapa tafadhali.
 
nakuomba uivaimie dar uwaue wanajeshì wetu ili na sisi wanume wa shoka tulioko mtaani tupate ajira, mtaan panatisha
 
Back
Top Bottom