Tuanze na Nigeria na Ethiopia hatusogei. Hata Angola yenyewe hatuiwezi. Unapigana kwa silaha, idadi ya wanajeshi, mafunzo, uzoefu na deployments. Sasa unapiganishaje nchi ambayo iko dormant kwenye ulinzi dhidi ya nchi zenye vita na mikiki mara kwa mara kiasi kwamba wamejipanga.
Kuna sababu kwa nini nchi za NATO huungana kufanya operations hata kama zinapigana na adui dhaifu. Sio unalala tu miaka zaidi ya 30 hakuna hata kamanda mmoja ashacommand unategemea ujue dunia inaendaje kiulinzi.
Huwezi linganisha Kenya inayofanya deployments Somalia, inatuma attack helicopters, inafanya landings, inafanyiwa ambush, inatuma armmoured vehicles zinashambuliwa na maroketi na IEDs, inategua mabomu na kuwa macho kambi zake zisivamiwe na magaidi, inapigwa na adui inalaumiwa na raia kisha serikali inaingia gharama kununua silaha na kufanya mafunzo kuhakikisha suala kama hilo halijirudii. Jeshi kama hilo haliwezi enda sawa na jeshi la nchi iliyotulizana